Miaka ya 90 Mwl. Nyerere alikiri kukosa imani na CCM

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,816
6,436
Kuna Kitabu cha Hayati Mwl. Nyerere kinaitwa UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA, 1994.

Inasemekana baada ya Mwl kutokuridhika na Uongozi wa CCM miaka ya 90 wakati wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, aliandika Kitabu chenye title hiyo hapo juu.

CCM ilipogundua hili, mamlaka zinazohusika zikazuia Kitabu hicho kisichapwe Tanzania na wale Wachapaji wa Mkuki na Nyota, ikabidi Mwl akakichape Zimbabwe kwa Zimbabwe Publishing House.

Alipokileta nchini tayari kwa usambazwaji, Serikali ikahujumu zoezi. Mwl akafariki mwaka 1999, mwaka 2010 Serikali ikachapisha TOLEO LA KIZAZI KIPYA ambalo lilifuta baadhi ya maudhui ya TOLEO HALISI la mwaka 1994.

Kwenye hicho Kitabu Mwl anakemea kuhusu kansa iliyomo ndani ya Uongozi wa CCM, ambayo inakitafuna Chama kizima; na kusisitiza kwamba angekihama Chama cha Mapinduzi kama angeona mbadala wa Chama cha upinzani chenye sera nzuri.

Zaidi zaidi anasema CCM inaweza kuendelea kuchaguliwa na wananchi kwasababu ya uzito wa historia yake, au inaweza ikafika pahala wananchi wakachoka wakasema potelea mbali, wakachagua chama kingine chochote cha upinzani, ili mradi tu waepukane na kansa ya Uongozi mbovu wa CCM.

Mwisho, Mwalimu anakiri kuwa Rais Mwinyi alikuwa kiongozi mpole lakini dhaifu. Akanawa mikono kwamba ameshatutahadharisha, anawaachia viongozi walipo madarakani wafanyie kazi maoni yake kwasababu yeye ameshang'atuka.

Kwahiyo yote yanayotokea sasa Mwl alishayatabiri.

Soft copy ya Kitabu hicho (TOLEO HALISI) imeambatanishwa kwenye uzi huu. Utamu unapatikana kuanzia ukurasa wa 35 na kuendelea. Karibuni.View attachment Kitabu-Uongozi_wetu_na_Hatma_ya_Tanzania-JK_Nyerere.pdf
 
Kuna Kitabu cha Hayati Mwl Nyerere kinaitwa UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA, 1994.

Inasemekana baada ya Mwl kutokuridhika na Uongozi wa CCM miaka ya 90 wakati wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, aliandika Kitabu chenye title hiyo hapo juu.

CCM ilipogundua hili, mamlaka zinazohusika zikazuia Kitabu hicho kisichapwe Tanzania na wale Wachapaji wa Mkuki na Nyota, ikabidi Mwl akakichape Zimbabwe kwa Zimbabwe Publishing House.

Alipokileta nchini tayari kwa usambazwaji, Serikali ikahujumu zoezi. Mwl akafariki mwaka 1999, mwaka 2010 Serikali ikachapisha TOLEO LA KIZAZI KIPYA ambalo lilifuta baadhi ya maudhui ya TOLEO HALISI la mwaka 1994.

Kwenye hicho Kitabu Mwl anakemea kuhusu kansa iliyomo ndani ya Uongozi wa CCM, ambayo inakitafuna Chama kizima; na kusisitiza kwamba angekihama Chama cha Mapinduzi kama angeona mbadala wa Chama cha upinzani chenye sera nzuri.

Zaidi zaidi anasema CCM inaweza kuendelea kuchaguliwa na wananchi kwasababu ya uzito wa historia yake, au inaweza ikafika pahala wananchi wakachoka wakasema potelea mbali, wakachagua chama kingine chochote cha upinzani, ili mradi tu waepukane na kansa ya Uongozi mbovu wa CCM.

Mwisho, Mwalimu anakiri kuwa Rais Mwinyi alikuwa kiongozi mpole lakini dhaifu. Akanawa mikono kwamba ameshatutahadharisha, anawaachia viongozi walipo madarakani wafanyie kazi maoni yake kwasababu yeye ameshang'atuka.

Kwahiyo yote yanayotokea sasa Mwl alishayatabiri.

Soft copy ya Kitabu hicho (NAKALA HALISI) imeambatanishwa kwenye uzi huu. Utamu unapatikana kuanzia ukurasa wa 35 na kuendelea. Karibuni.View attachment 2743907
Yeye rais asiye mpole na dhaifu aliwafanya watz wapange foleni kununua unga,na makalioni suruali zenye viraka
 
Huyo jamaa bado tu mna mtukuza ?

Jamaa alipenda kukosoa wenzake ila yeye kukosolewa kidogo tu anakupaka mavi nchi nzima na joto la jiwe utaliona, ukimbie nchi au upotezwe.

Michezo yote michafu ya CCM unayo iona sasa imeanzia kwa huyo huyo.
 
Inawezekana.

Lakini unaonaje tukijikita kwenye hoja badala ya kumfanyia Hayati J.K Nyerere personality assassination?
 
Back
Top Bottom