MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

chief ihunyo high school anaepafahamu plz. tujuzane.
 
Ni vema ukaweka wazi ni sehemu gani ya Tandahimba unaiulizia. Ila swali lako ni la ujumla sana. Kuhusu umeme upo ktk vijiji vilivyopo ktk Barbara ya Tandahimba-Newala ila vya ndani bado. Na kuhusu maji sehemu kubwa ya wilaya hii yana shida kubwa ya maji ukiondoa maeneo yanayopakana na mto Ruvuma.

waifahamu shule ya Nandonde? Ipo wapi hapo Tandahimba
 
Nmepangwa kufundisha shule ya utengule mbarali mbeya, naombeni kujuzwa sifa za eneo hili wakuu

Utengule Usangu sec ndio nyumbani maeneo hayo.
Ni mbali kidogo kutoka mby mjini maana ipo mbali na barabara kuu., maji na umeme ni changamoto kidogo
Ila pamechangamka sana na hakuna shida ya misosi. Kama unatokea kokote kule shukia Mswiswi au Igurusi then ulale hapo afu kama ni mswiswi utapanda bodaboda mpaka shuleni, kama ni igurusi nahis vipo vicanter. kama kuna la zaidi ni pm.
 
duh.. kakonko! aende tu na nguo za kawaida sana kama ana pamba kali aziache tu.
kule sharti ufanane na wenyeji ukiwazidi radi inakuhusu.
masuala ya kuchapa watoto asahau.
usalama ni 0 kabisa majambazi kutoka burundi wanavamia na kufuata walimu. wanateka haice au kigrosari na silaha nzito sana. r.p.g mashine.
pia kuna masuala ya kuwekeana sumu sana asiwe anapenda kula vimigahawani hata ka hana kisa na mtu huwa wana tabia ya kufanya majaribio kama sumu inaua.
wake za watu/waume za watu..na zaidi ya sumu.
awe charming kiasi.

kwa ujumla si pazuri mkuu manake unaishi kwa wasiwasi sana.
my take. waha si watu wazuri kwa kweli ni watu wenye ukarimu na lugha laini lakini moyoni anawaza atakuuwaje.
wayungu dah..

Nimecheka weeee mpaka nahisi njaa
 
Utengule Usangu sec ndio nyumbani maeneo hayo.
Ni mbali kidogo kutoka mby mjini maana ipo mbali na barabara kuu., maji na umeme ni changamoto kidogo
Ila pamechangamka sana na hakuna shida ya misosi. Kama unatokea kokote kule shukia Mswiswi au Igurusi then ulale hapo afu kama ni mswiswi utapanda bodaboda mpaka shuleni, kama ni igurusi nahis vipo vicanter. kama kuna la zaidi ni pm.

Nashukuru sana mkuu, je naweza kukaa maeneo jirani yenye umeme? Huku nafundisha utengule?
 
jamani naombeni ushauri nimepangiwa ruvuma mbinga shule inaitwa nanswea now nipo feza boys naombeni mnisaidie mazingra kwa aneye fahamu

kaka nanswea IPO bush saaaanaa..hakuna umeme barabara tope KWA nasika hayaaa...ni km kama 30 toka mbnga mjini...so jipangee vzr na usafir wake ni ndoki au Kenta au tipa
 
ha ya jamani anaeifahamuu KWA undani Wilaya ya Kilindi mkoani tanga
 
Naombeni msaada ndugu zangu NJECHERE SECONDARY SCHOOL iko wapi hapa Dar es salaam
 
wadau ni kweli kwamba unaweza kukaa dar maeneo ya kimara au mbezi huku unafanya kazi kibaha? naombeni details kwa anayefahamu kiwango cha nauli na umbali
 
Naombeni msaada mwenye kufahamu should ya sec mabui iliyoko Musoma vijijini, je huduma za kijamii zipoje? umbali toka mjini upo vp? umeme, shugjuli za kiuchumi kijijini n.k . Dadaangu kapata kituo cha kazi leo ktk shule hiyo. Asanteni
 
we mwambie akapige kazi bana...una ulizia huduma za kijamii unadhani huko hakuna wanaoishi!na kwa mazingira yalivyo lazima ataolewa na mtendaji wa kijiji nakwambia!
 
we mwambie akapige kazi bana...una ulizia huduma za kijamii unadhani huko hakuna wanaoishi!na kwa mazingira yalivyo lazima ataolewa na mtendaji wa kijiji nakwambia!

Akili na mawazo ya namna hii hua nayaita ni mawazo yenye utapiamlo; huna tofauti na akili ya mtoto wa chekechea.

unadhani sijui kama huko wanaishi watu? Nauliza nipate mwangaza zaidi in reflection to environment. Hatuishii tu kufanya kazi ya serikal bali tunayatumia mazingira tunayoishi kujiongezea maendeleo binafsi.

Yaani hata hili unahitaji elimu ya kurusha Rocket??? Half knowledge is very dangerous!!
 
Aende tu ajionee kama ana option ya kufanya ataamua baada hapo.
 
Shule inaitwa mabuimerafuru,ni kijijin,hakuna umeme.atapanda gari za majita hd njia panda ya mabui kisha boda hd huko.
Namtakia kila la kheri,ajiandae na udongo mwekundu wa mfinyanzi.
 
Back
Top Bottom