Mwakyembe umechemka, acha kujing'ata ulimi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe umechemka, acha kujing'ata ulimi.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crucifix, Oct 5, 2012.

 1. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  KLM wanaposema ndege itaruka saa 11:45 basi tegemea saa11:40 ndege itaanza kutembea tayari kuelekea njia ya kurukia. Haya ndio matarajio ya kizazi hiki. Kama kuna hitilafu, tutatangaziwa ndani ya muda wa kutosha kuwa ile ndege iliyokuwa iruke saa 11:45 sasa itaruka saa 12:45...hakuna longolongo.

  Mwakyembe ulisema treni zako zitaanza 'kuruka' Oktoba. Sasa kwa akili ya haraka, kama hujataja tarehe sisi tunachukulia Oktoba mosi. Leo unasema, "Nipeni muda wa miezi sita ili muweze kuona sekta ya reli itakavyokua imekamilika nchini.... "Unataka kutuzuga kuwa sio Dar bali nchi nzima hivyo tuendelee kusubiri kwa matumaini. Hii lugha haipishani na ile ya kiranja wako Pinda ambaye kila siku anakariri, ”tumejipanga........”

  Tena unaongeza bila aibu, ”Tuacheni tufanye kazi na nyie endeleeni kutunga ngojera kuhusiana na usafiri wa reli lakini sisi tunajua tunachokifanya kwani niliposema usafiri wa reli unaanza mwezi Oktoba sikumaanisha utaanza Oktoba Mosi kwani hata Oktoba 15 ipo ndani ya mwezi huo huo Ndio lazima tuchonge ngonjera kwa sababu umekuwa mwongo!!! Kama hukumaanisha Oktoba mosi, sema sasa Oktoba ngapi na uache kujing’ata ulimi kwani heshima yako inaanza kushuka kwa kasi.
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Kikwete na familia yake wanahodhi kampuni kubwa sana ya uchukuzi, je reli ikipona atakula wapi?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mbona jamaa Alishachemsha tokea akatae kusema kuhusu ule ungonjwa wake wa kumomonyoka!!!
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,954
  Trophy Points: 280
  so? ina maana hukumuona alivyohangaika kuhakikisha hiyo tarehe treni zinatembea? au hujui kuwa kutotembea kumetokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wake! btw hizo wiki mbili ndo zinakutoa povu namna hiyo au ufuasi wako wa makundi pinzani yasiyolala kuona Mwakyembe akitekeleza ahadi zake za maendeleo
   
 5. B

  BORGIAS Senior Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mie nakushangaeni siku zote mlikuwa hamjajua kama huyu ni HOT AIR?

  Mimi namjua sana toka enzi zake za pale mnazi mmoja alipokuwa na na ofisi jengo la ushirika na mwenzie aliyeamua kurudi kufundisha UD bwana MVUNGI

  Sasa wakati sisi tunaletewa upuuzi wa treni isyo na kichwa wala miguu tazama kule Nairobi na commuter trains zao zilivyo safi na kueleweka

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  [youtube]http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=FbwS8mWJT6U[/youtube]

  Syokimau Railway Revolution - YouTube

  [youtube]FbwS8mWJT6U[/youtube]


  Halafu mnaanzisha thread kuuliza eti wakewnya wamewazidi nini
   
 6. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Tafadhali elewa pia Oktoba inaweza kuwa 2013, au hata 2015!
  Usafiri ni zaidi ya mabehewa.......miundombinu inabidi iwe tayari na huduma itolewe kwa faida. Stay tuned
   
 7. K

  KVM JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kizazi hiki cha wapi? Bongo? Wapi kunatokea hivyo?
   
 8. Kingmairo

  Kingmairo JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 4,976
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Ni kweli aliahidi October na bado hajafanikiwa kutimiza alichoahidi, lakini angalau tumeona jitihada alizoweka na nia ya dhati aliyonayo. Inawezekana anakwamishwa au amekwama lakini hata jitihada kidogo alizofanya ni sawa na bure? Mawaziri wangapi wamekaa pale kwenye wizara husika hata wazo wahakuwa nalo? Mnyonge mnyongeni lakini ujira wake mpatieni.
   
 9. B

  BORGIAS Senior Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 126
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  the man is full of hot air
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Nchi ya Kusadikika- Shaaban Robert 1958
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mhh mimi sitaki hata kuchangia kuhusu lini inaanza!! Maandalizi tu yanatosha kutuonyesha kuwa hizo ni ndoto!! Maana hatakwenye ile reli iliyopo hatujaona vituo wala platform kwa ajili ya abiria!!!

  Mimi nilidhani wanakarabati reli, pamoja na kuweka miundo mbinu japo kiasi ya kuwezesha "commuter train" All we see mabehewa yanapakwa rangi ya nyumba tu, na wanasiasa wana-test route isiyokuwa na vituo!!!

  Jamaa zangu walioko bongo wanansema ni maneno tu, kama kawaida!!!
   
 12. S

  Shekispia JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwakyembe nia anayo ila uwezo ndo tatizo.
   
 13. Annael

  Annael JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 13,228
  Likes Received: 10,194
  Trophy Points: 280
  Mwacheni wazirir afanye kazi yake. Nadhani wewe ni kati ya wale waliofukuzwa.
   
 14. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,417
  Likes Received: 258
  Trophy Points: 180
  sema,mwakyembe nia anayo ila riz one yale malori ya mafuta yatafanya kazi gani?
  Ezekieli maige naye anamalori yanaenda mpaka kongo nayo je
  ?
   
 15. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,252
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha
   
 16. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hatutaki jitihada, tunataka matokeo ya jitihada! Jitihada bila matokeo ni maneno matupu hayavunji mfupa. Kuna tofauti gani katika maisha ya watu kutokana na jitihada hizo?
   
 17. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  anasubiri mda mwafaka wa kutangaza yaliyomkuta [ugonjwa]. naskia anasubiri mpaka 2014 kuelekea 2015 ili amwaribirie mtu ambaye anautaka urais 2015.
   
 18. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama Mkulu aliyemteua alitoa ahadi ambazo alijua hatoweza kutekeleza unategemea Mwakyembe ataona haya kutupiga kalenda kuhusiana na huu usafiri wa treni?!! Think again.
   
 19. moto2012

  moto2012 JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 2,165
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Huyu jamaa ni mchemfu wa siku nyingi, mnakumbuka hata kwenye ile riport ya Richmond iliyompa umaarufu alikiri kuwa kuna UKWELI ALIOUFICHA ili kuinusuru serikali, tangu hapo mi najua si msemakweli, na hata huko kwa makanisa anakoenda kuomba ni kama kuzuga tu! Kama alishindwa kusema ukweli akiwa nje ya serikali kwa akili ya kawaida ataweza kweli kusema ukweli akiwa ndani ya serikali?
   
 20. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni mapema mno kuanza kumshutumu Dr Mwakyembe kwa kutoanza kwa usafiri wa treni Dar. Mambo mangapi yamepangwa kufanyika lakini hata dalili hatuioni? Naamini watendaji wengine serikalini wakimpa ushirikiano Dr Mwakyembe soon tutaona matunda ya jitihada zake.
   
Loading...