Mwakyembe umechemka, acha kujing'ata ulimi.....

Mwakyembe umechemka, acha kujing'ata ulimi.....

so? ina maana hukumuona alivyohangaika kuhakikisha hiyo tarehe treni zinatembea? au hujui kuwa kutotembea kumetokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wake! btw hizo wiki mbili ndo zinakutoa povu namna hiyo au ufuasi wako wa makundi pinzani yasiyolala kuona Mwakyembe akitekeleza ahadi zake za maendeleo

Hapa tunahitaji utendaji mkuu, wala si kwa sababu ya makundi pinzani. Naamini kila mtu (hasa sisi tulio dar) alikua anasubiri kuona matokeo ya ahadi. Pia kama kuna tatizo lingetolewa ufafanuzi makini. Tatizo la viongozi wetu mara nyingine hulewa sifa hata wanatoa ahadi zisizo na halisia katika utekelezaji. Hakuna aliyemlazimisha kutoa ahadi. Kama ni suala la mda alitakiwa ajadiliane na wataalamu wake ili wampe uhalisia wa kinachotakiwa kufanyika na muda wake. Hapa ndo viongozi wetu wajifunze kutumia wataalamu, wanafikiri uwezo wao wa kuongoza kisiasa ndo kila kitu! Wakati mwingine unahitaji (technical personnel) ili kufanikisha jambo. So ajipange, katika hili kweli alikurupuka na inampasa atutake radhi
 
Hapa tunahitaji utendaji mkuu, wala si kwa sababu ya makundi pinzani. Naamini kila mtu (hasa sisi tulio dar) alikua anasubiri kuona matokeo ya ahadi. Pia kama kuna tatizo lingetolewa ufafanuzi makini. Tatizo la viongozi wetu mara nyingine hulewa sifa hata wanatoa ahadi zisizo na halisia katika utekelezaji. Hakuna aliyemlazimisha kutoa ahadi. Kama ni suala la mda alitakiwa ajadiliane na wataalamu wake ili wampe uhalisia wa kinachotakiwa kufanyika na muda wake. Hapa ndo viongozi wetu wajifunze kutumia wataalamu, wanafikiri uwezo wao wa kuongoza kisiasa ndo kila kitu! Wakati mwingine unahitaji (technical personnel) ili kufanikisha jambo. So ajipange, katika hili kweli alikurupuka na inampasa atutake radhi

Tena ukizingatia hii sio ahadi yake ya kwanza! Zipo kadhaa na hajatekeleza.....kazi kutafuta sifa tu!
 
Tafuta unae muamini mweke ashughulikie ishu nzm ya tren utakavyo wew. Otherwyz acha kubwabwaja!
 
