Mwana JF aukwaa uongozi wa watanzania huko Uholanzi

Status
Not open for further replies.
..hongera sana Mzee Shughuli Bwana.

NB:

..hii tabia ya kuwa na matawi ya vyama vya siasa ughaibuni imeanza na CUF.

hata kama imeanzwa na cuf au ccm ni tabia ya kujikomba, mwanaiidi sinare ni mtu wakujikomba kwa kikwete, lakini ajue kuwa watanzania wote walioko uingereza hata kama watakipigia ccm kura hakiwezi kuwa na effect hata ya kunyakua nyumba kumi, hali kadhalika na cuf. tuwe kama wayahudi yaani waisraeli,ifike mahali TUSEME HILI NI TAIFA LANGU, AU UTAIFA WANGU KWANZA,UCHAMA BAADAYE
 
Mimi naamini unaweza kuishi bila ya kujikomba wala kuwa mwizi wa mali za watanzania .Sidhani kuleta vyama nje ya Tanzania kama ni jibu kwa Taifa letu .Nadhani umoja na nia ya kuiendeleza liwe lengo kwetu ndiyo maana JF watu wanapiga kelele za kutaka maendeleo muda wote .
Siamini katika kumwangukia mtu kwa umri huu ila naamini katika Heshima yangu na kuwaheshimu wengine na kuibeba Tanzania kwa nguvu zangu zote .Niko hivi sasa na nimekuwa hivi siku zote za maisha yangu ugenini .Nadhani nikubali kwamba tuwe kama Wayahudi.Tanzania iwe mbele .Vyama vibakie Tanzania .
 
hongera sana mkuu Mzeeshughuli Bwana.kwanza nakupa hongera ya ushujaa wa kutoogopa lolote na umeonyesha umakini wako kwa kukubali utajwe kwa jina lako la JF.kula 5.pili ,naomba uungane na balozi wako kuunganisha watanzania hapo udachi bila itikadi.tatu ,karibu sana toronto ukiwa na muda tule good time
 
hata kama imeanzwa na cuf au ccm ni tabia ya kujikomba, mwanaiidi sinare ni mtu wakujikomba kwa kikwete, lakini ajue kuwa watanzania wote walioko uingereza hata kama watakipigia ccm kura hakiwezi kuwa na effect hata ya kunyakua nyumba kumi, hali kadhalika na cuf. tuwe kama wayahudi yaani waisraeli,ifike mahali TUSEME HILI NI TAIFA LANGU, AU UTAIFA WANGU KWANZA,UCHAMA BAADAYE

Hapo kweli!
Maana hawa ndugu zetu wanachekesha kweli!
Eti CCM imekumbwa na kashfa kubwa ya ufisadi na wao ndio wanafungua matawi ya vyama kwa kasi badala ya kuchukua majukumu ya kuukemea ufisadi!
Sasa hapo kweli mahesabu yao mabaya kwasababu yamegundulika!

Vitendo vyao ni vya kuleta migawanyiko kwasabau nakubaliana na wewe kuwa wao ni CCM kwanza then WATANZANIA baadae...Na wengine tumechoose the other way round and the later being any party!
 
Napenda kumpongeza mwan JF mwenzetu. Ninaamini kabisa Uholanzi hakutakuwa na 'upuuzi' wa UK wa kufungua matawi ya vyama. Watanzania wanahitaji umoja zaidi kuliko kujigawa kivyama.

Nimefurahishwa sana na wenzetu wa US ambao mambo ya vyama hawana isipokuwa wanautana kama Watanzania.

Uholanzi tunatarajia makubwa sana kwenu kwani Uholanzi ni 'strategic country, kwa Tanzania. Watalii wameongezeka sana na biashara ya maua imekua sana.

Kila la kheri Watanzania wa Uholanzi

Thank you Zitto!
 
