Mwakyembe umechemka, acha kujing'ata ulimi.....

Mkuu nashukuru sana kwa hilo, labda niweke wazi kwamba sio kwamba huwa nam-support Mh.Mwakyembe blindly in fact kuna thread fulani niliwahi kumshambulia sana ntajaribu kui-trace hiyo ilikuwa mwaka jana, lakini pamoja na mapugufu yake kama binadamu - alipo teuliwa kuwa Waziri nilivyo ona anavyo fatilia utendaji kazi katika wizara yake kidogo hiyo ilinipa matumaini sana, niakaona finally jamaa huyu anaweza kutukwamuwa kutoka katika lindi ya ukosefu wa uwajibikaji katika TAIFA letu - I might be wrong, lakini tujaribu kumpa moyo ili tuone kama atafanikiwa ku-deliver goods au atatuacha kwenye mataa, mkuu hata akiwa a jack of all trade finally mambo yatajipa kama ana moyo wa kweli wa kukwamuwa TAIFA letu. Once again thanks a lot kwa angalizo lako "OBIBEMU".
Bukyanagandi, sijui una umri gani lakini ngoja nikurudishe nyuma kidogo...unamkumbuka Raisi mstaafu Ali Hasan Mwinyi alivyoingia madarakani kwa mwembwe?...eti na fagio la chuma! Unamkumbuka Raisi mstaafu Benjamin William Mkapa?...eti na utandawazi na uwajibikaji! Huyu Raisi wa sasa je?...eti kasi, ari na nguvu mpya! Sitawataja mawaziri waliomtangulia Mwakyembe na mwembwe walizoingia nazo wakati wanateuliwa ila nitamtaja moja, mwanasheria Waziri Mkuu Pinda, sina hakika kama bado yupo lakini safari ya mwisho nililolisikia ni lile la wananchi kukamatwa kwa kumzomea! Hiyo ndiyo Tanzania yetu, huo ndio mfumo wetu na hao ndio viongozi wetu...Mwakyembe? mmh, sina hakika lakini katu huwezi ukapanda mbaazi ukavuna nyanya!
 
Last edited by a moderator:
watu wana upuuzi mmoja kuna mtu ametoa picha za treni za Nairobi na akaanza kukejeli kuhusu za kwetu wakati inajulikana pasi shaka kuwa Mwakyembe ametumia bajeti isiyozidi Tshs 4 bio. kuanzisha commuter trains kwa kupitia mabehewa, njia na vipuri tulivyonavyo na si vipya! Sasa badala ya kumpongeza kwa kutoa ajira na kutumia gharama kidogo watu wana CCM wa makundi (i guess) wanaanza kumfitinisha wakati huyu huyu Mwakyembe tumemuona akisaini air agreements na kutafuta wawekezaji wa Railway ya kati huko Ujerumani katika kipindi kisichopungua miezi sita tangu akwae wizara ile! na pia tumemuona huyuhuyu Mwakyembe akiwaajibisha watu mafisadi katika mashirika na pia tumemuona akikataa ku-extend leasing agreement ya aircraft za ATC toka Dubai firm kwa vile zilikuwa hazina manufaa! Kusema kweli kuna watu wanaudhi na huwa sidiriki kusita kuwatukana maana akili zao nathani ni punje ya mchele! Wamuache jamaa afanye kazi zake kwa nafasi tunajua hata bandari inatengamaa kwa kasi ya ajabu! Mie nina uhakika kwa usimamizi wa mwakyembe hata haya mabehewa tutakayotumia yanaweza kununua mabehewa mapya kabisa mbali na njia za usafiri (reli) kupanuka!