Tuache siasa, bandarini tunaua uchumi
Mwandishi wetu
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe sasa ametangaza kupokea ripoti ya
tume aliyoiunda kuchunguza tuhuma ambazo zimekuwa zikidaiwa kuwa chanzo cha
kuzorota kwa huduma za bandari zetu na hasa Bandari ya Dar es Salaam.
Tuhuma za Dk. Mwakyembe wakati akiunda tume yake na hata sasa, zinaelekezwa
tu kwa uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzani (TPA) na zaidi viongozi maalumu
anaowalenga yeye tu na mfumo mzima katika sekta husika.
Kwa kuwa waziri hana taaluma katika maswala ya usafiri kwa njia ya majini bandari
nikiwa kama mmoja wa wadau kwenye sekta hiyo naamini sasa atakuwa amepata
ufahamu wa kuifahamu vema sekta nzima ikiwa ni pamoja na mfumo mzima wa
kupokea, kuhifadhi na kusafirisha mizigo ipitayo kwenye bandari zetu zikiwamo zile
za maziwa.
Kwa wadau waliobobea kwenye eneo hili na ambao biashara zao za kila siku
hutegemea ufanisi endelevu wa kila mdau kwenye eneo hili wanategemea kuona
ripoti yenye weledi na muonekano wa kitaaluma kuliko ya kutafuta makosa ndani
ya mdau mmoja.
Kwa maelezo ya Dk. Mwakyembe na wanaoungana naye, kwa sasa inaonekana
tuhuma zinaelekezwa TPA ili kuhalalisha mbele ya umma kwamba Bandari ya Dar es
Salaam kuna uozo, wizi, rushwa na kila aina ya uovu unaofahamika duniani.
Baadhi ya wadau wanaona matamshi kama haya na ambayo hayajahusisha wadau
wote kwa kina yanatoa taswira ambayo inaweza kuwapoteza wateja kabisa hata
wateja wachache tulionao Tanzania.
Waziri anadiriki kusema eti amehakikishiwa na mawaziri wenzake wa uchukuzi wa
nchi jirani kwamba nchi hizo zitaendelea kuzitumia bandari zetu hasa ya Dar es
Salaam.
Baadhi ya wadau na wafanyabiashara wanasema kwamba mawaziri siyo wanaofanya
biashara ila kazi yao ni kuweka na kusimamia sera ya biashara husika.
Tunafahau na waziri lazima afahamu kwamba bandari haiwezi kufanya kazi zake bila
kuhusisha kwa umakini sekta nyinginezo na mfanyabiashara mmoja anayemiliki meli
kubwa duniani ameliambia gazeti hili wazi kwa kusema, “Bandari haiwezi kufanya
kazi kivyakevyake kama kitu kilichojitenga bila vifaa, watu au taasisi na mitandao
inayopaswa kufanya nayo kazi!”
Hali kadhalika bandari haiwezi kufanya kazi ikawa na ufanisi bila kuwa na
viunganishi thabiti kwa maana ya barabara, reli na mabomba ya mafuta.
Pia bandari haiwezi kuwa na ufanisi wa kupokea mizigo mingi kwa wakati mmoja
kama haina miondombinu ya kutosha na ya kisasa kama gati za kutosha na zenye
kina kinachoweza kuegesha meli kubwakubwa ambazo zinaweza kutia nanga hapa
kama zilivyo kwenye bandari zinazoshindana na Bandari ya Dar es Salaam.
Ikumbukwe baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 wa Kenya kugubikwa na vurugu,
wafanyabiashara wa Uganda walipata shida kutokana na mizigo yao kukwama
kwenye Bandari ya Mombasa kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka hali ilipotengemaa.
Ni wakati huo ujumbe mzito ulikuja kutoka Uganda ukiongozwa na Waziri wa
Uchukuzi, kuja kuona uwezekano wa kutumia Bandari ya Dar es Salaam na kuahidi
kwamba Uganda ingetumia kupitisha asilimia 30 ya mizigo yake hapa kama mbadala
wa Bandari ya Mombasa.
TPA ilibidi iweke wakala kule Uganda kama njia ya kuwavutia Waganda lakini
wafanyabiashara wamekuwa wanasita kutokana na ukweli kwamba miundombinu
yetu bado ni hafifu.
Kukosekana kwa reli kumefanya Waganda waghairi kutokana na gharama kubwa kwa
njia ya barabara wakilinganisha na umbali wa kutoka Mombasa mpaka Kampala.
Hoja hapa ni kwamba pamoja na kuhakikishiwa na Waziri wa Uchukuzi wa Uganda
wa kutoa ahadi ya asilimia 30 ya mizigo ya Uganda kupitia hapa imekuwa ni
kitendawili kutokana na changamoto za mapungufu katika mtandao wetu wa njia za
usafirishaji mpaka mzigo ufike Uganda au utoke Uganda mpaka bandarini Dar es
Salaam.
Kama wadau, tunaona changamoto za uendeshaji bandari ziangaliwe kitaaluma zaidi
kuliko kuchukua mrengo wa kisiasa.
Inashangaza kuona inachukua zaidi ya miaka mitano kuamua namna ya kuongeza
gati mbili kwa nia ya kuongeza ufanisi kwenye sekta nzima kwa njia ya bahari
ambayo faida yake yake ni kuongeza pato la taifa kwa kuwa kila mdau kwenye
biashara inayohusiana na Bandari ya Dar es Salaam atakuwa anachangia kwa kiasi
kikubwa kwenye GDP!
Mombasa wanaongeza gati nne kwenye katika bandari yao na mkandarasi yuko
kazini mwaka wa pili sasa.
Pia wanajenga bandari mpya ya Lamu ambayo pia mkandarasi yuko kazini; hapa
tunalumbana wakati wenzetu wanashangilia kwa ujinga wetu.
Waziri anahusisha vipi TPA peke yake na wizi wa makontena?! Mizigo hutolewa
bandarini kwa njia ya nyaraka ambazo zina mlolongo mrefu.
Je, kama nyaraka za mzigo husika zimeghushiwa wakati mzigo unapotolewa
bandarini au toka kwenye eneo linalomilikiwa TICTS, bandari au mkaguzi mkuu wa
bandari atajuaje?
Tumeona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna makontena yameshikwa huko
Hongkong yakiwa na pembe za ndovu zikitokea Dar na Mombasa.
Je, hapa TPA inahusika vipi wakati anayetakiwa kufungua na kukagua makontena
kabla hayajapelekwa kwenye meli kupakiwa ni ofisa forodha?
Ni vema wanasiasa wakajifunza kwanza jinsi bandari inavyofanya kazi kwa
kushirikiana na taasisi nyingine ndani ya mfumo kabla ya kufanya maamuzi ambayo
kwa kiasi kikubwa yatakuwa hayajengi zaidi ni kuuvuruga mfumo wote wa
usafirishaji kwa njia ya majini na kuua uchumi wetu kwa maslahi ya kisiasa.
juu
Habari Mpya | Matangazo | Bei zetu | Wasiliana nasi