Asante san Baba Lao
Kuogopa kutotajwa jina basi huo ni uhaini .Nitashirikiana kwanza na Watanzania wa Holland kwanza na Ubalozi pia .Bila kukaa nao karibu hawa wenzetu na kuwaambia ukweli hatuwezi kubadilisha lolote .Uzuri mmoja ni kwamba Balozi Mlay ni mwelewa si kama huko wanako lia UK.Mlay ni straight forward person na hata katika presentation wote tutakubali analilia Tanzania sana .Anatoa mwanga kwa Watanzania kuchukua kazi kokote inakowezekana .Sasa kujificha si neno kabisa .Kukubali kuto kubaliana ni maisha na kwa maana hiyo haiwezi kunifanya niache kusema mawazo yangu iwe hapa ama popote .

Nia namba moja ni Tanzania na Watanzanai wote si zaidi ya hapo .Malengo yako ukiyasimamia mnafanya maajabu wote kama Watanzania .Naamini katika misingi ya usawa na kusema ukweli bila kuumba umba maneno kum appease mtu .Ndiyo maana sauti ilisema Damian mwenyekiti mwa kura zote na Balozi akasema Mr.George watu wanakuamini chukua imani .Nikachukua imani ili niwatumikie na muda wowote wajue niko tayari kusahihishwa .

Ushirikiano ndiyo key factor hapa pia .Kotekote yaani kwa Ubalozi na sisi Watanzanai tunao explore Dunia .
 
Napenda kumpongeza mwan JF mwenzetu. Ninaamini kabisa Uholanzi hakutakuwa na 'upuuzi' wa UK wa kufungua matawi ya vyama. Watanzania wanahitaji umoja zaidi kuliko kujigawa kivyama.

Nimefurahishwa sana na wenzetu wa US ambao mambo ya vyama hawana isipokuwa wanautana kama Watanzania.

Uholanzi tunatarajia makubwa sana kwenu kwani Uholanzi ni 'strategic country, kwa Tanzania. Watalii wameongezeka sana na biashara ya maua imekua sana.

Kila la kheri Watanzania wa Uholanzi

Zitto,kufungua tawi la chama sio upuuzi, ni kuwapa fursa waishio nje kushiriki katika mchakato wa kukiongoza chama husika. Je nyinyi CHADEMA mnadhani watanzania walio ndani ya mipaka ya Tanzania peke yao ndio wanaohitaji kushirikishwa kwa kuwa na matawi ya chama?
Najua mnayaogopa matawi yanayoanzishwa nje lakini kuyaita upuuzi si sahihi hata kidogo, tafadhali omba radhi kupitia hapahapa kwenye Forum.
 
kufungua matawi nje ya nchi na kuwagawa watanzania waishio nje kwa itikadi za vyama ni upuuzi
 