Well said mkuu GEZA, watu hawataki kumpa kumpa credit yoyote katika kuangahika kwake! Yaani mimi naona aibu sana nikiona Wazalendo wenzetu wanamkandia mtu kama Mh.Mwakyembe bila simile, pamoja na mapungufu yake kama binadamu lakini sio vizuri kumkatisha tamaa na kuonekana kama wanamzomea hivi yaani wako hell bent kuhakikisha hafanikiwi katika kutimiza azma zake, hii ni culture ya namna gani if I may ask? Kama unavyo sema ndugu GEZA the most culprit katika sakata ili wenda ikawa ni makundi ndani ya chama chake - sielewi kabisa mantiki yakutaka kumkatisha tamaa!!!.

Tukiwa wakweli ndugu Mwakyembe amepewa a tall order on a shoe string budget, yaani nilipo ona wameweza kufanya majaribio ya kusafirisha abiria in no time nilijuwa jamaa huyo sio mtu wa kawaida hata kidogo, nilijiuliza hivi huyu jamaa vipuri vya kukidhi projects hizi mbili kavipata wapi au ali-cannibilise kutoka accidented rolling stock maana aigii akilini kwamba hela alizo pewa angeweza kweli kufanikisha zoezi hili, kwa watu ambao hawaelewi mambo haya wanafikili ni kazi ndogo wanakazania eti ameshindwa ku meet deadline, yaani wanacho tafuta ateleze kidogo tu basi ajengewe HOJA ya kumuondoa fasta - watanzania bwana!!

Si hilo tu hata hili la kuhusu ATC na kutafuta wawekezaji kutoka Ujerumani nk sio jambo dogo hii inathibitisha kwamba ni mtu anaye thubutu, swali ni je haya mambo anayafanya kwa nia nzuri au kujitafutia sifa kama wengine wanavyo sema, mkuu katika hilo mimi siwezi kumuhukumu, anaye weza kufahamu udani wa moyo wake ni his MAKER sisi la kufanya ni kumpongeza na kumtia MOYO.

Geza umenichekesha kidogo, sina shaka unajuwa kwamba picha zilizo tolewa zikionyesha eti treni za Nairobi wakikejeli za kwetu - mkuu picha hizo zimetolewa kwenye chapisho la International Railway Journal hazihusu train za Nairobi hata kidogo, ingekuwa picha hiyo imetolewa na Wakenya ninge elewa lakini inapo kuja Watanzania kukejeli Reli/Train zao ndio inaonyesha tuna matatizo ya aina fulani si bure.
 
watu wana upuuzi mmoja kuna mtu ametoa picha za treni za Nairobi na akaanza kukejeli kuhusu za kwetu wakati inajulikana pasi shaka kuwa Mwakyembe ametumia bajeti isiyozidi Tshs 4 bio. kuanzisha commuter trains kwa kupitia mabehewa, njia na vipuri tulivyonavyo na si vipya! Sasa badala ya kumpongeza kwa kutoa ajira na kutumia gharama kidogo watu wana CCM wa makundi (i guess) wanaanza kumfitinisha wakati huyu huyu Mwakyembe tumemuona akisaini air agreements na kutafuta wawekezaji wa Railway ya kati huko Ujerumani katika kipindi kisichopungua miezi sita tangu akwae wizara ile! na pia tumemuona huyuhuyu Mwakyembe akiwaajibisha watu mafisadi katika mashirika na pia tumemuona akikataa ku-extend leasing agreement ya aircraft za ATC toka Dubai firm kwa vile zilikuwa hazina manufaa! Kusema kweli kuna watu wanaudhi na huwa sidiriki kusita kuwatukana maana akili zao nathani ni punje ya mchele! Wamuache jamaa afanye kazi zake kwa nafasi tunajua hata bandari inatengamaa kwa kasi ya ajabu! Mie nina uhakika kwa usimamizi wa mwakyembe hata haya mabehewa tutakayotumia yanaweza kununua mabehewa mapya kabisa mbali na njia za usafiri (reli) kupanuka!

