Crucifix
JF-Expert Member
- Feb 20, 2011
- 1,655
- 593
KLM wanaposema ndege itaruka saa 11:45 basi tegemea saa11:40 ndege itaanza kutembea tayari kuelekea njia ya kurukia. Haya ndio matarajio ya kizazi hiki. Kama kuna hitilafu, tutatangaziwa ndani ya muda wa kutosha kuwa ile ndege iliyokuwa iruke saa 11:45 sasa itaruka saa 12:45...hakuna longolongo.
Mwakyembe ulisema treni zako zitaanza 'kuruka' Oktoba. Sasa kwa akili ya haraka, kama hujataja tarehe sisi tunachukulia Oktoba mosi. Leo unasema, "Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini.... "Unataka kutuzuga kuwa sio Dar bali nchi nzima hivyo tuendelee kusubiri kwa matumaini. Hii lugha haipishani na ile ya kiranja wako Pinda ambaye kila siku anakariri, tumejipanga........
Tena unaongeza bila aibu, Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo. Ndio lazima tuchonge ngonjera kwa sababu umekuwa mwongo!!! Kama hukumaanisha Oktoba mosi, sema sasa Oktoba ngapi na uache kujingata ulimi kwani heshima yako inaanza kushuka kwa kasi.