Mwakyembe apuuza data za JamiiForums!

Mwakyembe apuuza data za JamiiForums!

Status
Not open for further replies.
Hajui atendalo, angejua kuwa kupona kwake kuna mkono wa JF angeishukuru na kuichangia mara dufu!

Jf ndio inayofichua maovu ya nchi hii na ndio kisima cha hekima kwa wanasia machipuko, na zaidi jf ndio iliyofichua njama za jaribio la yeye kuuawa na kila aina ya hila dhidi yake lakini leo anaiona si chochote?

Aje ajiunge huko tumpige msasa huyo!

JF ndo ilikuwa inamtibu?
 
sishangai chochote, ni kawaida ya wana ccm kukejeli chochote kinapokuwa na ukweli mbaya kuhusu wao na serikali yao. refer list of shame ya mwembeyanga, walikana na kuikashifu cdm mpaka povu likawatoka midomoni, lakini muda mchache baadae serikali ilivunjika kwa hilo hilo na leo wanaona aibu.
 
sasa na ninyi wana jf mmeamini kuwa ni kweli hakukuwa na mpango huo?
 
mwakyembe inampasa kujivua Gamba nakuwa mkweli..He is smart lakini u system wa si-si-em unamwaribia sifa..
 
Katika hatua za mwisho za kupitisha bajeti ya Miundombinu, Wenje alisimama na kusema kuwa ana taarifa za kuwepo vikao vya kuipa kampuni fulani bandari(sijaimaki vizuri) ikiwa ni namna ya kulipa deni la ATCL ambalo ni kubwa mno.
Mwakyembe amejibu kuwa kama kuna mtu anafanya hiyo mipango bila kumjuza yeye aendelee.
Lakini katika hali isiyo ya kawaida akamwambia Wenje, kuwa ana wasiwasi na taarifa zake, na akamalizia..."Ndiyo shida ya kutegemea habari za JamiiForums hiyo!
Mwakyembe Anaichkuliaje Jf huyu?

Jamani,
tusipotoshe hili, usichukue tafsiri yako, weka neno kwa neno kama ni nukuu kwani wewe umeacha neno SANA katika hiyo kauli ya Mwakyembe, and thats where the difference kicks in. Mwakyembe ametamka kwamba: "Hiyo ndiyo shida ya kutegemea SANA Jamiiforums."
 
Wakati nakubali kuwa taarifa zingine humu huwa ni za kutengeneza (jambo ambalo lazima litegemewe ktk forum kama hii), nadhani ku-underrate mchango wa jf kama whistle-blowing forum ni kufanya cheap generalization. Asipuuze Jf, huenda hata yeye imemfaa bila kujua. Mimi ningekuwa kiongozi, Jf ningekuwa siikosi kila siku.
 
"msg sent" ni wazi kuwa yeye ndo anafatilia sana JF au mawaziri wote, maana cjaona kama Wenje ametamka jf dataz, bali yeye, kudos to JF.
 
Mojawapo wa watu wenye dharau na majigambo Tanzania hii ni Mwakyembe. Ni mchapakazi lakini anatakiwa kujirekebisha katika hili. Apunguze dharau kwa watu.

Nakumbuka kuna kipindi aliitisha mkutano na waandisi wa habari kabla hajawa waziri, lol, baadhi yao walimkoma jinsi alivyokuwa anawadhihaki kuwa hawajaenda shule ndo maana hawajuwi chochote.

Mwisho wa siku hatuangalii dharau/majigambo, tuaangalia uchapakazi na uadilifu, jamaa anapiga mzigo!
 
Ni mara ngapi?na ni data zipi ziliwekwa jamii forum ni za uongo??

Mara kibao tu! JF mtu yoyote anaweza kupost data na hakuna verification kabla ya thread kufunguliwa. Kumbuka kuna members zaidi ya 10,000 humu, si kila member hutoa data za kweli.

Ni wewe mwenyewe msomaji watakiwa kupima uhalisia wa data.
 
Mwakyembe apuuza data za Jamiiforums...kasema kweli kuna data zingine ni za uwongo kama data ya CT SCAN moja sawa sawa na shangingi moja au mfuko wa Saruji kuuzwa Sh5000. Kuna data zingine ni za kweli ndio maana mods data zingine wanazipigia mistari.
 