tena kwa sasa pale bandarini kutoa gari huchukui muda mrefu kama ilivyokuwa zamani,tatizo ni wafanyabiashara wa mabasi ya daladala hapo dsm wanadhani uwepo wa train ndio kufa kwa biashara zao,sasa hatuwezi kuwafaidisha wachache na kuwaumiza watanzania waliowengi,na kama ni hivyo basi nchi zilizoendelea zisingekuwa na subway ama town train ili kuwalinda wafanyabiashara wa mabasi.
tuache upuuzi watz,tuwape nafasi mawaziri wanaonyesha mwanga,na ni kweli inawezekana tatizo kuna vikwazo vingi sana moja wapo ni mtoa mada hii
 
Sasa Mwakyembe mapovu ya nini tena??? Mbona unaanza mipasho??? Au ulitaka tukae kimya tuu ilihali oktoba ndo hii??? Vipi tena mzee wa Polonium 210, bado born marrows zinaleta shida??? Acha zako bhana, we tenga kitu reli hapo sie tukwee treni, acha longolongo.
 
tena kwa sasa pale bandarini kutoa gari huchukui muda mrefu kama ilivyokuwa zamani,tatizo ni wafanyabiashara wa mabasi ya daladala hapo dsm wanadhani uwepo wa train ndio kufa kwa biashara zao,sasa hatuwezi kuwafaidisha wachache na kuwaumiza watanzania waliowengi,na kama ni hivyo basi nchi zilizoendelea zisingekuwa na subway ama town train ili kuwalinda wafanyabiashara wa mabasi.
tuache upuuzi watz,tuwape nafasi mawaziri wanaonyesha mwanga,na ni kweli inawezekana tatizo kuna vikwazo vingi sana moja wapo ni mtoa mada hii

Well said, well done MKUU.
 
Jamani mfumo ukiwa mbovu si rahisi kwa mtendaji mmoja mmoja kufanikisha jambo hata kama ana nia sana kufanya hivyo. Bila mabadiliko makubwa ya kimfumo Tanzania tutabaki watu wa kulalamika kila upande na kila uchao.
 
Crucifix, heri hata usihangaike na hawa wapuuzi, Tanzania haitasogea hadi mapinduzi ya kifikra yafanyike na watu kama hao walio usingizini waamshwe ikibidi hata kwa mijeledi. Ni Mwakyembe mwenyewe aliyekurupuka na kuwapa matumaini Watanzania kwa kutangaza tena kwa mbwembwe kwamba treni zingeanza mwezi Oktoba.

Nakubaliana na wewe, viongozi wengi Mwakyembe akiwa mmoja wao wamesahau wapiga kura ni waajiri/wateja wao. Tunapaswa kupewa taarifa sahihi na siyo kutufanya kama watoto wadogo, hakuna aliyemlazimisha kutangaza kuwa usafiri wa reli utaanza Oktoba, na kwa mtizamo huo huo alipaswa kuja kusema kama haitawezekana tena kuanza oktoba, basi lini utaanza badala ya kutoa kashfa. Ni dharau ya ajabu waziri kuamini anawajibika kwa Rais pekee na si kwa wapiga kura/walipa kodi.
 
huyo mwakyembe msanii hana jipya Tazara aliahid mishahara ya miez 2 tangu mwez wa 6 mpaka leo kapotea...tren unandaa behewa vituo huna si uhuni huo watu watapakia kwa kamba?..
 
wabongo kelele nyingi sana,hampendi kuona watu wakifanikiwa ktk malengo yao,makyembe hajasema kuwa reli za dsm zitaanza baada ya miezi 6,ila alichokisema ni ukarabati wa reli ambao hauingiliani na mtandao wa reli za dsm

tuache kulazimisha mambo na kuona kuwa kiongozi hafai kwa kuunganisha matukioa yasiyo fanana.namkubali makyembe kwani anasimamia kile anachokiongea,je miaka yote 50 iliyopita dsm ilikuwa hata na wazo la kuwa na train za kusafirisha abiria? tumpe nafasi makyembe naimani tutafika kule tutakako kwa kuwatumia hawa mawaziri wa 3 yaani
1.mwakyembe
2.kagasheki
3.magufuri
wanasimia kile wakisemacho,tusilete propaganda hapa za kutaka kumwangusha na kuona si mkweli.