Tuache siasa, bandarini tunaua uchumi
 
Wadanganyika tuwe na uwezobasi wakutumia akili zetu japokwa kusema ukweli, Mwakyembe ni mzuri wa kujenga hoja lakini kwa mtu yoyote ambaye ni makini na mkweli kwa nafsi yake ulipaswa kumtambua ni mtu wa aina gani baada ya sakata la Richmond maana alikuwa yupo radhi kwa watanzania kuteseka na kunyanyasika kwa ufisadi uliokuwa wazi kabisa kuliko kukiumbua chama chake na kuilinda serikali iliyo kuwepo madarakani. Ndo maana amezawadiwa uwaziri so huo ni muendelezo wa porojo zake na uwezo wake wa kujenga hoja lakini kwa watu makini tulijua mapema kuwa ni siasa za mimi ndiye muweza wa kutatua matatizo yenu. WANAO AMINI KUWA NI MCHAPA KAZI MKO SAWA LAKINI UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI TU
 
Mwacheni Mwakyembe afanya kazi yake. Problem si Mwakyembe, ni mfumo wa kitaasisi. Kama umewahi kufanya kazi serikalini hapa Tanzania, kuna uzembe mkubwa na urasimu wa kupindukia. We need radical changes of the institutions and leadership in some of them. Wako watu walio kimaslahi binafsi zaidi kuliko maslahi ya taifa. Hii ndio maana ATC na reli ziko kaburini. Duniani kote usafiri rahisi kujenga na gharama nafuu za usafirishaji ni reli, lakini hapa kwetu tumeamua kuua reli na kutumia resources nyingi kwenye barabara. I would expect, kwa nchi kubwa kama ya kwetu barabara zingekuwa zina-complement railway lines maeneo mengine. Mizingo inayobebwa na reli always ni bulky. With reliable power, usafiri wa reli unaweza pia kuongeza efficiency ya uchumi. Mtu unaweza kaa Bagamoyo au Morogoro na kufanya kazi Dar. Tatizo kubwa la nchi yetu ni ubinafsi wa viongozi na kukosa utashi. Kama rais au waziri husika ana malori au mabasi,, unategemea kasi ya utekelezaji wa lolote linalohusu uboreshaji wa usafiri nchini??
 
Mhh mimi sitaki hata kuchangia kuhusu lini inaanza!! Maandalizi tu yanatosha kutuonyesha kuwa hizo ni ndoto!! Maana hatakwenye ile reli iliyopo hatujaona vituo wala platform kwa ajili ya abiria!!!

