a. Ubalozi/Balozi hashiriki kwa namna yoyote ile si kuwa mlezi, mjumbe n.k awe nje kabisa ya mfumo wa CCM kwani yuko huko kuwakilisha Tanzania na si CCM. Hili binafsi ningependa Ikulu watoe tamko la kuwakataza mabalozi wake kujihusisha na shughuli za chama.
b. Jumuiya za Watanzania zikatae kabisa kuwa sehemu ya vyama vya kisiasa moja kwa moja au kwa implication. Kwa mfano, Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania wote anapokuwa mjumbe wa tawi la Chama chochote cha kisiasa na hivyo kuweza kuleta mgongano wa kimaslahi.
c. Endapo inatokea kuwa wanachama wa chama fulani ndio wengi katika jumuiya zetu basi utaratibu uwekwe wazi na ukubaliwe kabisa kuwa mikutano ya Jumuiya kamwe haitatumika kuzungumzia, kutoa taarifa, kujadili au kwa namna yoyote ile kuyapa nafasi mawazo na hoja za chama hicho hata kama wanajumuiya wote kwa muda huo ni wanachama wa chama hicho.
Vinginevyo, mgongano wa kisiasa utaanza kutokea na kujionesha hasa shughuli za vyama vya kisiasa zitakapoanza kuingiliana na maslahi ya jumuiya nzima ya Watanzania.
Mkuu kale kaibara ka 15 ka chama chetu umekasahau? Au hakatumika ughaibuni?