Mkuu wangu kwa mawazo haya hauna tofauti na wale wanaopewa pilau,tshirts,na pombe za kienyeji wakaipigia kura CCM! Pili nikujulishe kama wakati wa uongozi wa Mwalimu ulikua bado mdogo ama hujafika mjini,aliondoka madarakani mipango hii ya kuwa train kwa usafirishaji wa mizigo na abiria imeisha andaliwa! Ni watawala wavivu na dhaifu toka chama chako cha CCM waliofuata waliharibu kila kitu! Mfano kulikua na njia ya reli ya kutoka mjini kwenda Wazo,wenzako wameiua na kugawiana viwanja. Matokeo milori mikubwa inayobeba sementi inatuharibia barabara na kusababisha ajali kila siku!
 
Please revisit my post, kama una an axe to grind na Mh.Mwakyembe please keep it to yourself - reading between the lines unaonekana wazi wazi una chuki binafsi na Mh.Mwakyembe!!! Hebu come clean utueleze kama na wewe au ndugu/jamaa yako wamekwaa upanga wa Mwakyembe katika harakati zake za kuweka mambo sawa, ukajikuta unakuwa muhanga wa fagio lake la CHUMA, chuki zako kwa mzalendo huyu sio za kawaida hata kidogo - hebu jaribu kusoma majibu ya watu wenye a brilliant analytical mind kama GEZA hapo juu, compare na ku-contrast majibu ya kwako - baada ya zoezi hilo nadhani utapa picha kamili ulivyo kuwa wired, usifikili nashindwa kutumia tirade kama za kwako a MEGATIMES - kumbuka hapa tunabadilishana mawazo sio kutuniana misuri.

Niwe na grind na Mwakyembe kwani ananilisha? we ***** kweli. naongelea deadline aliyoset yeye mwenyewe na sio kitu kingine. Kama hawezi kusimamia maneno yake yeye mwenyewe ina maana ni debe tupu haliachi kelele!
 
Nakubaliana na wewe, viongozi wengi Mwakyembe akiwa mmoja wao wamesahau wapiga kura ni waajiri/wateja wao. Tunapaswa kupewa taarifa sahihi na siyo kutufanya kama watoto wadogo, hakuna aliyemlazimisha kutangaza kuwa usafiri wa reli utaanza Oktoba, na kwa mtizamo huo huo alipaswa kuja kusema kama haitawezekana tena kuanza oktoba, basi lini utaanza badala ya kutoa kashfa. Ni dharau ya ajabu waziri kuamini anawajibika kwa Rais pekee na si kwa wapiga kura/walipa kodi.

Mkuu tuko pamoja, hakulazimishwa! Na asingeweka tarehe, wala tusingehangaika nae; tungejua ni uongo wao wa siku zote. Lakini kaja na staili za kina 'obama' kuweka deadline, sasa imemshinda anaanza eti hata tarehe 32 ipo oktoba....
 
Aliyeleta mada hii sitaki kuamini kuwa ana chuki binafsi na mwakyembe na kama ni kweli basi atakuwa miongoni mwa waliotimuliwa na mwakyembe. Kwa upande wangu mwakyembe bado hajaangukia kwennye lawama kwani oktoba haijesha na ndio maana hakutaja tar. Hata hiyo KLM uliyotolea mfano na ukasema kama inaruka 11:45 basi huanza kutembea na dakika 40 hii nayo kisha ifanya kwa kuzitest treni zote mbili kwahiyo wewe endelea kuamini kuwa mko tayari ndani ya ndege na muda wowote ndani ya mwezi huu itaruka. Mwisho nakushauri uwe mvumilivu,wizara kakabidhiwa juzi na kwa juhudi zake binafsi kaibuka na mpango huo hata miezi 3 bado kuisha wewe subira imekushinda? Subiri kwanza oktoba ikiisha ndio urejee na lawama zako.
 