Ndugu waTanzania salaaam, Siku ya Jumamosi jioni Balozi wetu wa nchi za BENELUX (Belgium, Netherlands and Luxemburg) Ndugu Simon Mlay alikutana na waTanzania katika Hoteli ya Crowne Plaza, The Hague. Kwa wale tulioudhulia mjumuiko huo, tutakubaliana kabisa kuwa Balozi wetu alitupokea kwa furaha na uchangamfu usio kifani. Kila mtu alifarijikana charisma yake pamoja na uhuru aliotupa kujichanganya naye mara tulipopata wasaa. Hata sisi tulikuokuwa 'tunamuogopa' kama tulivyomuogopa yule mtumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusadikika ;) tulishangaa kwa jinsi Mheshimiwa alivyojichanganya nasi na kutufanyatujisikie si tu kuwa tuna Balozi, bali pia mlezi wetu wa huku ughaibuni. Kwa kweli ilikuwa mgeni njoo mwenyeji apone :D Kwa sababu hili suala ninalotaka kuliongelea ni suala siriasi, basi naomba niache mbwembwe na kuaddress serious issues seriously. Balozi Mlay alikuja na agenda kadhaa. Baada ya kujitambulisha yeye na ofisa mwingine wa ubalozi aliyeandamana naye - Mama Hyera -, Mh Mlayalitoa muktasari wa yale yaliyomleta Netherland. Balozi pia alituruhusu tumuulize maswali mbalimbali. Mwishoni, Balozi aliangusha agenda muhimu kabisa ya kikao. Kwa miaka mingi waTanzania wanaoishi Netherlands wamekosa umoja ambao unawaunganisha bila kujali kabila, dini, rangi, elimu , status nk. Ingawakumekuwa na jitihada za baadhi ya waTanzania ku-take-initiatives za kutuunganisha kwa kupitia groups mbalimbali, jitihada hizi zimekuwa zikigongamwamba kwa sababu mbali mbali. However hivi karibuni ubalozi wetu wa nchi za BENELUX ulianzisha viguvugu la kuunda Umoja wa waTanzania wa nchi hizi tatu ukiwa na malengo ya kutukutanisha na kushughulikia maslai ya waTanzania wa kanda hii. Jitihada hizi pia zilishindwa kutoa matunda yaliyotarajiwa. Badala yake, ubalozi ukaonelea ni vizuri kwanza kuundwe Associations za waTanzania katika kila nchi na baadae iwe ni raisi kuwaunganisha waTanzania kwa kupitia associations zao. Hizi associations zina nia moja tu - kuwaunganisha na kutetea maslai ya waTanzania palewanapoishi bila kujali rangi zao, dini zao, kabila zao, na hata umri wao. Associations hizi si govermental bali zitapata mibaraka yote ya serikali kupitiaubalozini na Balozi kama mlezi wake (unless voted otherwise). Kwa maana hii, Balozi Mlay alitoa wazo la kuundwa kwa Tanzanians Association hapa Uholanzi na kuhaidi kusaidia katika kutoa mawazo, muundo na ushauri ili hatimaye Netherlands iweze kupata Asssociation yake kama zilivyo nchi nyingine duniani. Kwa kuanzia, Balozi Mlay alitoa nafasi kwa waTanzania walioudhuria kupendekeza majina ya Tanzania Association interim committee ambayo mandate yake ni kukusanya mawazo na kujadili katiba itakayounda Tanzania Association hapa Netherlands. Majina yaliyopendekezwa na kupitishwa ni kama ifuatavyo, Damian George Mwenyekiti Utrech dcgeorge@gmail. comKweba, Bulemo Katibu The Hague Bulemo@gmail. comHarold Sungusia Mjumbe Groningen Haroldsung@yahoo. comJoyce Challe Mjumbe Wageningen Joycechalle@ yahoo.comNasobile Mwakila Mjumbe The Hague ma07080@iss. nl Donald Mmari Mjumbe The Hague odara98@yahoo. comLadslaus Modest Mjumbe Delft ladslaus@yahoo. comConjesta Kabete Mjumbe The Hague Miza Mwinyimbegu Mjumbe The Hague Way forward: - In few days kamati itaanza majadiliano online na baadae kupanga muda muafaka wa kukutana na ku-finalise collected reccomendations kuhusu katiba ya Tanzanians Association.- Mtu yeyote mwenye maoni kuhusu muundo wa katiba ya TA, tutaomba atutumie kwenye anuani zetu kama zilivyo hapo juu (au ajibu email hii as addressed in the relevant forum/s)- Naomba umfikishie mTanzania yeyote (hapa Uholanzi) ambaye labda kwa namna moja au nyingine atashindwa kupata hii email. Mara maongezi ya katiba yatakapokamilika tutawajulisha ili tukutane tena kwa ajili ya kupitisha katiba na pia kuchagua viongozi wakwanza wa Tanzania Association hapa Uholanzi. (wagombea binafsi mkae tayari ;) Siku njema,

Ndugu Kweba, BulemoInterim Secretary Tanzanians Association in The Netherlands.
 
Upuuzi ni kushirikisha wawakilishi wa Rais (mabalozi) katika mambo ya kufungua vyama. Kama Watanzania wanataka kuungana katika chama chochote nje ya nchi wanaweza. Lakini isije kutokea kuwa watanzania ambao wanajulikana kuwa ni wanachama wa chama tawala wanapata ujiko au upendeleo wa aina fulani wanapohusiana na Balozi, au taasisi mbalimbali za serikali.

