Mwakyembe augua ghafla Bungeni

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge kuchunguza mkataba wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameugua ghafla akiwa bungeni na kulazimika kukimbizwa katika zahanati ya bunge.

Taarifa zinasema kuwa baada ya kuchunguzwa,ilibainika kuwa alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu.

Mwakyembe anasema kuwa alianza kusikia kizunguzungu na hali ilipokuwa mbaya alitoka nje akisindikizwa na baadhi ya wabunge hadi katika zahanati hiyo ba Bunge.

Baadaye alisema kuwa hiyo ilikuwa ni homa ya kawaida tu
 
Du!

Basi twamtakia kheri mheshimiwa Mwakyembe apate nafuu haraka na aepushwe na midubwana na mabalaa haya.

Inaeleweaka kwamba kwa sasa mheshimiwa ana kazi ya kutazama mabegani yake kila aendako.
 
Dah!
watu tulijua tayari amekula chakula kibovu maana huko Dom pana historia yake kwa kunyonga wapigania haki za walalahoi walio sahaulika katika nchi hii,.
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati teule ya bunge kuchunguza mkataba wa Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameugua ghafla akiwa bungeni na kulazimika kukimbizwa katika zahanati ya bunge.
Taarifa zinasema kuwa baada ya kuchunguzwa,ilibainika kuwa alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu.
Mwakyembe anasema kuwa alianza kusikia kizunguzungu na hali ilipokuwa mbaya alitoka nje akisindikizwa na baadhi ya wabunge hadi katika zahanati hiyo ba Bunge.
Baadaye alisema kuwa hiyo ilikuwa ni homa ya kawaida tu

Nuhakika itakuwa homa ya kawaida tu. Sisi tunamwombea 24 hrs na massage kutoka kwa e mkuu aliye juu yaani SIMBA WA YUDA ametuhakikishia kuwa hawezi kumchukua mpaka ametimiza kazi aliyomtuma kuifanya baada ya sisi kumlilia na kutubu dhambi ya kuwaachia viongozi wetu matapeli watoe unabii wa uwongo (changuo la mungu). Asante Emanuel!
 
Dah!
watu tulijua tayari amekula chakula kibovu maana huko Dom pana historia yake kwa kunyonga wapigania haki za walalahoi walio sahaulika katika nchi hii,.

Hata hivyo hatujawa na hakika. Viongozi wa Tanzania wana jeuri bwana. Wanaweza kufanya lolote tu kama ukiingiz kwenye anga zao.
 
Daktari acheni kuunderstimate mambo. swala la mtu kusikia usingizi sio "homa tu ya kawaida". Mwakyembe ashauriwe kuonana na specialist physician kwa vipimo zaidi.
 
Nuhakika itakuwa homa ya kawaida tu. Sisi tunamwombea 24 hrs na massage kutoka kwa e mkuu aliye juu yaani SIMBA WA YUDA ametuhakikishia kuwa hawezi kumchukua mpaka ametimiza kazi aliyomtuma kuifanya baada ya sisi kumlilia na kutubu dhambi ya kuwaachia viongozi wetu matapeli watoe unabii wa uwongo (changuo la mungu). Asante Emanuel!

wow..........hiyo service ni free au ??
 
Maadam yeye alishajua matatizo yake, hofu kwetu inapungua. Still anatakiwa kuendelea kuwa makini na nyendo zake especially inapofika mambo ya makulakula.
 
Bora iwe ni magonjwa ya kawaida.
Ila jinsi huyu bwana alivyojijengea maadui, napate wasiwasi kiaina
 
Tunamwombe mheshimiwa Dr. Mwakyembe apate nafuu haraka na kurudi kuendelea na majukumu yake bungeni.

Ila nao waheshimiwa inabidi wajitahidi mazoezi maana huo ugonjwa utawamaliza.

Ninawashangaa vigogo wetu yaani hata meter 500 anaenda kwa gari. Jamani tuache hayo magari muda wote hasa kule wilayani ambako mtu unaweza kutembea au kutumia baiskeli bila matatizo.

Middle class ya Tanzania angalieni huo ugonjwa kwa faida zenu binafsi pamoja na taifa.
 
Taarifa Ni Kwamba Jana Baada Ya Bunge Kufungwa Jioni Mbunge Moja Aliomba Aingie Achukuwe Kitu Alichosahau Ndani. Camera Za Bunge Zilimnasa Ananyunyiza Dawa Kwenye Viti Vya Watu Na Moja Ya Viti Kilikuwa Ni Cha Mwakyembe. Mimi Sisemi Ndiyo Maana Kaanguka Lakini Mambo Hayo Huwezi Kuyapuuza.
 
Haya ya kweli au ndiyo twist ya habari.................... Pole Prof. Mwakyembe tunakuombea afya njema!!!!
 
Taarifa Ni Kwamba Jana Baada Ya Bunge Kufungwa Jioni Mbunge Moja Aliomba Aingie Achukuwe Kitu Alichosahau Ndani. Camera Za Bunge Zilimnasa Ananyunyiza Dawa Kwenye Viti Vya Watu Na Moja Ya Viti Kilikuwa Ni Cha Mwakyembe. Mimi Sisemi Ndiyo Maana Kaanguka Lakini Mambo Hayo Huwezi Kuyapuuza.

vooodoo jamani, na wabunge pia!!?? sitaki kuamini hadi atajwe huyo mchawi! kwikwikwi...
 
Hallo Tujisent,

Please huyo mtu ingependeza angetajwa. Tupe habari ili atumiwe nyota huyo kwani hawa waheshimiwa sasa wanataka kutugeuza ndondocha na si misukule tena. What kind of a country is this.
 
Tujisenti,

Mwaga habari utuletee huyo mmwaga vijidawa!!
. Asante kwa taarifa, tunamwombea apone.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom