MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

MWALIMU: Uliza kuhusu kituo ulichopangiwa

usijali ndugu we ukiwa na shida ni pm tu haina haja ya namba.
maeneo mengi ya moshi dc ambayo ndo inaitwa vijijin ni maeneo condusive sana utakuta barabara, umeme maji ni shida kidogo maeneo ya ukanda wa chini namaanisha ukiwa unatoka dar mkono wa kushoto ndo pabaya kidogo. ila maeneo kama marangu, kibosho, uru, old moshi , himo, njiapanda, waweza ishi mkuu na ndizi kibao. hamna eneo ambalo halina usafir/ kabisa .

watu wa huku nmependa ni wajanja watakufanya uchangamke sio kuzubaa hovyo hela utaitafuta tu. ukitaka kwenda masomoni baada ya miaka miwili unaenda.

mf. mi nlianza kazi 2012 mwaka jana nmepata ruhusa . ni wilaya ambayo ina waalimu walosoma sana na wengi kuliko wilaya zote kilimanjaro utashangaa kwa mwaka watu wanaoomba wakasome masters ni wengi waalimu wengi from primary wana degree sekondari masters kibao lazima akili itacharge faster karibu



Much love,mkuu..
 
Mdogo wangu amepangwa huko ualimu sekondari, je mazingira kwa ujumla yapoje?umbali upoje kutoka Arusha mjini? hali ya hewa pamoja na shule za karibu ni zipi?

karibuni wadau...

mwambie tubadilishane aje sengerema mwanza niende huko
 
Sina hakika sana na maisha uliyolelewa na kukulia zaidi kwa upande wa lugha ila naona lugha unayotumia ni ngumun kwa mtu kama mimi..Nisamehe bure ndugu yangu ila kila mmoja ana interest zake hivyo huwezi mfanya mtu ajione mjinga kwa vile hataki tu kukaa Moshi..

njoo sengerema mwanza
 
Napenda kuwapongeza kwa bahati mliyonayo kupata wilaya nzuri.Napenda kuwatoa hofu maisha ya kahama hasa hasa tc shule zote za sekondari zipo karibu na mjini iliyopo mbali kabisa ni maili tisa ambayo ni Bukamba sec na barabara inapitika majira yote na ipo mita 200 kutoka barabara kuu ya kwenda tabora.Kwa mwenye duku duku au swali kuhusu shule na mji wa kahama aniulize

Mkuu mimi nimepangwa halmashauri ya Msalala ambayo mwanzo nackia ilikuwa ndani ya kahama. Vipi unazifahamu baadhi ya shule za sekondari zilizopo ndani ya halmashauri ya Msalala? Km unazijua plz naomba unisaidie kunipa ABC za shule hizo
 
Mkuu mimi nimepangwa halmashauri ya Msalala ambayo mwanzo nackia ilikuwa ndani ya kahama. Vipi unazifahamu baadhi ya shule za sekondari zilizopo ndani ya halmashauri ya Msalala? Km unazijua plz naomba unisaidie kunipa ABC za shule hizo

Karibu Msalala' wilaya hii ni mpya ina shule za secondary zifuatazo:Isaka sec, Jana sec, mwaluguru sec, Bulige, Bugarama, Bulyahulu, mwl nyerere, Ngaya, Busangi, Lunguya, Ntobo..nyingne 4 Nmezsahau' lakin ktk hizo zote Isaka sec ipo mahali pazuri mno' ipo isaka dry port hapo international road inapita na n km40 kufka kahama mjin' hizo nyingne barabara zinafika lakkin si za lami' Karibu Msalala
 
Msalala ni kahama vijijini japo kuna miji midogo ambayo ndipo shule za sekondari zimejengwa baadhi ya sehemu zilipo shule ktk halmashauri ya msalala ni is aka,segese,chela nk.cha ajabu tu shule za huko wanafunzi ni wachache.mbunge wako ni Ezekiel maige
 
Bukombe to kahama nauli ni 4000-5000 baadhi ya shule zipo pembezoni mwa barabara ya kimataifa ya kwenda Rwanda na Burundi kilimo ndo mpango mzima kwa wilaya hiyo
 
Bukombe to kahama nauli ni 4000-5000 baadhi ya shule zipo pembezoni mwa barabara ya kimataifa ya kwenda Rwanda na Burundi kilimo ndo mpango mzima kwa wilaya hiyo

Umesahau madini mkuu (dhahabu)
 
kama umepangwa Moshi vijijn ni pm nkusaidie Mwl
 
Tandahimba ni moja kati ya wilaya tano Tanzania yenye uchumi mkubwa. Karibu 60% ya korosho zote zinazozalishwa Tanzania zinatoka wilaya ya Tandahimba hivyo uchumi wa mtu mmoja mmoja ni mkubwa sana. Ni wilaya changa ambayo zamani ilikuwa ndani ya wilaya ya Newala lakini imepiga hatua sana kimaendeleo. Ni kilometer takriban 90 kutoka mtwara mjini. Karibu kwa wamakonde ni wakarimu ila masikini jeuri.

Asante Mkuu
 
rafk yang kapangiw huko..plz anaomba msaad japo wa taarf chache yaan pakoje,?
 
Ni wilaya iliyogawanyika kutoka Kibondo. Sehemu kubwa inapakana na nchi ya Burundi, na game reserve ya Mwaiwosi. Ni sehemu nzuri . Inapakana na Biharamuro, Ngara na si mbali kufika Kahama
 
Ni wilaya iliyogawanyika kutoka Kibondo. Sehemu kubwa inapakana na nchi ya Burundi, na game reserve ya Mwaiwosi. Ni sehemu nzuri . Inapakana na Biharamuro, Ngara na si mbali kufika Kahama

hapo saf..but ndo ilvyo lazma kwend kulinga hakuna ten
 
Back
Top Bottom