Binafsi sina tatizo la kimsingi la watu kuwa katika vyama. As long as:

a. Ubalozi/Balozi hashiriki kwa namna yoyote ile si kuwa mlezi, mjumbe n.k awe nje kabisa ya mfumo wa CCM kwani yuko huko kuwakilisha Tanzania na si CCM. Hili binafsi ningependa Ikulu watoe tamko la kuwakataza mabalozi wake kujihusisha na shughuli za chama.

b. Jumuiya za Watanzania zikatae kabisa kuwa sehemu ya vyama vya kisiasa moja kwa moja au kwa implication. Kwa mfano, Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania wote anapokuwa mjumbe wa tawi la Chama chochote cha kisiasa na hivyo kuweza kuleta mgongano wa kimaslahi.

c. Endapo inatokea kuwa wanachama wa chama fulani ndio wengi katika jumuiya zetu basi utaratibu uwekwe wazi na ukubaliwe kabisa kuwa mikutano ya Jumuiya kamwe haitatumika kuzungumzia, kutoa taarifa, kujadili au kwa namna yoyote ile kuyapa nafasi mawazo na hoja za chama hicho hata kama wanajumuiya wote kwa muda huo ni wanachama wa chama hicho.

Vinginevyo, mgongano wa kisiasa utaanza kutokea na kujionesha hasa shughuli za vyama vya kisiasa zitakapoanza kuingiliana na maslahi ya jumuiya nzima ya Watanzania.
 
NA IWE MARUFUKU KWA FAMILIA YA BALOZI KUJIINGIZA KWENYE MAMBO YA KUFUNGUA MATAWI YA CHAMA, KWANI TUNAWEZA KUSEMA KUWA BALOZI HAHUSIKI KUMBE ANAFANYA HIVYO KUPITIA KWA MUME AU MKE, HAPO UINGEREZA KUNA HUYU MTU ANAITWA MAJAAR, HUYU NI MUME WA BALOZI WETU HAPO, HUYU MZEE ANAKUWA KAMA YEYE NDO MWENYEKITI WA CHAMA NA MKE NI RAIS, KAZI YAKE KUFUNGUA MATAWI, JE TUNAWEZAJE KUJUA KUWA KWA UHUSIANO WAKE WA KINDOA NA BALOZI HATUMII RESOURECES ZA UBALOZI KUFANIKISHA UCHAFU HUU?

NI VEMA VYAMA VYA SIASA VIKAJIPANUA NJE YA NCHI KWA KUTUMIA VYAMA RAFIKI, AU KAMA VINA UWEZO VIFUNGUE ORGANISATION CENTRE ZAO HUKO NJE

NI VEMA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA NCHI IKAMKEMEA MHESHIMIWA BALOZI. AU ACHAGUE KUKITUMIKIA CHAMA ARUDI HAPA TZ AENDE DODOMA PALE ATAKITUMIKIA CHAMA MPAKA HAMU IISHE BILA MSHAHARA
 
Mimi nafikiri tumuombe Mhe Zitto awakilishe rasmi malalamiko yetu juu ya familia ya balozi kujihusisha na ufunguaji wa matawi ya CCM Uingereza katika mawasilisho ya bajeti ya wizara ya mambo ya nje katika bunge la bajeti la mwaka huu. Kama italazimika tunaweza kuandika petition ambayo itasainiwa na watanzania wanaoishi nje ambao wanakerwa na tabia ya vyama kufungua matawi. Tumekusanya ushahidi wa kutosha, wa picha na maneno, wa balozi wa Uingereza kushiriki kufungua matawi ya CCM hapa Uingereza na ukihitajika bungeni tutampatia mbunge wa Taifa mhe Zitto auwakilishe huko.

Zemarcopolo: Sio kweli kwamba CHADEMA au chama kingine cha upinzani hakiwezi kufungua matawi nje. In fact kuna wapenzi na wanachama wetu wengi wameomba sana tujibu mapigo ya CCM kwa kufungua matawi huko kote walikopita. Tumekataa. Na sababu yake ni rahisi, nayo ni kuwa hatuamini kwamba kufungua matawi nje ya nchi katika kipindi hiki ni sawa. Tunaamini katika kukusanya nguvu za watanzania wote waliopo diaspora kwa jina moja tu la Tanzania. Tunaamini na tunafikiri ni hivyo kwamba kitendo cha kuanzisha matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi ni cha kuwagawa watanzania na hakifai na kinapaswa kukemewa.

