Kuhani.. mitandao inaweza kutumika kurecruit, kupanga, na kutekeleza vitendo vya kihalifu. Katika uhuru wa maoni na mawazo ni vizuri kujua mawazo mabaya nayo yapa, lakini ni jambo jingine kuyakubali, kuyahifadhi na kuyavumilia. Na ni hatari zaidi kutoa nafasi kwa watu kusambaza mawazo ya kihalifu kwa kisingizio cha uhuru wa maoni. Kwenye ukumbi uliojaa watu kama ukumbi wa sinema mtu akipiga kelele "moto, moto" kiutani akidai ni uhuru wa maoni mtu huyo atashitakiwa kiuhalifu kama kutatokea madhara kwa watu kwa sababu ya kukimbia kuokoa maisha yao.
Mawazo ya kokolo ni zaidi ya uhuru wa maoni, ni mawazo yenye kupakana na kupanga uhalifu. Hivi kweli Mwakyembe akifa (mungu aepushie mbali) halafu mmoja wa aliowataja hapo tukasikia ameraruriwa na risasi, JF tutaweza kusimama na kusema hatukuonywa? No sir, mawazo ya namna hiyo hayana nafasi hapa.