Mwana JF tuambie...

Zamu yangu narudi na chips take away Lizzy. kupika nilifeli hili somo wallahi natafuta mwalimu anisaidie japo chai tu. lol

Hahahaha we mbaya kweli. Yani mwenzio anapika we unamlisha chips tu? Not fair!
 
We zamu yako hua unapika nini?
Dah mwanangu perege ma** umenikumbusha mbali sana....
Kuna mmama mmoja pale kati uswazi alikuwa anapika mida ya saa kumi na moja hivi huyo utamuona na meza lake ikifika saa moja hivi kishamaliza sufulia zima...
Ila mambo ya uswazi bwana si watu wakadai kuwa eti anauza huku yupo uchi (yaani kinguvu za giza)..... so toka ametimuliwa huku uswazi perege hawaliki tena wangu.......
So umeingia kwenye deni kwa kunikumbusha perege wa uswazi lol
 
Hahahaha we mbaya kweli. Yani mwenzio anapika we unamlisha chips tu? Not fair!
asa ntafanyaje lizzy na somo limekaa kushoto. japo ujitolee unifundishe hata kutengeneza ka omlette ili nikitembelewa na wanaJF na mimi nivae kale ka nusu gauni ka jikoni nijifanye niko busy nawaandalia wageni menu kumbe ni kukarangiza mayai ya kisasa tu! ubwabwa wa mate tayri sasa karibuni tule. ubwabwa samaki na mziki wa all 4 one kwa mbaaali.
 
Dah mwanangu perege ma** umenikumbusha mbali sana....
Kuna mmama mmoja pale kati uswazi alikuwa anapika mida ya saa kumi na moja hivi huyo utamuona na meza lake ikifika saa moja hivi kishamaliza sufulia zima...
Ila mambo ya uswazi bwana si watu wakadai kuwa eti anauza huku yupo uchi (yaani kinguvu za giza)..... so toka ametimuliwa huku uswazi perege hawaliki tena wangu.......
So umeingia kwenye deni kwa kunikumbusha perege wa uswazi lol

Hahahahaha. . . . watu wabaya jamani.

Deni lako ntakulipa kwa kukuletea perege fresh out of Nyumba Mungu. We nipe address ya duka la mtaani kwenu tu ntaacha hapo.
 
asa ntafanyaje lizzy na somo limekaa kushoto. japo ujitolee unifundishe hata kutengeneza ka omlette ili nikitembelewa na wanaJF na mimi nivae kale ka nusu gauni ka jikoni nijifanye niko busy nawaandalia wageni menu kumbe ni kukarangiza mayai ya kisasa tu! ubwabwa wa mate tayri sasa karibuni tule. ubwabwa samaki na mziki wa all 4 one kwa mbaaali.
Mbona nyie mnakula vyakula nnavyopenda na nimemiss jamani? Sijui mmeamua kunikomoa? Haya enjoy huo wali alafu nikupe darasa umshangaze hata mate wako hapo siku moja.
 
Mi napumzika baada ya siku ndefu... alafu najipanga kwa usiku mrefu pia unao nisubiri.
 
Mbona nyie mnakula vyakula nnavyopenda na nimemiss jamani? Sijui mmeamua kunikomoa? Haya enjoy huo wali alafu nikupe darasa umshangaze hata mate wako hapo siku moja.
jumatatu ndo zamu yangu, jumamosi na jumapili huwa hatupiki maana tunakula bar na hamna anayekuwepo nyumbani mida iyo, nitaanza kula nikishafikisha post ya 700!
 
Nyie wenye vimiili hivyo huwa hamnitishi kabisa....
Ah hata hivyo nshamaliza ilikuwa bondo la dona kwa samaki wa kukaanga...
Na wewe ulikuwa wapi mda wote huo??

daaah samaki wa kukaanga ukiweka ndimu na pilipili kwa mbali....joune vibaya hivyo hujui kama vitu vizuri unatakiwa u share na wenzio...
 
jumatatu ndo zamu yangu, jumamosi na jumapili huwa hatupiki maana tunakula bar na hamna anayekuwepo nyumbani mida iyo, nitaanza kula nikishafikisha post ya 700!

Basi jifunze kuunga hata mchuzi ili na wewe uwe unapika.
 
Mbona nyie mnakula vyakula nnavyopenda na nimemiss jamani? Sijui mmeamua kunikomoa? Haya enjoy huo wali alafu nikupe darasa umshangaze hata mate wako hapo siku moja.

wanasema a way through a man's heart is through a stomach!! Kweli mapishi ukiyawezea ni raha sana..
 
Kabisa aiseee. Alafu ukiyawezea mapishi utapenda hata kupika, maana unajua mezani watu watalamba sana vidole.
 
Back
Top Bottom