Mwigulu Nchemba na mkandarasi, China Civil Engineering construction corporation biashara yenu ina harufu mbaya

Apr 24, 2011
29
542
Mwigulu Nchemba, mmeingia makubaliano ya awali na kampuni ya China Civil Engineering construction corporation kwa utaratibu wa single source (bila ushindani) yenye thamani ya Shs. 6,698,935,255,040.00 kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ bila ushindani.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation alipewa ujenzi wa lot Na. 5, Isaka – Mwanza (249 km). Miezi 16 amejenga 4.4% pekee na HAKUNA hata kipande kimoja cha reli ameweka katika miezi 16. Mwigulu anasema bungeni kwamba haukuwepo ufadhili wa kifedha. Ni mzaha.

Utaratibu wa ‘single source’ ni LAZIMA mkandarasi awe amekidhi vigezo na uwezo. Huyu mkandarasi wa Mwigulu hana sifa hizo. Miezi 16 ameshindwa kupeleka hata ambulance, hakuna usala kwa wafanyakazi, na amefanya kazi kwa 4.4%. Mkandarasi huyu hajakidhi vigezo vya single source.

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation tena kapewa ujenzi wa lot Na. 6 ya kutoka Tabora - Kigoma (411km). Na gharama za ujenzi wake ni US$4.8M (Sh.11.1bn) kwa kila 1km. Hivyo kwa 411km mkandarasi atatumia Shs. 4.6 trilioni. Kapewa tender bila ushindani.

Phase 1 Dar es Salaam – Morogoro (300 km) kandarasi ni Yapi Merkezi na Mota Engil Africa. Phase 2 Morogoro- Makutupora (422 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Phase 3 Makutupora–Tabora (294 km) kandarasi ni Yapi Merkezi. Kumbuka, phase 3 imegharimu US$1.9 billion (TZS 4.4 trillion)

Mkandarasi China Civil Engineering construction corporation (CCECC) ndugu Mwigulu, ametokea wapi hadi kupewa kandarasi ya trilioni 4.6 wakati kwa miezi 16 amejenga lot Na. 5 kwa 4.4% pekee? Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion).

China Civil Engineering construction corporation (CCECC) Tabora - Kigoma (411km) amechukua Shs. 6.7 trilioni. Zaidi ya nusu ya fedha zote ambazo zimetengwa kwa ujenzi wa Dar Es Salaam - Mwanza ujenzi wake jumla ni Shs. 14.7 trillion (US$6.4 billion). Ni UJAMBAZI hakuna shaka.

Kwamba Rais (ambaye ni mwenyekiti wa mikutano yote ya Baraza la mawaziri) hajui lolote kuhusu wizara ya fedha na mipango chini ya usimamizi wa waziri Mwigulu Nchemba kutumia single source yenye BID ID 421346 ambayo ipo secured? Opening na Closing date yake ni siku moja 04/04/2022

Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7 ya mwaka 2011 imefutwa lini? The Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) haina mamlaka tena? Zabuni shindanishi zimefutwa lini na bunge? Kwamba waziri anaweza kutumia ‘single source’ idhini ya PPRA kutoa Shs. 6.7 trilioni bila kumueleza Rais?

Utaratibu wa ununuzi katika kazi za ujenzi, ununuzi wa huduma na bidhaa kwa njia ya “single source” unasimamiwa na Kanuni ya 159, 160 na 161 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma, 2013 kama zilivyofanyiwa marekebisho na Tangazo la Serikali Na. 333. la mwaka 2016.

Kwa utaratibu wa ununuzi wa ‘single source’, PPRA inatakiwa kuhakikisha wanapata wazabuni wenye sifa, uzoefu na uwezo wa kutekeleza mikataba hiyo kwa haraka na ndani ya muda wa mkataba na kuhakikisha Serikali inapata thamani ya fedha kwa manunuzi yote yatakayofanyika.

Edward Lowassa akiwa waziri mkuu na Dk. Ibrahim Msabaha walipotimuliwa serikali kwa shinikizo la tume ya Harrison Mwakyembe kwa kushindwa kuzingatia taratibu za manunuzi na zabuni (procurement and tendering) katika kashfa ya RICHMOND. Sheria ya manunuzi ya umma ikaongezewa meno.

Richmond; kampuni ilipewa tenda ya kuzalisha umeme huku ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa hawa China Civil Engineering construction corporation nao wamepewa tenda katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Richmond; kampuni ilipewa tenda ya kuzalisha umeme huku ikiwa haina fedha, wataalam wala ofisi. Ndiyo iliondoka na Edward Lowassa. Sasa hawa China Civil Engineering construction corporation nao wamepewa tenda katika mazingira kama hayo. Mwigulu anakiri kweli hawakuwa na fedha

Athari za kutumia mzabuni mmoja kwa utaratibu wa manunuzi wa moja kwa moja ‘single source’ ni kiini cha rushwa, uzembe, upendeleo, pamoja na uwezo mdogo wa mzabuni. Ndiyo sasa tunaona yanayotokea kati ya Mwigulu Nchemba na China Civil Engineering construction corporation.

