zaleo
JF-Expert Member
- Dec 6, 2011
- 1,902
- 766
Hivi kumbe kumwambia baba yako "MWONGO" ni tusi? nimeamini usanii ni kazi mbaya kumbe, unahitaji limbwata kuwa msanii makini. Siku moja Mwalimu Nyerere alipokuwa analitangazia Taifa habari za vita dhidi ya Nduli Iddi Amini aliwaahidi watanzania kwamba atalitangazia Taifa kila kitu kinachoendelea wakati wa vita hivyo. Haikuchukuwa muda Amini alipowatandika baadhi ya vijana wetu akiwemo mpwa wake Nyerere mwenye kuongoza ndege ya kivita, watu tukasubiri mwalimu atasema nini. Waandishi wa habari walivyo wachokozi walimuuliza siku nyingine mbona wanasikia hivi na vile naye hawaelezi wananchi kila kitu kama alivyoahidi? Alicheka kwanza halafu akajibu, "Sio rahisi kueleza kila kitu hasa katika mazingira kama ya vita....ukiumizwa ukalalamika unampa turufu adui yako, kwa hiyo unatakiwa kuchambua nini useme kweli na nini usiseme kweli...."
Sasa kama hapo utamsemaje baba yako, hakukuongopea katika ahadi yake? Tusi sio tusi tena kama utaliangalia mazingira yake ambamo limetolewa. Hata mambo ya chumbani saa nyingine huitwa matusi, sasa ni matusi kweli? Kwamba baba na mama wanatukanana kila siku chumbani na walifunga ndoa ili watukanane kila mara ili watoto wapatikane?
Mtu mwingine atakuambia, "Unapendeza kama huna akili nzuri dah!" Je, utampeleka mahakamani kwamba amekutusi? Au utajidhalilisha mwenyewe kujionyesha kwamba wewe ni mshamba kutotumia akili ya kawaida kupambanua sifa na matusi? "Huyu kijana chizi sana yaani, amewajengea ghorofa wazazi wake hadi nammaidi kinoma..." Jamani kuna namna nyingi za kuelezea kitu ilimkuvuta akili za wanaokusikiliza wakuelewe haraka kwa kutumia lugha ya kawaida. Hata wakati mwingine Nyerere aliwatukana wanaomsikiliza nao wakapiga makofi kumshangilia, baadaye wakagundua kumbe walikuwa wanatukanwa. Mwalimu Nyerere kwa wakati wake alikuwa na akili za ushawishi sana na ilimchukuwa mtu kuwa mchambuzi makini ili kuelewa sawasawa anachokiongelea, ndio maana kina Kambona ilibidi wakae kando maana walishatambua mapema anachokimaanisha na kisha wakampinga waziwazi, lakini yeye hakutaka apingwe moja kwa moja pasipo kutumiaa mbinu ya ushawishi hasa kwa wasaidizi wake, alitaka watu makini lakini wanaotambua kwamba yeye ni boss.
Mbona mwingine aliwaambia watanzania wana akili za kijinga na ufinyu wa kufikiri na wivu wa kike na mkabaki kunung'unikia mvunguni hadi leo? Mbona JK anatukanwa hadharani naye anacheka tu ila wapambe wake wanaojishauwa kwake ndo wanayafanya makubwa wakati yeye anayetukanwa ana-enjoy? Nampenda JK kwa style yake ya kupuuzia mambo yasiyo na tija anayorushiwa hata ya nguoni, ambayo angekuwa mtu mwingine ingekuwa patashika. Acha uhuru wa kujieleza aliouasisi JK uendelee kujitanua ili mradi hadhuriki mtu. Watu wengine wanataka kutufanya watanzania wote ni punguani katika kutafakari mambo ila wao tu wanataka kututafsiria. Acha tujichambulie mambo kwa kadiri tunavyoweza, wala msiturubuni kama CCM wanavyotaka Katiba ya chama chao ndoyo iwe katiba ya nchi hata kwa kumwaga damu wakiweza. Mwizi hapendi kuibiwa, akigundua unamwibia atataka kukuua.
Hao wanaosema Tundu Lisu kamtukana Mwalimu ndio wenyewe wanaomtukana kila siku kwa kuyapiga chini yale aliyoyapigania hadi kifo chake, sasa kwa kuwa Lisu ni Mpinzani wao wanaitumia nafasi hiyo kumgeuzia kibao Lisu wanayemwona anawazidi kete, ili waonekane wenyewe wanamjali sana Mwalimu kuliko kina Lisu na kuwafunika wanaoitaka Tanganyika. Mbona mliliua Azimio la Arusha hata kabla hajafa, tena mkalinyonga akiwa anaona nanyi mkimkodolea mimacho kuona atafanya nini? Hivi hamjui kwamba mlimchefua sana Mwalimu kiasi kwamba huenda mlichangia kuiharibu afya yake kwa msongo wa mawazo mlipokanyaga kila kitu kizuri alichokipigania na kuchukuwa kila alichokipiga vita? Nani anamuenzi zaidi Mwalimu ninyi wanafiki na wale wanaosema kweli waionayo?
Nene mvifile hilo! Swela Mwagito.