Mimi nilidhani wanakarabati reli, pamoja na kuweka miundo mbinu japo kiasi ya kuwezesha "commuter train" All we see mabehewa yanapakwa rangi ya nyumba tu, na wanasiasa wana-test route isiyokuwa na vituo!!!

Jamaa zangu walioko bongo wanansema ni maneno tu, kama kawaida!!!
mI NIPO DAR NA TREN IMETESTIWA NA SOON INAANZA KAZI MAKELELE YA NINI NINYI WATU MBONA HAMNA SHUKRANI, HEBU TUWE NA USTAARABU WA KUJALI JUHUDI ZA WENGINE VINGINEVYO HUU MNAOLETA NI UBINAFSI WA KUTOJALI MEMA YA WENZENU. MWENZENU KAWEZA KUONYESHA KWAMBA KAZI ANAIWEZA SASA NINYI VP HAPO? AU MNAWEZA KUPIKA MAJUNGU, WATU WENGINE WANAKERA KWELI. MWAKYEMBE NI JEMBE PENDA MSIPENDE NA HULKA ZENU ZA WIVU NA HUSDA.
 
mwakyembe ni bogus sana basi tu nashangaa ga wanaomsifia ....
 
mI NIPO DAR NA TREN IMETESTIWA NA SOON INAANZA KAZI MAKELELE YA NINI NINYI WATU MBONA HAMNA SHUKRANI, HEBU TUWE NA USTAARABU WA KUJALI JUHUDI ZA WENGINE VINGINEVYO HUU MNAOLETA NI UBINAFSI WA KUTOJALI MEMA YA WENZENU. MWENZENU KAWEZA KUONYESHA KWAMBA KAZI ANAIWEZA SASA NINYI VP HAPO? AU MNAWEZA KUPIKA MAJUNGU, WATU WENGINE WANAKERA KWELI. MWAKYEMBE NI JEMBE PENDA MSIPENDE NA HULKA ZENU ZA WIVU NA HUSDA.

Ok, wengine hatuna majingu, tumezoea ya CCM, huwa ni blah blah tu!! Mkuu ikianza we noo na picha tu huku tujionee. Kwa kiasi ambazo tumekwisha danganywa, we cant take any risk any more!!!

Mapovu ya nini?
 
Ni kweli aliahidi October na bado hajafanikiwa kutimiza alichoahidi, lakini angalau tumeona jitihada alizoweka na nia ya dhati aliyonayo. Inawezekana anakwamishwa au amekwama lakini hata jitihada kidogo alizofanya ni sawa na bure? Mawaziri wangapi wamekaa pale kwenye wizara husika hata wazo wahakuwa nalo? Mnyonge mnyongeni lakini ujira wake mpatieni.

Profesa Mwandosya akiwa waziri wa uchukuzi kipindi cha mkapa aliwahi kuizindua hiyo treni, na tangu ilipozinduliwa haikufanya safari hata moja hadi Mwakyembe alipolirudisha hilo wazo tena.

Ndugu, ni kwamba watu wamechoka kuishia kuona nia na jitihada za dhati kama unavyosema zisizo na mwisho. Kama amekwama au amekwamishwa aseme wazi ili umma ujue hilo kuliko kukaa kimya.
 
Profesa Mwandosya akiwa waziri wa uchukuzi kipindi cha mkapa aliwahi kuizindua hiyo treni, na tangu ilipozinduliwa haikufanya safari hata moja hadi Mwakyembe alipolirudisha hilo wazo tena.

Ndugu, ni kwamba watu wamechoka kuishia kuona nia na jitihada za dhati kama unavyosema zisizo na mwisho. Kama amekwama au amekwamishwa aseme wazi ili umma ujue hilo kuliko kukaa kimya.

Mkuu haraka haraka haina baraka, Watanzania mna maneno sana. Akikiuka taratibu moja tu ndo mtakuwa wa kwanza kusema amevunja sheria, amekiuka taratibu nk, kwani we hujasikia SUMATRA wameitisha mkutano wa wadau ili kupata mapendekezo ya bei ya nauli? hii ni moja ya taratibu iliyopo. Baadhi ya taratibu zinaweza kuwa ndo sababu za kuchelewesha. Waliosema its better late than never walimaanisha mkuu.
 
Back
Top Bottom