Mfumo wa ushindani wa wazabuni wengi, ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi, huchukua takriban miezi mitatu au zaidi hadi kutangazwa mshindi. kutoa zabuni bila ushindani kunaleta upendeleo kwa baadhi ya wazabuni kwa gharama za watu wengine. Rushwa inaweza kutamalaki.

Katika mfumo huu, kuna uwezekano mkubwa wa kutekeleza miradi chini ya kiwango, hili ni jambo ambalo uzoefu unaonesha yapo maeneo ambayo miradi mingi haijadumu kwa sababu ya kutekelezwa chini ya kiwango, lakini gharama za mradi zikiwa za chini. Mashaka ni makubwa sana.

Gharama za mradi zinaweza zisiwe halisi. Kwamba zinaweza kuwa gharama kubwa zaidi, maana makubaliano ndio yanasimamia gharama za mradi. SASA hili la Mwigulu kupigania kandarasi ya CCECC bila uwepo wa zabuni shindani ni jambo lenye mashaka mengi ya dhahiri na lazima tuhoji.

Ahsante pia Aeshi Hilaly, mbunge wa Sumbawanga Mjini, nimeona bungeni ukimueleza Mwigulu Nchemba kwamba wewe na kamati yako ya miundombinu mmefika hadi kwenye ujenzi, hamridhiki na ujenzi wa lot Na. 5 na kuna ufisadi mkubwa katika zabuni ya ujenzi wa lot Na. 6. Barikiwa

MMM, Martin Maranja Masese
 
kuna kipindi mnavyolalamika na haya malalamiko yenu ndio maana wengine tunasema yule Mwamba JPM alikuwa anafaa sana...

nchi hii ili mambo yaende yanahitaji, ubabe, ukatili na unyama wa hali ya juu...kifupi kuna watu wanapaswa kufa na makaburi yao yasionekane kabisa, wengine wanapaswa kukaa kwenye jela zenye mateso makali...

Mwisho kabisa, HAKUNA DEMOKRASIA KWA MPUMBAVU, vinginevyo mtalalamika sana..
 
Mchina ndiye anagharamia mradi huo, hawezi kubali hela iende kwa nchi nyingine.

Chadema mmemaliza kuomba omba Hela mitaani?

Umeshafanya retirement za mamia ya mamilioni ya Chadema uliyolipwa kwa kigezo Cha kukaa Dsm kuripoti kesi ya Mbowe ?
 
Putin bora angevamia Bongo kisha apige nuclear kizazi hiki chote kipotee.

Licha ya yote haya kujirudia kwa style tofauti tofauti miaka nenda miaka rudi, bado mitaani utakutna na raia wanaona ufahari kuvaa nguo za kijana.

Pathetic!


issue sio nguo za kijani, iwe kijani au nyeupe shida iko kwa watanzania woote tabia zinafanana pande tofauti...

bila kuangalia vyama, tuna tatizo la msingi lililoanzia mahala, either kwa waasisi au historical problems inayotukumbuka waAfrica woote...
 
upigaji huu sasa unatisha, nilifikiri Mkataba huu ni wa tangu Mwendazake, hata CAG kaonesha hela nyingi imeenda huko, sasa wajanja wanazifuatilia kupitia reli ya Isaka, duh hakuna anayefaa tena hawa vijana.
Hata Waziri wa Nishati kaomba wale wenye mafuta hata km ni kijijini kwao huko Uajemi wakamuone, hapo nina shaka na %
km una PDF fungua hiyo hapo chini ingawa CAG ana vitabu kama 9
1650130503143.png
1650130503143.png
 

Attachments

  • RIPOTI_YA_UKAGUZI_WA_MIRADI_YA_MAENDELEO__MWAKA_2020_21 (2).pdf
    3.3 MB · Views: 3
  • RIPOTI_YA_UKAGUZI_WA_MASHIRIKA_YA_UMMA_MWAKA_2020_21.pdf
    3.3 MB · Views: 5
ujinga na wizi wa kifala ni tatizo la WaAfrica woote..... kuna stages WaAfrica tumeziruka...

tunalalamikia CCM waliopo madarakani lakini wengine nasisi hukohuko sekta binafsi na mitaani ni wezi na madhulumati....

Wengi wa hawa waliopo kwenye mifumo ni ndugu zetu,na jamaa zetu na wakija kwenye misiba au harusi wanatoa mamilioni ya hela tunawashangilia na kuwasifia..
 
Wamekalia kuponda awamu iliyopita kuficha uozo wao,natamani viongozi wote waliopo wadarakani kipite kimbunga cha kifo wote wafe,maana kuhalalisha upigaji tunaoumia ni sisi waganga njaa,Samia nae yupo mawinguni tu hana habari, stupid kabisa
Waombee waishi miaka mia mbili ili waje washuhudie ujinga wao tutakapoibadilisha serikali.
 
Putin bora angevamia Bongo kisha apige nuclear kizazi hiki chote kipotee.

Licha ya yote haya kujirudia kwa style tofauti tofauti miaka nenda miaka rudi, bado mitaani utakutna na raia wanaona ufahari kuvaa nguo za kijana.

Pathetic!
🤣🤣🤣🤣watu wanalamba asali
 
51 Reactions
Reply
Back
Top Bottom