Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,352
- 1,935
Napenda kuwataarifu kuwa mwana JF mwenzetu, Mzee Shughuli Bwana, amechaguliwa na watanzania wenzake wanaoishi nchini Uholanzi kuwa kiongozi wao. Mzee Shughuli Bwana alichaguliwa kwenye mkutano wa watanzania ulioitishwa na balozi wetu nchini Ubelgiji (unajumuisha pia nchi ya Uholanzi) uliofanyika Jumamosi 17 Mei 2007. Mzee Shughuli Bwana ataongoza kamati ya muda ya kuandaa katiba hadi uchaguzi kamili utakapofanyika ndani ya miezi mitatu.
Hii ni changamoto kwa Mzee Shughuli Bwana maana kapata nafasi nadra ya kutekeleza kwa vitendo yale ambayo amekuwa akiyahubiri sana hapa kuhusu uongozi na utawala bora, hasa kwa kuzingatia kuwa huyu bwana amekuwa yupo mbele sana katika kukivurumishia makombora chama tawala.
Hongera sana Mzee Shughuli Bwana; tunatarajia kuwa utakuwa mwakilishi mzuri wa principles za JF hasa katika kuukataa ubwenyenye na ufisadi!
Kila la heri.
PS: Hii sijui hapa ni mahala pake, kama sio basi MoDs mtanisamehe na kuipeleka panapohusika.