Hii sio sawa na kusema kwamba wana diaspora hawapaswi kujihusisha na siasa za vyama vyao, la hasha. Wanaweza sana lakini sio kwa njia ya kufungua matawi na sio kwa ushiriki wa balozi anayewakilisha nchi.
 
Napenda kumpongeza mwan JF mwenzetu. Ninaamini kabisa Uholanzi hakutakuwa na 'upuuzi' wa UK wa kufungua matawi ya vyama. Watanzania wanahitaji umoja zaidi kuliko kujigawa kivyama.
Nimefurahishwa sana na wenzetu wa US ambao mambo ya vyama hawana isipokuwa wanautana kama Watanzania.

Uholanzi tunatarajia makubwa sana kwenu kwani Uholanzi ni 'strategic country, kwa Tanzania. Watalii wameongezeka sana na biashara ya maua imekua sana.

Kila la kheri Watanzania wa Uholanzi

Kwa nini usipendekeze kufutwa kwa vyama vyote vya siasa hapa nyumbani ili viache kutugawa???
 
Hata wewe unaweza kupendekeza hili.

Kinachogomba hapa ni kuwatumia mabalozi (ambao wanatakiwa kuwa msaada kwa watanzania wote bila kujali vyama vyao) kuwa walezi wa matawi ya ccm.
 
Naomba nami nimpe HONGERA Mzeeshughuli Bwana. Naona Watanzania tulio nje ya nchi tumeshikana vizuri.

Naunga mkono mawazo ya wengi hapa, hasa ya Kitila Mkumbo, kwamba si vema tujigawe kwenye makundi ya vyama vya siasa. Tu wachache, na malengo yetu yanafanana sana. Nguvu za pamoja zinahitajika ili kutokomeza utawala wa kimangimeza na usiofuata sheria.

Tunapambana na mafisadi kwa sasa. Si vema kuanza kupingana sisi kwa sisi, kwa mfumo wa wewe ni CUF, wewe ni CHADEMA, etc. Hili lifanyike nymbani, lakini hapa nje hatutafaidika kuwa na matawi ya vyama. Kwanza wala tusiwe wanasiasa. Zaidi ya hayo ni kwamba uanzishaji wa matawi ya vyama unalenga zaidi kwenye kujikomba kwa wakubwa kuliko kujenga Tanzania. That is beneath most of us.

Siku zijazo huenda tukadai kiti kule Dodoma. Kuna viti vya Watanzania wa majimbo mbalimbali. Sisi cha kwetu kitakuwa cha Watanzania wa Nje. Mzeeshughuli Bwana ataweza kuwa mfunguzi mzuri wa kiti kama hicho.

Augustine Moshi
 
Mimi nafikiri tumuombe Mhe Zitto awakilishe rasmi malalamiko yetu juu ya familia ya balozi kujihusisha na ufunguaji wa matawi ya CCM Uingereza katika mawasilisho ya bajeti ya wizara ya mambo ya nje katika bunge la bajeti la mwaka huu. Kama italazimika tunaweza kuandika petition ambayo itasainiwa na watanzania wanaoishi nje ambao wanakerwa na tabia ya vyama kufungua matawi. Tumekusanya ushahidi wa kutosha, wa picha na maneno, wa balozi wa Uingereza kushiriki kufungua matawi ya CCM hapa Uingereza na ukihitajika bungeni tutampatia mbunge wa Taifa mhe Zitto auwakilishe huko.

Zemarcopolo: Sio kweli kwamba CHADEMA au chama kingine cha upinzani hakiwezi kufungua matawi nje. In fact kuna wapenzi na wanachama wetu wengi wameomba sana tujibu mapigo ya CCM kwa kufungua matawi huko kote walikopita. Tumekataa. Na sababu yake ni rahisi, nayo ni kuwa hatuamini kwamba kufungua matawi nje ya nchi katika kipindi hiki ni sawa. Tunaamini katika kukusanya nguvu za watanzania wote waliopo diaspora kwa jina moja tu la Tanzania. Tunaamini na tunafikiri ni hivyo kwamba kitendo cha kuanzisha matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi ni cha kuwagawa watanzania na hakifai na kinapaswa kukemewa.

