MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

We njoo tu kiongozi,yote utayafahamu huku huku.

Kwa ujumla pako njema,fursa kibao za kiuchumi.

Karibu sana,ukifika nitafute.
 
huku ni ugali wa muhogo na samaki nchanga kwa kwenda mbele, umeme utoke wapi porini huku labda wilayan ndo upo kwa 20%
 
Tandahimba..
Kuna basi limeandikwa TANDAHIMBA... kakomae tu.
 
Msaada kwa anaepafahamu wilaya ya buhigwe kigoma
 
Mimi navyoifahamu Kakonko Ni wilaya mpya ilogawanywa kutoka wilaya ya kibondo waha wakule wanaitwa wayungu jumbo la buyungu maana kibondo INA waha wahambwe, Kakonko hamna shida sana kama kibondo shifa kubwa kule Ni kulishana sumu tu kuua kwa sumu Ni jambo la kawaida iaipokua usile kwa vijimigahawa, pika mwenyewe .ila hamna benki hadi kibondo, hamna umeme bado , na maji Ni shida shida ila ukifika utazoea utapapenda sana utapata mashamba ya kulima mazao ya biashara, nenda bhana lie pia nipo Kakonko ila nipo idara ya afya Ni c.o tutakua pamoja
 
Karibu sana kakonko na usitishwe na maneno ya watu,kakonko ya dhamani si kama ya sasa.
Ni kweli kakujaendelea sana,ila kama sehemu zingine napo panapa maendeleo.

Mfano umeme umefika sasa kutoka kibondo.

Pil lami imeanza kujengwa kutoka nyakanazi,hvyo muda si mrefu itakamilika.

Mengine hata ungekuwa dar es salaama yangekukta,jaribu kuyaepuka.

Karibu sana,japo sipo kakonko.
 
Naomba mnijuze juu ya wilaya ya rorya pakoje, hasahasa shule ya raranya sec.
 
Yani nunua jembe, panga, shoka, sumu ya mamba na kama unasmartphn bora uuze ununue nokia ya torch, yani huko ni shida
 
Tandahimba pako poa tu ila vijijini kuna simba bana wakati wa mvua wanatapakaa kama ng'ombe au mbuzi
 
Bunda ni wilaya iliyopo mkoa wa Mara pako safi,maji yapo na vijiji vingi usafiri upo pia umeme upo maeneo meng.Kama unatokea mikoa mingine ukifika Mwanza panda magari yanayoenda Mwanza au Tarime yote yanapita Bunda ukifika watakushusha.Nenda kalitumikie taifa mwalimu.

hizo ni sifa za bunda mjin ukitoka kidogo tu shiida. nimeish serengeti hivyo mara nzima nimeitembelea du usiache nyumban kisu vuta bange kwanza ndo mtawezana
 
Sio mbaya, itabidi uende mpaka shirati, halafu uwaulize wenyeji lazima kuna usafiri wa kwenda huko. Ni vizuri ufike mapema.
 
We nenda mkuu lakini bukoba vijijini mhhh kuna baadhi ya sehemu ziko powa lakini nyingine majanga,,,maana unaweza pelekwa huko bugabo,kasharu hayo ni baadhi ya maeneo ambayo ni mabovu saaana,

Mungu apishie mbali huko.
 
Tandahimba vijiji vingi vilivyopo pembezoni mwa barabara ya mtwara ,tandahimba mpk newala vina umeme ila maji shiiiida, zao la korosho ndio linalimwa kwa wingi, so kapge mzigo unaweza ukajipigia hela kwa kudeal na korosho, jiandae lilac ming'oko
 
Back
Top Bottom