Mkuu GEZA ili ndilo tatizo kubwa la mindset za Watanzania tulivyo, hivi raia ambaye yuko in his/her right mind anaweza kweli kuanza kumdhihaki/kumbeza mtu mzalendo kama Mwakyembe!!!
Hizi tabia zilizo kubuhu ndani ya nafsi zetu za kutafuta kila njia kumkatisha tamaa mtu anayejituma sana na mfatiliaji wa hali ya juu kuna hashiria nini?? Kwamba Watanzania tumeanza kukosa utu na kushabikia vyama tu as if chama kingine kikitawala ndio utakuwa muarobaini wa matatizo yetu, tunashindwa kutoa pongezi au kitia moyo watu/viongozi wanao jituma, tunakuwa blinded na chuki tu za vyama fulani mpaka tunasahau uzalendo.
Wakati mwingine tunapaswa kujifunza kutokana na matatizo yaliyo wakumba wenzetu kwa kufanya makaso kama haya haya yanayo inyemelea nchi yetu, ntatoa mifano ya nchi mbili ili tujifunze kitu.
Warusi walifanya blunder ya kutaka kuondoa uongozi wa kikominisiti kwa njia yoyote ile, yaani walikuwa hawasikii la mtu kuhusu hilo, niliwahi kuwauliza hivi kwa nini mnachukia Uongozi na chama namna hiyo wakati Uongozi huu ndio uliweza kuifanya URUSI mpaka ikawa Super Power, inawezekana Viongozi wakawa na mapungufu yao kama binadamu, lakini hii radical change mnayotaka inaweza kuwa cost an arm and leg at end of the DAY - wakasema sisi tunataka mabadiliko they have had enough of communist party - miaka 65 waliokaa madarakani inatosha sana!
Nikawauliza hivi huyu Yelstin mnaye mshabekia mbona wanasema ni mlevi sana, wakasema sisi hilo hatujali tunacho taka ni mabadiliko, Yelstin hata kama ni mlevi atakuwa na wasaidizi wa kumuwezesha kuendesha nchi bila matatizo, sitaki kurudia yaliyo tokea URUSI baada ya Yelstin kupata madaraka - lakini kipindi chake madarakani nchi ikavurugika, jeshi lao likakosa vipuri, mafia wakawa ndio kama wanaongoza nchi, Urusi ikarudi nyuma kimaendeleo na kijeshi kwa kasi ya kutisha na infact tukiwa wakweli ni kwamba URUSI karibu ifilisike licha ya kuwa na natural resources lukuki, Mungu bariki kaingia Putin ndio sasa Urusi inajikongoja kujaribu kurudi kwenye nafasi yake iliyo kuwa imepotea kwa kukosa kutafakali MAMBO. Nataka nieleweke kwamba hapa sio kwamba nashabikia chama chochote, mimi natoa angalizo tu kwamba wakati mwingine tunapaswa kuwa makini sana katika mahamuzi yetu, ushabiki tu hautatufikisha mbali.
Nayo kama ilivyokuwa URUSI walitaka mabadiriko bila ya kujali kundi ambalo linataka kupewa mabaraka lina viongozi gani, Wazambia nao walikuwa wanasema maneno hayo hayo ya Warusi kwamba hawajali kiongozi wao kama amesoma au la cha muhimu eti "is a good ORATOR" na ni kiongozi peke yake jasiri wa kuweza kum-teach a lesson Mzee Kahunda!!! Na kweli Chiluba aliwahi kumfunga Kahunda mpaka Kambarage akapaswa kuingilia KATI, lakini Zambia je ilikuwa katika hali gani baada ya Chiluba kushika usukani - niliwahi kwenda Mpika wakati huo nikakuta wafanya kazi kwenye workshop wanakula mahembe!! Hawana chakula wala ada za kuwalipia watoto wao kwenda shule - nchi ilikuwa katika hali mbaya sana, Zambia was no longer under the SUN.
Nimalizie kwa kusema kwamba sio vizuri kuwakatisha tamaa viongozi wanao jitahidi kutukwamuwa,
partisians not withstanding, kumbuka Tanzania ni yetu wote - mwenyekiti MAO aliwahi kusema kwamba mtu usijali ni paka mweupe au mweusi cha muhimu ni yupi yuko mahili kukamata panya.