Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Mwalimu Nyerere ametukanwaje hasa?

Unawezaje kumtetea mwl huku ukiwa unayasigina maoni ya wananch? Unawezaje kumlilia mwl huku ukiwa bingwa wa kula rushwa? Unawezaje kuwa upande wa mwl ukiwa umetorosha wanyama pori......nijuavyo hata mwl mwenyewe time without number amewah kukiri kwamba hata wao wana makosa sasa iweje anaetueleza makosa aliyoyakiri mwl yaonekane ni makosa tatizo kubwa ninaloliona hapa ni UNAFIKI
 
TL hajamtukana baba wa taifa hata kidogo, tatizo ni kwamba amesema ukweli tupu kwa yale Nyerere aliyofanya na wanayomfanyia.
Suala la Muungano, Nyerere alilifanya sirisiri na hakulitafutia ufumbuzi wa kweli badala yake akawa anaweka painkiller tu sasa cancer imekuwa ndiyo maana tunakuja kuhangaishana mpaka muda huu.
CCM wakiambiwa waache uwongo miaka 50 ya uwongo iishe wao hawataki kusikia hilo wanataka kuendeleza uwongo.
Kule zanzibarWatu waliuawa enzi za Nyerere historia ipo inajieleza, CCM wakiambiwa hilo hawataki kusikia.
CCM wameuwa Azimio la Arusha baada ya hapo tumeshuhudia watu waliokuwa hawatakiwi ktk chama/waliokimbia wamerudi na kuchukua madaraka makubwa ktk nchi hii na nii baada ya kumuuwa baba wa taifa wakaona wamalize kazi waliyokuwa wamekusudia, ufisadi/ukwapuaji/wizi/ujambazi/utapeli mkubwa ndiyo ikawa sera ya chama.
Kama Azimio la Arusha lilivunjwa na wakaunda Azimio la Zanzibar linaloruhusu wizi, nanu aliyemtukana baba wa taifa??
Hawa kina Lukuvi, Mkapa, J.K, Lowassa, Rostam, Sitta & CCM. Ltd(Intarahamwe) ndiyo waliomtukana na wanaendelea kumtukana baba wa taifa.
Ni matusi makubwa leo wakijinadi eti nao wanamuenzi baba wa taifa, UHUNI mtupu.
Majizi, manyang'anyi, mauwaji makubwa.
 
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.

Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?

Hata mimi najiuliza sana tusi hasa linalodaiwa kuelekezwa kwa mwalimu ni lipi? ukiuliza wanakwambia hatuwezi kurudia tusi we elewa tu amemtukana..ukisikiliza hotuba hauoni hicho kinachoitwa tusi..Nimegundua kuna watu ukikinginzana tu na alichokiongea nyerere basi umemkosea,umemtusi umemdhihaki..hii ajabu sana, Nyerere kafanya mema kwa nchi hii hilo halipingiki lakini na yeye ni mwanadamu yapo aliyoyafanya mabaya,hatuwezi kukumbatia kila alilolisema ama kulisimamia eti kwa vigezo tu kwamba yeye ni Baba wa Taifa..Na kama maoni na msimamo wa walioshika madaraka ni kukumbatia kila yaliyoasisiwa na viongozi waliopita bila kutathmini hali ya sasa basi taifa hili linaelekea gizani..Hatuwezi kuwa tunakataa mabadiliko kwa sababu tu tutatofautiana na walicho shauri waasisi..huu ni wakati tofauti kabisa halafu cha ajabu tunakataa kwa hoja nyepesi ya gharama..hivi tunapoteza mamilioni mangapi kwa ufisadi,un-necessary cost ku run government,mikataba mibovu n.k?mbona zilipopigwa kelele kuhusu kuondolewa posho halikupokelewa kama njia ya kupunguza gharama na wabunge wote wakaafiki? Muungano wa nchi 2 kuunda moja baada ya kuungana,kuna serikali ya umoja wa nchi mbili husika,lakini pia moja ya nchi husika ina serikali yake peke yake..muungano wa ajabu sana huu.ni ajabu kuona bado kuna watu leo hii hawaoni tatizo katika huu muungano...mwisho wake utakuwa mbaya sana!!
 
Nyerere mwenyewe aliwahi kusema, " Mimi si malaika. Na wala serikali yangu haikuwa ya malaika. Tulifanya mengi mazuri na mengine ya kijingakijinga. Tatizo lenu ni kuwa mnaacha yale mazuri na mnang'ang'ania yale ya kijinga!" Alichofanya Lisu ni kutaja yale ya kijinga ili watu wajihadhari nayo wasije kuyang'ang'ania! Kosa liko wapi hapa!
 
Sipendi mtu atukane wala atukanwe. Lakini naombe mniambie ni matusi gani hayo aliyomtukana Hayati Baba wa Taifa? Hata yule Mgiriki ambaye Nyerere alimpa masaa 24 kuondoka nchini hawezi kumtukana Nyerere Sasa huyu Tundu katukanaje? Mbona hamnitajii hayo matusi? Naomba mniandikie tu niyajue ili niungane nanyi katika kumlaumu Lissu na aliyemtuma kama yupo.
 
Ndipo tunapokosa direction kama taifa iwapo sifa ya kisiasa ni kumwaga matusi tu.

Kama matusi kwa nini hajapelekwa Kamati ya Maadili na Uongozi ya bunge kwa kutumia lugha chafu kwenye kikao cha bunge?

Kwa nini haukuombwa mwongozo kwa kuvunja kanuni(nakumbuka Leticia ndiye aliyepropose kuwalinda waasisi) liyowekwa ya kuvunjia heshima waasisi wa Taifa?
 
namkubali sana nyerere, lakini hiyo haitamaanisha kuwa pale alipokosea iwe dhambi kumkosoa! Naungana na mtoa mada: Kama tumeshindwa kutaja makosa ya tundu lissu, kama tumeshindwa kuyataja matusi aliyo tukana, basi tukae kimya. Nilichokiona mimi ni mtu kukosolewa alipokosea na mkosoaji alikuwa sahihi!

Anayetaka kueleweka aje na hoja yenye ushahidi kwamba aliyosema lissu siyo kweli na hayakusemwa na mwalimu, hayakufanywa na mwalimu na hayakuandikwa na mwalimu!

Napenda kusisitiza, ni katika jamii ya wendawazimu na wasanii wa kisiasa tu, ambapo watu watajidai kupenda kujali na kumtetea marehemu, huku tukishindwa kuwaheshimu wazee wetu walio hai kama kina mzee warioba, kina mzee aboud jumbe na wengineo. Halafu tusubiri mpaka nao wafe ili tujidai tunawaheshimu. Tuache unafiki!
mkuu big up sana mkuu,nawashangaa sana ccm jk alipokuwa hai hawakutimiza wala kuyaishi yale sahihi aliyosema..walisema yamepitwa na wakati,leo ni marehemu wanajifanya kumtumia kama nukuu za biblia,wanafiki hawa tulione hili...wanatafuta tonge tu
 
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.

Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
Ni taarabu na ngonjera tu wanazotaka kutuaminisha hawa ccm,binafsi namuunga mkono mh lissu kwa ukweli alioutoa,amesubutu big up LISSU udumu daima
 
[h=2]Edwin Mtei asikitishwa na alaani kitendo cha Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere[/h]
Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!

With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.

Edwin Mtei,

Founder Chairman of CHADEMA.

Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.

Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
 
Mh. Tundu Lisu ni miongoni mwa wabunge ninaowaheshimu sana tena sana. Japo sina chama cha siasa lakini nimekuwa nikikunwa na siasa za chadema. Lakini kwa hili kwakweli napenda kutofautiana na Mh. Lisu na chama cha chadema kwa kuendelea kukaa kimya kwa jambo kubwa kama hili na linalogusa hisia za watu wengi kwa namna tofauti. Naamini kuna watu wengi waliosikitishwa na tukio hilo na kupelekea kupunguza imani kwa Lisu napengine Chama kwa ujumla.

Ni ukweli Mwl. amefanya mambo mengi mazuri na mabaya pia na hata mimi kuna mbambo ambayo kimtizamo ninatofautiana naye mfano hili la Muungano. Tatizo langu kubwa kwa Lisu ni namna ya utumiaji wa maneno katika kufikisha hoja yake nzuri. Lisu inawezekana kabisa kutoa hoja yako na ikaeleweka pasipo kutumia lugha kali namna hiyo na pengine kutafsiliwa kama matusi. Mimi binfsi nayatafsiri maneno hayo kama matusi kulingana na nilivolelewa jinsi ya kuongea na kufikisha ujumbe kwa watu hasa wanaonizidi umri.

Kumbuka kuna watu wanamheshimu Mwl. kulingana na mambo aliyoyatenda na wengine mwalimu ni mtu wa level nyingine kiimani (Kulingana na imani zao za kidini) Hivyo muda mwingine matumizi mazuri ya maneno yanaweza kujenga taifa pasipo kuleta mgawanyiko katika jamii.

NOTE: Kwangu mimi tatizo siyo aliyoyaongea Lisu ila Jinsi alivyoongea.
Mkuu,

Mh Tundu Lissu ni mwanasheria aliebobea na kila mara yupo mahakamani kutetea kesi za washitakiwa wa CDM, swala la kuchagua maneno amna mtu anae lielewa vizuri kama mwanasheria na mwanasiasa, yeye ni vyote.

Cha muhimu ni kufuta kauli yake na kutuomba msamaha watanzania kwa kumziaki na kumtungia baba wa taifa, ukosefu wa heshima kama ule si wa kuvimiliwa.

Aliyoyaongea alikusudia kuyasema hii si mara ya kwanza Lissu kumdhihaki baba wa taifa mwaka jana aliwahi kutoa lugha za kejeli kwa yule mzee vilevile akiwa anaongelea maswala ya ujamaa na kumkashifu kwa maneno makali baba wa taifa, he is setting a trend ambayo aikubaliki kabisa kwenye macho ya wengi wetu.
 
Wengi wa kina nani? Sisi na #DiniYetu mpaka leo tunamadai na Tuna maalni na tutanedelea kumlaani kwa kutukandamiza na kutuletea Bakwata.
 
Tusiwe watumwa wa mawazo .Nyerere hakuwa malaika ni binadamu anamapungufu yake. na kukosolewa isiwe kosa CCM hawana hoja wamebaki kusema amemtukana baba wa taifa ametukana nn? CCM wanafiki wakubwa

nashukuru kwa kuliona hilo. Hakuna mkamilifu hata mchungaji na mashekhe wanakosea
 
Mkuu,

Mh Tundu Lissu ni mwanasheria aliebobea na kila mara yupo mahakamani kutetea kesi za washitakiwa wa CDM, swala la kuchagua maneno amna mtu anae lielewa vizuri kama mwanasheria na mwanasiasa, yeye ni vyote.

Cha muhimu ni kufuta kauli yake na kutuomba msamaha watanzania kwa kumziaki na kumtungia baba wa taifa, ukosefu wa heshima kama ule si wa kuvimiliwa.

Aliyoyaongea alikusudia kuyasema hii si mara ya kwanza Lissu kumdhihaki baba wa taifa mwaka jana aliwahi kutoa lugha za kejeli kwa yule mzee vilevile akiwa anaongelea maswala ya ujamaa na kumkashifu kwa maneno makali baba wa taifa, he is setting a trend ambayo aikubaliki kabisa kwenye macho ya wengi wetu.

wewe ujawahi kukosea mkuu? Hakuna mkamilifu ktk dunia hii hata huyo Nyerere
 
mbona watu mmekereka sana kuhusu mwalimu kuitwa muongo na mzandiki?au ndio siasa zenyewe?mbona maandiko matakatifu yanawakataza msiue,msiibe,msiseme uongo,msizini,msiwe walevi nk lakini bado ndio kwanza mnafanya yale yasiyompendeza mwenyezi mungu,ila hili la baba wa taifa mnalishupalia kweli,nyie ni wakamilifu?
 
Wengi wa kina nani? Sisi na #DiniYetu mpaka leo tunamadai na Tuna maalni na tutanedelea kumlaani kwa kutukandamiza na kutuletea Bakwata.
Wengi nikimaanisha ni tunaopinga udini, siasa za ukanda na ulaghai as what Lissu is insinuating.

For that matter wengi ni watanzania wanao heshimu jitahada za JKN kuweza kutuacha alipo tuacha kwengine bado wanabaguana. Sasa mtu kwenye kulilia ubaguzi anaenda kumtukana mtu alietuachia neema, na watu kama nyie wenye akili za hovyo za kubagua bagua mnashangilia.
 
Wanaosema Tundu Lissu kamtukana Nyerere wanamatatizo kwenye akili zao akil. Au wanau ccm unausumbua
 
wewe ujawahi kukosea mkuu? Hakuna mkamilifu ktk dunia hii hata huyo Nyerere
Ni kweli akuna aliemkamilifu lakini kamwe siwezi kwenda kuwatukana wazazi wangu katika kukosea kwangu hata nilipokuwa sikubaliani nao natafuta namna sahihi ya kutofautiana nao lakini si kuwakejeli hizo sio mila zetu za kitanzania. Alicho fanya ni kuwafunza watoto kukosa heshima na misingi ya utaifa lao na kuto waheshimu viongozi waliotumia nguvu nyingi sana kujenga taifa hili imara.
 
Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.

La kusikitisha ni kuwa hata askofu (Si askofu wa kujipachika kwani aliwahi kuwa askofu mkuu wa kanisa la Anglicana Tanzania na Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo (CCT)) ameingia kwenye mtego huo. Nyerere tunamuheshimu sana ila inabidi kujua alikosea wapi ili tujisahihishe. Hata kama ikikubaliwa serikali 2 zilizoboreshwa, wataboresha wapi bila kujua udhaifu na makosa yako wapi? Tuambiwe kamrushia tusi gani?
 
Back
Top Bottom