Mwalimu Lwaitama: Kesi ya Mbowe: " Rais Samia anayo Mamlaka ya kuifuta"

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,857
35,868
Msomi Nguli Mwalimu Lwaitama amefunguka yenye kujenga, kwake Mheshimiwa Rais:

Yawezekana kuganga yajayo kwani yaliyopita si ndwele.

Hoja ya Mwalimu Lwaitama ina mashiko.

Hoja ya Mwalimu Lwaitama ni yenye kuzingatia katiba ya sasa na hasa uwepo wa ule mhimili uliojichimbia zaidi.

Habari za tashwishi ya afya au hali ya mheshimiwa Mbowe kwa ujumla gerezani ambako hakuweza kuonwa leo, zimfungue macho Mheshimiwa Rais.

Hala hala kabla ya hatari.

Mola ampishilie mbali pepo mbaya.
 
Mkumbusheni dr Lwaitama kuwa Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa kufuata misingi ya sheria. Rais kufuta kesi inayoendelea mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Aache mahakama ifanye kazi zake kwa mujibu wa katiba na sheria. Kufuta kesi kwa kufuata hisia za kisiasa ni upuuzi na kusigina katiba na sheria zake.
 
First of all, why should be dismissed while there are serious allegations against Freeman Mbowe?

Second of all, Samia has no such a power.

Lastly, time will tell but according to the trial within trial conducted by the Court, I hope that Mr. FREEMAN MBOWE will be convicted & sentenced for what he did. MEANING: He will get what he deserves.
 
katiba inampa rais mamlaka ya kufuta hukumu bila ya kutoa sababu (hii pia ni kuingilia uhuru wa mahakama)na hata Nyerere mwenyewe katika kikao kimoja aliwahi kusema "mimi ni rais,naweza tu kusema kamateni hawa" hapo alikuwa anajadiliana na ma CCM,yakamshauri "mwalimu huu ni uhaini kamata hao".
kitu ambacho hakipendezi hapo ni kwamba huyu anashauri Samia afute kesi wakati rais anaamini Mbowe ni gaidi
sidhani hata Mbowe kama atakubali huu upuuzi
 
Kwanza huyu ni Mwalimu Lwaitama. Mtake radhi tafadhali.

Pili zingatia:

1. Katiba iliyopo yenye mhimili wenye kujichimbia zaidi,
2. Kesi ya kubumba.

Nini kinashindikana hapo?

Uhuru upi unaouongelea wewe?
Kwani hukumu ya Siyani hujaiona au hata kuisikia?
 
Ibara ya ngapi ya Katiba inampa mamlaka ya kufuta kesi iliyopo mahakamani? Knowledge is power
Embu nipe maarifa hapo.
nilikuwa nazungumzia kesi iliyohamuliwa tayari yani hukumu,nita edit hapo mkuu, nazungumzia ibara inayompa rais mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote
hii nayo ni kuingilia uhuru wa mahakama,hivo basi hoja yangu ni kwamba hakuna uhuru wa mahakama kwenye katiba
 
First of all, why should be dismissed while there are serious allegations against Freeman Mbowe?

Second of all, Samia has no such a power.

Lastly, time will tell but according to the trial within trial conducted by the Court, I hope that Mr. FREEMAN MBOWE will be convicted & sentenced for what he did. MEANING: He will get what he deserves.

Mwalimu Lwaitama is not speaking from nowhere. The basis of his argument is solid:

1. The prevailing Constitution embraces the presence of "the executive" as the superior. The rest are subordinates.
2. The case itself is politically orchestrated.

To qualify the two statements, the explanation is provided.

"The truth of this, is obvious even to a small child", concludes the don.

He could not have a better conclusion 😁😁.
 
katiba inampa rais mamlaka ya kufuta hukumu bila ya kutoa sababu (hii pia ni kuingilia uhuru wa mahakama)na hata Nyerere mwenyewe katika kikao kimoja aliwahi kusema "mimi ni rais,naweza tu kusema kamateni hawa" hapo alikuwa anajadiliana na ma CCM,yakamshauri "mwalimu huu ni uhaini kamata hao".
kitu ambacho hakipendezi hapo ni kwamba huyu anashauri Samia afute kesi wakati rais anaamini Mbowe ni gaidi
sidhani hata Mbowe kama atakubali huu upuuzi

Msikilize Mwalimu Lwaitama kumwelewa. Wazi wazi kasema:

1. Kwenye mazingira ya katiba tuliyomo
2. Kesi ni ya kubumba.

#1, anatambua uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi. Mifano ipo pale kuishibisha hoja hii. Anatambua mhimili huo haukusubiri kumpandisha cheo japo atoe hukumu iliyokuwa ikisubiriwa ndani ya siku chini ya wiki!

#2, anatambua rais alidanganywa kuwa Mbowe alikuwa katoroka, tena wenzake tayari walishafukuzwa.

Kahitimisha mwalimu pale kuwa haya ni wazi hata kwa mtoto mdogo. Sembuse watu wazima na akili zao?
 
Msikilize Mwalimu Lwaitama kumwelewa. Wazi wazi kasema:

1. Kwenye mazingira ya katiba tuliyo
2. Kesi ni ya kubumba.

#1, anatambua uwepo wa mhimili uliojichimbia zaidi. Mifano ipo pale kuishibisha hoja hii. Anatambua mhimili huo haukusubiri kumpandisha cheo japo atoe hukumu iliyokuwa ikisubiriwa ndani ya siku chini ya wiki!

#2, anatambua rais alidanganywa kuwa Mbowe alikuwa katoroka, tena wenzake tayari walishafukuzwa.

Kahitimisha mwalimu pale kuwa haya ni wazi hata kwa mtoto mdogo. Sembuse watu wazima na akili zao?
hapo sasa nimeelewa Mkuu,nitamsikiliza nikiwa na bando.kama amesema hivo ni sahihi
 
Back
Top Bottom