MAJIBU 10 BORA YA MAWAZIRI WETU...
1. Jambo hili tumelisikia, limetugusa, tunalitafakari na tunaamini tutalipatia ufumbuzi.
2. Serikali ina mkakati kabambe.
3. swala hili liko ktk mchakato na tutawajulisha wananchi litakapokamilika.
4. Mipango na mikakati imekamilika na sasa tuko na mazungumzo na wafadhili.
5. Sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha tunaitatua kero hiyo.
6. Lakini pia kufikia malengo ya milenia ifikapo 2015.
7. Hili jambo hata sisi linatunyima usingizi kwa kweli.
8. serikali inajitahidi ila kuna changamoto nyingi.
9. Tunajadiliana na timu ya wataalamu wetu.
10. Serikali imeunda tume...
 
1. sina chuki binafsi na Mwakyembe, nampenda na nilimuombea lipokuwa anaumwa
2. oktoba 6 leo......
3. lini hii treni itaruka? mimi ni mtumiaji wa public transport.....
4. wizara hajapewa juzi bana, ni miezi sasa.....aache visingizio
5. juhudi binafsi? mi nilijua ni kazi ya wizara

Tafakari. Chukua hatua
 
Dr. Mwakyembe amebebeshwa bomu kumlipua kisiasa, hizo train zitahujumiwa na mwisho wa siku tusubiri kuzika na kuuguza maelfu ya watanzana. There are a lot of questions need to answered kabla ya huo usafiri kuanza,
1) Ubora wa hayo mabehewa na usalama wa njia za reli
2) Ubora wa vituo na usalama wa abiria
3) Usimamizi na ukusunyaji wa nauli
and many more
 
MAJIBU 10 BORA YA MAWAZIRI WETU...
1. Jambo hili tumelisikia, limetugusa, tunalitafakari na tunaamini tutalipatia ufumbuzi.
2. Serikali ina mkakati kabambe.
3. swala hili liko ktk mchakato na tutawajulisha wananchi litakapokamilika.
4. Mipango na mikakati imekamilika na sasa tuko na mazungumzo na wafadhili.
5. Sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha tunaitatua kero hiyo.
6. Lakini pia kufikia malengo ya milenia ifikapo 2015.
7. Hili jambo hata sisi linatunyima usingizi kwa kweli.
8. serikali inajitahidi ila kuna changamoto nyingi.
9. Tunajadiliana na timu ya wataalamu wetu.
10. Serikali imeunda tume...
Hebu tupe na ahadi za ze piipoooz!
Kwa ulinganishi tu.
 
Dr. Mwakyembe amebebeshwa bomu kumlipua kisiasa, hizo train zitahujumiwa na mwisho wa siku tusubiri kuzika na kuuguza maelfu ya watanzana. There are a lot of questions need to answered kabla ya huo usafiri kuanza,
1) Ubora wa hayo mabehewa na usalama wa njia za reli
2) Ubora wa vituo na usalama wa abiria
3) Usimamizi na ukusunyaji wa nauli
and many more
Watanzania kwa kuwa na negative trains of thought hamjambo.

Kwa hiyo kwa sababu hizo hapo juu usafiri wa treni wala usifikiriwe?
People love to live in their own boxes of thoughts!
 
Watanzania kwa kuwa na negative trains of thought hamjambo.

Kwa hiyo kwa sababu hizo hapo juu usafiri wa treni wala usifikiriwe?
People love to live in their own boxes of thoughts!
To me usafiri ni jambo zuri, but safety is my first concern. Unasafirisha watu kwa treni wakati reli mbovu, hiyo akili? Tembea duniani ujifunze miundombinu ya wenzetu wanaofanya usafiri kama huo, kabla ya kuita watu negative
 
Back
Top Bottom