Kigoda cha Mwalimu Nyerere okoa mustakabali wetu

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Ulinzi wa rasilimali za nchi ni jukumu la nani?

Kuna mjadala mpana na makini unaendelea duniani juma hili huku duru mbalimbali zikitilia shaka ujio wa ndege kubwa ya mizigo iliyotua uwanja wa ndege wa KIA.

Licha ya ufafanuzi kutolewa, bado imeonekana kwenye umma kuna ombwe la kutoridhika na ufafanuzi wa uongozi wa uwanja wa KIA kuhusiana na ujio huo.

Awali ya yote, tunapojadili hili, ieleweke kwamba kuna ulinzi wa mipaka ya nchi na ulinzi wa rasilimali za nchi. Hizi ni dhana mbili tofauti.

Wakati wa kuchangia mada zingatia ukweli wa tofauti kati ya ulinzi wa mipaka na ulinzi wa rasilimali.

Kiini cha Mada.

Enzi za utawala wa Mwl. Nyerere, alizisuka taasisi mbalimbali zikiwemo vyuo vikuu kuwa chemichemi za mawazo na dhana chanya za kuchagiza mustakabali wa nchi na Afrika kwa ujumla wake.

Taasisi hizi zikawa mbwa-doria (watchdogs) ambazo zilisaidia pia udhibiti wa utendaji mbovu kwa kuzalisha wataalam mahiri lakini pia kufuatilia na kuchagiza utendaji makini serikalini, zikisaidiana na Mihimili kuiweka nchi kwenye mstari stahiki kulingana na falsafa ya taifa.

Zaidi, taasisi hizi zikawa wapiganaji wazuri wa kupatikana ukombozi wa Afrika na walinzi imara wa uhuru wake, zikitumia silaha mahiri za taaluma, maarifa, mijadala-pevu, migomo na machapisho mbalimbali.

Viongozi walioko kwenye hatamu leo, walikuwa wanafunzi kwenye vyuo hivyo enzi hizo na walishiriki harakati hizo kwa umahiri wa kiwango cha juu kabisa usiotiliwa shaka; kiwango ambacho kilikuja kuwapa sifa za kuwa viongozi wa leo.

Leo mambo yanapoenda ndivyo sivyo pasina wao kuibua vita dhidi ya maovu haya je, nchi na dunia ziwachukulieje? Je, ni wao kweli walewale walioshiriki harakati hizo wakiwa vyuoni?

Kipi kimewasibu leo (hata wasiweze kuokoa mustakabali wa nchi na Afrika) ambapo wana dhamana kubwa kubwa kuliko nyakati zile walizokuwa wanafunzi tu?

Ina maana walipokuwa wanafunzi bila mamlaka rasmi kiserikaki walikuwa na nguvu kubwa kuliko leo wanapokuwa viongozi na mamlaka makubwa namna hii?

Je, taasisi hizi e.g. UDSM, SUA, MZUMBE, Mwl. Nyerere Academy (zamani Chuo cha Itikadi Kivukoni), Chuo cha Diplomasia Kurasini nk zimefungwa vinywa? kwanini zimekubali kufungwa vinywa?

Au kilichowafunga vinywa ni udahili wa wanafunzi wasiojuwa historia ya nchi na wasio na ragba (interest) ya kujuwa mustakabali wa nchi bali waliotingwa tu (mbali na taaluma) na siasa za Simba na Yanga na Mondi na Konde boy na Joti na Umiss Tz?

Kigoda cha Mwalimu Nyerere okoa mustakabali wetu na Afrika.

Mwl. Nyerere Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.

Benjamin William Mkapa Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.

Jakaya Mrisho Kikwete Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.

Taasisi za elimu ya juu zimepoteza dira katikati ya kilindi cha bahari kuu, chombo kinahitaji uokozi.
 
Mambo yamebadilika itabidi Kuna watu wazikwe kwanza ndo tupumue maana wanafanya mambo ya nchi kama famili yake
 
Zimebaki taaisis za Uchawa tu
 
UDSM hii hii iliyojaa udini, ubaguzi na hata kurogana hii ndiyo iwe mbwa-doria? Majitu yamesoma lakini roho mbaya na ushirikina utafikiri hayajaenda shule?

Wasomi wetu wapo bize na uchawa ili walambishwe asali. Sasa watamfanyia doria nani?
 
Mwl. Nyerere Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.
Ndio Foundation ya Kweli Tanzania.
Inachokosa: Kiongozi
...na ilianzishwa kwa Malengo mazuri.
Suggestion: Board of Directors Director- Mwanae.

Benjamin William Mkapa Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.
Foundation mahiri iliyoanzishwa kama kioo Cha Nyerere Foundation

Kimekosa Viongozi mahiri.
Sababu: Mwenyewe alikuwa anajua kuendesha Mwenyewe

Lengo lake halikueleweka
Suggestion: Board of Directors Director- Mwanafunzi atakaye fuzu Vizuri Chuo cha Waandishi. Pascal .M perhaps

Jakaya Mrisho Kikwete Foundation okoa mustakabali wetu na Afrika.
Ilimradi tu ipo na Jina
Ilianzishwa kwa msukumo wa Rafiki Blair kama sikosei

Uongozi wake una walakini walakini
Suggestion: Kije kiendeshwe na Mwanae, baada 2025

Lengo lake: Kukusanya viroba kwa namna yeyote vile ilimradi CCM -Alwatan washinde

Inafanana fanana na yule wa "Lock her Up"

Zaidi ya mbili za Kwanza, zingine zote ni maigizo.

Hayo ni maoni yangu. Hayana kichwa wala miguu.

Disclaimer: Nimekurupuka kwa kukosa weledi wa Bandiko. Hivyo basi Majina kama yanafana fanana haimanishi ndio hao tajwa.

Mungu nisaidie.
I meant, Kibatalla Nisaidie.
 
Kigoda cha Mwalimu Nyerere okoa mustakabali wetu na Afrika.
Wakati Prof. Issa Shivji akiwa Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, nilimtafuta kumuuliza kuhusu udikiteta Tanzania, angalia nilichojibiwa Gwiji wa Sheria na Katiba, Prof. Issa Shivji, Agoma Kuzungumzia Dhana ya Udikiteta/Uvunjifu Katiba!, this means, it depends on who is sitting on the driver's seat. Aliyeshika usukani, akiogofya, abiria wote watanyamaza kimya, hivyo sometimes hata Kigoda or taasisi yoyote can do nothing to help out!.
P
 
Back
Top Bottom