Mwakyembe arejea nchini; afya yake yaimarika

Pengine tunaweza kumshukuru Mungu, Mbunge wa Kyela Dr. Harrison Mwakyembe anaweza kutinga ofisini Jumatatu kupiga Mzigo. Mwakyembe sasa umepona njoo toa nusu ripoti ya Richmond iliyobaki, tumechoshwa na tambo za mafisadi.
 
Katika siku za karibuni, kumekua na watu kadhaa ambao wamekua wakimzulia KIFO Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, mpambanaji Dk. Harrison Mwakyembe. Baada ya taarifa hizo, watu wa karibu na mwanasiasa huyo ambaye ugonjwa wake umehusishwa na madhara yatokanayo na sumu, wamezungumza naye mara kadhaa jana na leo na kubaini kama ni mzima na afya yake inazidi kuimarika na kuwa bora zaidi ya siku anakwenda India kwa matibabu. Mmoja wa aliyezungumza naye alisema;

"Kuna post imetumwa jamii forums kwamba dr mwakyembe amefariki sio kweli, nimeongea naye kama dk ishirini zilizopita." "Dk. Anasema kwa sasa ukimuona utashangaa maana amepata nafuu ajabu."

Moani yangu: Wana JF, Mwakyembe ni binadamu na kama kiumbe yeyote hawezi kuishi milele duniani, lakini hiyo si sababu ya kumzushia mtu mauti angali hai. Wale wote wanaofanya hivyo kwa nia mbaya wajue hakuna aliye juu ya Mwenyezi Mungu na kwamba kila nafsi itaonja mauti na tumekuja kwa udong na tutarudi kwa udongo. Taarifa za msiba hazipaswi kuwa hisia bali kutoka kwenye vyanzo mahsusi.

PONA Mwakyembe pona! Taifa lahitaji mchango wako katika ukandarasi na fani nyingine! Njoo Mwakyembe! Njoo upesi!
 
Acha kupima upepo! Nikikutukana utaanza kulalamika. Tumeshaukataa huu upumbavu wa kupost taarifa zisizo na source!
 
Habari zilizotangazwa na TBC1 zinasema Dr Mwakyembe amerudi nchini leo na jumatatu ataanza kazi rasmi na ndipo ataongea na waandishi wa habari. Afya yake yaelezwa kuwa imeimarika sana.
 
Source tbc1

Dr Harison Mwakyembe ameridi leo toka Appolo tofauti na baadhi ya wadau kudai kamfuata mwl kule alikopelekwa na CCM wenzake.

Je nae atamjibu Lowasa kuwa karudi kupambana?
 
Invisible alitakiwa arushe thread kama hii tokea asubuhi, sijui alidharau maoni ya members ama hakuwa na uhakika na habari zile! Anyway, get well soon Mwakyembe, tunahamu ya kusikia ile siri nzito kutoka kwako!
 
Acha kupima upepo! Nikisema muniyo munyokwe utaanza kulalamika. Tumeshaukataa huu upumbavu wa kupost taarifa zisizo na source!

Haya ni matusi makubwa sana! jamani JF inaelekea wapi?
 
Kama amerejea na afya yake imeimarika hii ni habari njema. Tunashukuru kwa taarifa.
 
Yeye hata asiposema kuwa 'karudi kupambana' watanzania tunatambua kuwa yeye ni mpambanaji wa kweli. Karibu tena nchini na pole sana.
 
Wana JF, Nimepost hiyo thread kwa nia nzuri, Chanzo cha habari ninacho, kama mtu alikuwa anahitaji angeweza kuomba nikarudi kuleta taarifa zaidi. Ila KWA MATUSI MAZITO ALIYONITUKANA MWANA JF MWENZANGU MUNGI....... Ninafikiri zaidi uamuzi wangu wa kuendelea kutumia JF, Maana itakuwa haijengi watanzania badala yake wote tunaonekana wahuni tu. Watu makini fuatilieni magazeti ya kesho kama hamtaiona habari hiyo kwenye kurasa za mbele. MUNGI UMENITOLEA MATUSI KUTUKANA MATUSI MPAKA YA WAZAZI...... KWA BUSARA NAKUSAMEHE, NAJUA IPO SIKU MUNGU ATAKULIPA.
 
['-\
'
Acha kupima upepo! Nikisema muniyo munyokwe utaanza kulalamika. Tumeshaukataa huu upumbavu wa kupost taarifa zisizo na source!

Chu Wamukhafia ndende mbuyane, nimesikia ITV kwenye taarifa ya habari msemaji wa familia akisema kuwa mh afya yake ni njema kabisa
 
kweli Pasco,sasa hivi makapi yamekuwa mengi! Lkn pia naona itakuwa ngumu kidogo maana JF sasa imefahamika zaidi na yanaingia makundi ya aina mbali mbali! Halisi asante kwa taarifa Mungu azidi kumrejesha Mwakyembe

The problem ni kwamba, siku hizi hata simu za Mchina, unapata internet.....Tigo nao na vifurushi vyao vya sh.450/= wamefanya wawe wanazoazoa makapi huko mitaani na kuja kuya-dump humu JF!!!
 
Pengine tunaweza kumshukuru Mungu, Mbunge wa Kyela Dr. Harrison Mwakyembe anaweza kutinga ofisini Jumatatu kupiga Mzigo. Mwakyembe sasa umepona njoo toa nusu ripoti ya Richmond iliyobaki, tumechoshwa na tambo za mafisadi.
Mwakyembe ni MNAFIKI MKUBWA, HANA TIJA KWA TAIFA LETU.
 
Wana JF, Nimepost hiyo thread kwa nia nzuri, Chanzo cha habari ninacho, kama mtu alikuwa anahitaji angeweza kuomba nikarudi kuleta taarifa zaidi. Ila KWA MATUSI MAZITO ALIYONITUKANA MWANA JF MWENZANGU MUNGI....... Ninafikiri zaidi uamuzi wangu wa kuendelea kutumia JF, Maana itakuwa haijengi watanzania badala yake wote tunaonekana wahuni tu. Watu makini fuatilieni magazeti ya kesho kama hamtaiona habari hiyo kwenye kurasa za mbele. MUNGI UMENITOLEA MATUSI KUTUKANA MATUSI MPAKA YA WAZAZI...... KWA BUSARA NAKUSAMEHE, NAJUA IPO SIKU MUNGU ATAKULIPA.

hakuna matusi acha kulalama wewe! Siku zingine tumia akili unapotoa taarifa, siyo unakimbilia kupost habari zisizo na source. Mimi huwa mstaarabu sana, lakini siyo mnyonge kusema. Narudia tena kuwa hii ni Jf, lazima upost taarifa zako kama Great Thinker, Jf siyo facebook kuwa makini IFAGHAA. Sorry for inconvenience caused! Kuna thread asubuhi iliyomhusu Mwakyembe ilisababisha kidogo nitupe simu kwenye mtaro, nikadhani na wewe ni wale wale!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom