Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,840
- 59,524
Habari zenu jamani?!
Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.
Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!
Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!