Afya ya Mwakyembe yazidi kuimarika endeleeni kumwombea!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
SERIKALI imesema hali ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, inaendelea vizuri na bado yupo nchini India akiendelea na matibabu.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari juu ya hali ya Waziri huyo.

“Kila siku huwa naongea naye kwa njia ya simu na amenihakikishia mwenyewe kuwa anaendelea vizuri na matibabu yake na kwamba hali yake ni nzuri,” alisema Nyoni.

Hata hivyo, aligoma kuzungumzia nini hasa kinamsumbua Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela na kueleza kuwa hairuhusiwi kimaadili kuweka hadharani ugonjwa wa mtu kwani ni siri yake na familia yake.

Pamoja na hayo, Dk. Mwakyembe anadaiwa kusumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaomsababishia uvimbe katika baadhi ya maeneo mwilini mwake na kitaalamu ugonjwa huo unajulikana kama Exfoliative Dermatitis.

Ugonjwa huo unadaiwa kuathiri wanaume na wanawake wenye umri kuanzia miaka 55 na dalili zake ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu na sehemu ya juu ya ngozi kupukutika.

Dk. Mwakyembe aliondoka takribani wiki moja iliyopita kwenda Hospitali ya Apollo iliyopo Chenai nchini India kwa ajili ya matibabu kufuatia hali yake kuzidi kuwa tete.
 
jamaa ana siri kubwa tunamuhitaji katika muda huu tunaelekea kwenye uchaguzi wa muhimu wa 2015 ambao utaweka mustakabali mpya wa nchi hii
 
Huyu bwana mkubwa ni muhimu katika nyanja zote ya taifa letu kwa 98% Na tunamshukuru mwenyeenzi MUNGU ampe maisha marefu na yenye fanaka nyingi. Na hata kama ni Gamba bado tu anahitajika popote pale Tanzania<<<<<<<<<<<<<<,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ndiyo tabia ya Pollonium hiyo, inakuacha upate nafuu then inakuchukua kwa nguvu. Hapati nafuu ila anachelewesha siku ya kuondoka tu.
 
Ndiyo tabia ya Pollonium hiyo, inakuacha upate nafuu then inakuchukua kwa nguvu. Hapati nafuu ila anachelewesha siku ya kuondoka tu.

Kila mtu duniani lazima ataondoka, na cha kushangaza wanaojiona wazima wanaweza kuondoka kabla ya tunaowaona wagonjwa. Yuko bwana alikuwa anaimba wimbo unaosema mzima kuwa mfu, na mgonjwa kuwa salama katika kipindi cha salaam kwa wagonjwa miaka fulani. It is all in the hands of God; we pray for the total healing of Mwakyembe and above it all we pray and fight for the healing of Tanzania because the country is seriously sick.
 
Kama Mungu hajakupangia kufa hata ukiwekewa Pollonium hufi bali mwili utakuwa kama umechakaa vile, Bwana asifiwe milele!
 
get well soon flowers.jpg

Get well soon Mkuu.
 
Back
Top Bottom