Angejua jins gani wana JF walikuwa wanamuombea kipindi cha ugonjwa
wake leo hii amepona leo anatudharau?Kweli madaraka yanalevya.
 
Mojawapo wa watu wenye dharau na majigambo Tanzania hii ni Mwakyembe. Ni mchapakazi lakini anatakiwa kujirekebisha katika hili. Apunguze dharau kwa watu.

Nakumbuka kuna kipindi aliitisha mkutano na waandisi wa habari kabla hajawa waziri, lol, baadhi yao walimkoma jinsi alivyokuwa anawadhihaki kuwa hawajaenda shule ndo maana hawajuwi chochote.

amesema ukweli kwan humu sio taarifa zote zina uthibitisho hvyp kuziamini moja kwa moja inakuwa ngumu
 
Mwakyembe apuuza data za Jamiiforums...kasema kweli kuna data zingine ni za uwongo kama data ya CT SCAN moja sawa sawa na shangingi moja au mfuko wa Saruji kuuzwa Sh5000. Kuna data zingine kweli.
Kaka,

Uko serious? Hizo data ni za JamiiForums?
 
Akimjibu Mh. Wenje kuhusu uwepo wa mpango wa kuwapatia wageni bandari ya Mtwara kw fidia ya deni la serikali Waziri Mwakembe alikanusha kata kata kuwepo kwa mpango huo na akaongeza kuwa "Taarifa kama hizi ndiyo matokeao ya kufuatilia habari za Jamii Forum".

Wana jamii tunakubaliana na hilo kwamba hapa JF ni mahali pa kupika taarifa za uwongo wakazitumia wabunge?
Kwanza sijakuelewa maana habari nyingi hapa jamii forum hazianzii hapa ila panakuwa na source ambayo inaanzisha then wanajamvi wanaingia chimbo kusaka za chini ya kapeti kuhusiana na ishu iliopo mbele na mara nyingi huwa si zote nyingi wnajamvi wanazikopi na kupest especially zile za kiutendaji na kiwizi kama kukodi ndege!Na katika swali hili la wenje na jibu la mwakyembe ninaamini hata CAG hutegemea JF ktk ripoti zake maana alichouliza wenje kipo kwenye ripoti za Utouh.Sijui kasahau huyu poti wangu?
 
Akimjibu Mh. Wenje kuhusu uwepo wa mpango wa kuwapatia wageni bandari ya Mtwara kw fidia ya deni la serikali Waziri Mwakembe alikanusha kata kata kuwepo kwa mpango huo na akaongeza kuwa "Taarifa kama hizi ndiyo matokeao ya kufuatilia habari za Jamii Forum".

Wana jamii tunakubaliana na hilo kwamba hapa JF ni mahali pa kupika taarifa za uwongo wakazitumia wabunge?

nashindwa kukubaliana na Mwakyembe moja kwa moja ila naukubali ukweli kwamba hapa jamvini pameibuka wapuuzi ambao wanaleta sio tu thread za kijinga bali zinakuwa ni za uongo kabisa. Hii inasababisha jukwaa kudharauliwa na kutoaminika kwa kiasi flani. Ndio maana wakongwe wamekuwa wachunguliaji tu siku hizi.
 
Kutokana na kauli ya Dr.Mwakyembe, mimi nina mitizamo ifuatayo;
1. Nimefurahi kusikia kuwa hadi viongozi wakuu wa serikali wanafuatilia JF so tuendelee kuhabarika kutumia JF
2. Ni kweli humu ndani huwa kuna thread za kizushi- we kama unabisha bisha tu!
3. Kwa kauli ya Dr.Mwakyembe, Waziri / Kiongozi wa serikali kutoa kauli hiyo Bungeni ambako kumbukumbu zimebaki kwenye Hansard kwa uthibitisho/ushahidi (kutamka wazi kuwa habari zake zina mushkeri) basi niwatoe hofu wale waoga wamwage data zote za uongo na ukweli Live bila kuogopa tena maana hawatafanywa lolote wala kushtakiwa maana JF haitatumika kama ushahidi maana taarifa zake ni za Uongo....
4. Dr Mwakyembe sio Muoga ndo maana kadiriki kusema ukweli ili liwalo na liwe kwa yeyote humu ndani aidha ni fan wake au lah!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom