Nitakujibu nikishakuwa na uhakika kuwa unajua maana ya "kutukana". Iwapo hujui maana ya matusi basi hakuna utakaloona tusi na itarudi tena kwenye "maneno na matumizi yake"'
Mkuu, nukuu hayo matusi aliyotukanwa Nyerere. weka bra bra pembeni.
Tatizo ni lisu na sio matukano, kwani yapo matusi mengi sana yaliyotumiwa na wale wa mipasho/ccm na kwa nini lisu tu. mbona hamkusema kwa mtikila kipindi cha kifo cha nyerere 1999
........MANENO yote yaliyowahi kutoka mdomoni mwa Lissu yanatakiwa yaangaliwa kwa makini, mfano yakiwa yale maneno yake dhidi ya Zitto na Kitila.........
Hebu niambie, alimhusisha na ushoga?Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.
Swali langu unatakiwa ulijibu wewe uliyeshikwa na kisebusebu na n..ge cha kuwasilisha hayo ya MTEI kwani wewe siku hizi umekuwa msaidizi wa MTEI hadi uwasilishe hoja zake?
Edwin Mtei ni member humu. Isije ikawa haya maandishi yameghushiwa, kama ccm walivyozoea kughushi hasa hiyo ya kuteuliwa IMF 1972. Ajitokeze mwenyewe kueleza madhara aliyopata kwa matamshi ya Lissu.
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.
Kwa akili zenu, na u CDM wenu bado mnaona kabisa Lissu alikuwa sahihi kutumia lugha zile na kumwita Mwalimu Nyerere mwongo! Kwa hiyo unataka kuwaambia watanzania kuwa mwasisi wenu wa CDM ni bongo lala kwa kuwa Lissu hakutoa tusi lolote? Kweli CDM sasa siasa zimewashinda!
Mi nasema mtu yeyote akikosea atakosolewa na akifanya vizuri atasifiwa na kwa mujibu wa imani yangu ni Mungu tu hakosolewi kwa sababu yeye ni PERFECT. Kutotaka Nyerere akosolewe ni kujidai eti alikuwa PERFECT katika maamuzi yote aliyofanya. Hii si Kweli lazima tubadilike tumweke binadamu yoyote kwenye mizani bila kujali umaarufu wala hekima ya kibinadamu aliyo nayo. tukijidai eti kumkosoa nyerere ni Dhambi inayostahili adhabu kubwa tutakuwa tumefisha uhuru wa fikra na hivyo kujifungia kwenye blanket la umbumbumbu wa hali ya juu. Nyerere was not God na hatakaa awe Mungu kwani kuna aliyofanya mazuri na kuna aliyokosea kama binadamu. Tumemsifia miaka yote kwa mazuri aliyofanya na kama alikosea basi anastahili kukosolewa. inakuwaje kukosoa mawazo na matendo ya nyerere eti ni MATUSI ;huu ni unafiki mkubwa wa kuzima mawazo chipukizi yenye mtazamo wa mawazo huru
Na wewe una matatizo ya kujua maana na matumizi ya meneno; umetafuta majina badala ya maneno. Nitakusaidia kwa kuanza hivi: " Maneno ni upanga wenye ncha mbili zinazokata pande zote. Maneno yako yanaweza kukufanya uwe na hatia na vile vile yanaweza kukuondoa kwenye tuhuma za hatia. Yote inategemea na jinsi unavyotumia maneno yako."
Halafu nitakurahishia hivi:
MANENO yote yaliyowahi kutoka mdomoni mwa Lissu yanatakiwa yaangaliwa kwa makini, mfano yakiwa yale maneno yake dhidi ya Zitto na Kitila.
Matusi ni maneno ya kawaida. Yanakuwa matusi tu pale yanapotumika kudhalilisha (discredit) watu wengine, vinginveyo siyo matusi. Nimeuliza iwapo muuliza swali ana threshold yoyote inayotofuatisha matusi na maneno mengine, hajanijibu ila wewe umeingia kumsaidia. Msioona matusi katika maneno ya Lissu ina maana kuwa hamuoni udhalilishaji katika maneno yake, na inakuwa ni vigumu kuwaridhisha. Nyie wanasheria nadhani mnajua sheria za Defamation of Character ambazo kwa lugha rahisi ni sheria dhidi ya kutukana. Ni mnajua ni mambo gani yanayotumika kutukana na ni yapi; na vile vile mnajua kuwa kuna hata sheria dhidi ya kutukana mtu aliyekiwsha fariki?
Ndipo tunapokosa direction kama taifa iwapo sifa ya kisiasa ni kumwaga matusi tu.
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.
Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.
Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
Siko tayari kutukana, ila jua kua maneno aliyoyasema hakustahili kuyasema dhidi ya Nyerere.