Wana jukwaa.
Nimejaribu kuvimilia hili kwa kuliweka mwoyoni ila nimeshindwa.
mimi ni kijana nimehitimu mwaka jana diploma ya uhandisi wa ujenzi (civil engineering) baada ya kuhitimu nimebahatika kufanya kazi katika makampuni binafsi na sasa taasisi ya kiserikali.
Katika shughuli zangu nimekutana na vijana vibarua ninaofanya nao kazi nikiwa kama msimamizi wao. Cha kushangaza kundi la vijana nilionao sasa kuna kijana mmoja ni muhitimu wa diploma ya ualimu.
Haikuwa rahisi kumtambua kama amehitimu ualimu mwaka jana lakini vijana wenzake anaofanya nao kibarua wamekuwa wakimtania kuwa yeye amesoma ualimu lakini anabeba zege pamoja nao ambao hawajaenda shule.
Utani huu nilipousikia mwanzo sikuitilia maanani lakinj nimeona ukizidi kila siku maana nimefanya nao kazi sasa wiki ya tatu.. nimefanya uchungunzi na kugundua kweli ni muhitimu wa diploma ya ualimu mwaka jana na baada ya kusubiri ajira bila mafanikio.
Ikumbukwe hata akijitolea katika shule hana posho ambazo walikuwa wanalipwa kwa michango ya wazazi sasa michango hiyo hakuna na shule haziwezi kuwamudu.
Imeniuma sana si kwa sababu anabeba zege na suruba za siku nzima juani lakikini kwa sababu ya elimu yake na watoto wa masikini tumekuwa tukikimbilia kada ya ualimu tukijua ndio yenye ajira ya uhakika...
najiuliza pia kwa kukata tamaa huku hata akiajiliwa kweli atakuwa na moyo wa kufundisha??
kimaadili imekaaje makundi ya vijana wa site mnawajua matusi ya midomoni na mambo mengine...je ataweza kuwapa elimu sitahiki watoto.
Serikali litazameni swala hili msidhani mnajenga. Manung'uniko walionayo walimu hawa ni sumu mbaya kwa elimu tunayotegemea waitoe hapo baadae kwa watoto na wodogo zetu.