Tatizo watu wanamuona nyerere kama mungu wao. Sishangai kusikia watu wana abudu mizimu na sanamu kwa hali hii.
Mleta mada anataka muyataje hayo maneno nyie mnakuja na ngonjera zile zile, NAOMBA UTUAMBIE LISSU AMETUKANA VIPI AU MANENO GANI MABAYA ALIYOYATAMKA JUU YA NYERERE. kwa hiki ulichokiandika bado haujajibu swali la mleta mada
kwa upande mwingine kumbe tafsiri ya msikilizaji inaweza kufanya hayo maneno kuwa matusi ama la,sasa basi ili kumuaminisha mwingine aamini unachoamini ni kumshawishi kwa hoja na mifano au nukuu toka ktk hayo maneno,tukirudi kwa lissu ninyi mnaoamini kuwa ametukana tunaomba nukuu ya yale unayoamin kuwa ni matusi ili tukikubaliana nanyi tuungane ktk kumkemea bwana lissu,lakini kinyume na hayo tutaendelea kuamini kuwa hizo ni siasa za majitaka ambazo hazina nafasi leo.
Kuna uvumi (binafsi naziita propaganda) kuwa Mjumbe wa Bunge Maalum na Wakili Msomi mwenzangu Tundu A.M.Lissu 'amemtukana' Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 'Matusi' husika yanadaiwa kuporomoshwa na Tundu Lissu alipokuwa akiwasilisha Maoni ya Wachache katika Kamati Nambari Nne ya Bunge.
Inasemwa kuwa Tundu Lissu amemtukana na kumdhalilisha Baba wa Taifa. Propaganda hizi zinazosambaa haraka na kwa kishindo zimemkumba hadi Mzee Edwin Mtei ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa CHADEMA. Nikumbukacho ni kuwa Lissu alipokuwa akitetea na kufafanua Maoni ya Wachache,alitoa mifano minne akiwataja watu mbalimbali wakiwemo Mwalimu Nyerere,Profesa Issa Ghulamhussein Shivji na Dr.Harrison Mwakyembe.
Kwanza,tufahamishane hasa matusi yaliyoporomoshwa na Wakili Lissu dhidi ya Mwalimu Nyerere. Tukiyajua na kutambua kuwa ni matusi na dharau kweli,tuungane kumkemea Wakili Lissu na kumuonya asirudie tena. Karibuni tutaje matusi au dharau za Wakili Tundu Lissu kwa Mwalimu Nyerere. Halafu,kwanini wengine waliotajwa hawaonekani kama wametukanwa au kudhalilishwa?
Jaji warioba wakati anawasilisha rasimu,aliwaasa wajumbe wa bunge maalumu la katiba kuwa,ili katiba mpya ipatikane,MAONI ya wananchi yalimo yenye kwenye Rasimu ni la lazima yaheshimiwe. Tunachokiona sasa ni janja ya kutunga katiba ya watawala badala ya katiba ya wananchi