Hii sio sawa na kusema kwamba wana diaspora hawapaswi kujihusisha na siasa za vyama vyao, la hasha. Wanaweza sana lakini sio kwa njia ya kufungua matawi na sio kwa ushiriki wa balozi anayewakilisha nchi.

Sioni tatizo la chama kufungua tawi na kama ulivyoelezea itikadi yenu haiko evidence based, anyway mimi kilichonigusa ni lugha aliyoitumia Zitto - upuuzi -nina uhakika unakumbuka kuwa lugha aliyoitumia Zitto bungeni iliwahi kuwa mwanya wa kuzuiliwa kwa hoja yake na yeye mwenyewe kufungiwa.

Language matters na bado naamini kuwa Zitto anapaswa kuomba radhi kwa lugha aliyotumia hapa.

Jitihada za kuendeleza nchi zinaweza kuwa za aina mbalimbali na si sahihi kwa watu wa itikadi fulani kuamua kutumia lugha kama aliyotumia Zitto katika kuonyesha kuwa hawakubaliani na njia inayotumiwa na wengine.

Tukiwa na lugha isiyoonyesha jazba then tunaweza kuendelea kujadili jinsi matawi hayo yanavyonufaisha au kudhoofisha juhudi za maendeleo.

Lugha ya kisilani inazuia mijadala pevu.Ndio maana ninawawakilisha watu wa UK waliofungua matawi ya CCM kumjulisha Zitto kuwa kuomba radhi kwake ndio njia itakayowezeha mijadala pevu, iwapo at all anahitaji mijadala pevu.
 
ingekuwa vizuri kama nyie watu wa UK mngemmwambia Mwanaidi awaombe radhi watanzania kwani anatumia pesa za walipa kodi ambao si wanaCCM kufungua matawi ya ccm huko UK. Ametumwa kuliwakilisha taifa na si ccm. Je ufunguzi wa hayo matawi ya ccm huko UK ni moja ya Terms za reference kwa katika majukumu yake kama balozi, na kama ni hivyo basi aencourage na cuf na chadema na vyama vingine vifungue matawi huko to make her sound with more non sense.
 
Sioni tatizo la chama kufungua tawi na kama ulivyoelezea itikadi yenu haiko evidence based, anyway mimi kilichonigusa ni lugha aliyoitumia Zitto - upuuzi -nina uhakika unakumbuka kuwa lugha aliyoitumia Zitto bungeni iliwahi kuwa mwanya wa kuzuiliwa kwa hoja yake na yeye mwenyewe kufungiwa.

Language matters na bado naamini kuwa Zitto anapaswa kuomba radhi kwa lugha aliyotumia hapa.

Jitihada za kuendeleza nchi zinaweza kuwa za aina mbalimbali na si sahihi kwa watu wa itikadi fulani kuamua kutumia lugha kama aliyotumia Zitto katika kuonyesha kuwa hawakubaliani na njia inayotumiwa na wengine.

Tukiwa na lugha isiyoonyesha jazba then tunaweza kuendelea kujadili jinsi matawi hayo yanavyonufaisha au kudhoofisha juhudi za maendeleo.

Lugha ya kisilani inazuia mijadala pevu.Ndio maana ninawawakilisha watu wa UK waliofungua matawi ya CCM kumjulisha Zitto kuwa kuomba radhi kwake ndio njia itakayowezeha mijadala pevu, iwapo at all anahitaji mijadala pevu.

Wewe ndiye unahitaji kuomba msamaha hapa kwa kumwaga pumba kama hizi hapa JF. Kutumia pesa za serikali na nafasi ya ubalozi (muda) kufungua matawi ya vyama vya siasa ughaibuni ni upuuzi na Zitto yuko right kusema hivyo.
 
I cant teach you what to believe, ngoja tuone Zitto mwenyewe ana nini cha kusema juu ya hili.
Msisahau kuwa forum sio mahali pa ushabiki na kuitana pumba au kusifiana bila kuchanganua.
 
Nani anataka kufundishwa na wewe? Unaonekana fisadi tu kwa kutetea matumizi ya muda na nafasi ya balozi kufungua matawi ya ccm ughaibuni. Nimekuita kuwa una pumba, je una tatizo na hilo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom