Tandahimba ni wilaya inayopatikana Mkoa wa Mtwara, unapotaka kwenda waweza panda mabasi ya Dar-Tandahimba mfano wa basi ni TANDAHIMBA XPRESS (Bovubovu hivi) au upande basi linaloenda Masasi kutokea Dar then shuka Mtama (Kwa Bwana Mkubwa) hapo utapata mabasi ya huko, changamoto ya huko ni barabara mbovu tu ndo maana hata mabasi yanayokwenda huko ni yale ya tripu moja Dar Tripu gereji.
Kuna mabasi yanaanzia pale Mbagara 3rangi yanaenda mpaka huko, mojawapo ni Tandaimba express na lingine ni Tembo express kama sikosei.
Halafu,changamoto kubwa ya Tandahimba ni Barabara tu,ni wilaya Kongwe ila duuuuuh...................
Asante sanaa Mkuu
Tandahimba sio wilaya kongwe, haina hata miaka mingi iliundwa 1995 kama sikosei