Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Pascal Mayalla

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
35,689
2,000
Wanabodi,

Naomba kuanza na Angalizo: Mamlaka pekee za kutangaza status report ya ugonjwa wa Corona kwa Tanzania ni
 1. Rais wa JMT
 2. Waziri Mkuu
 3. Waziri wa Afya
 4. Msemaji Mkuu wa Serikali
Hivi wajameni hii siyo taarifa ya status ya ugonjwa wa Corona na wala sio update ya Corona, hili ni angalizo la swali nimeuliza na alama kabisa ya kuuliza! Mimi mwenzenu kazi yangu ni kuuliza tuu maswali, na kuna swali niliwahi kuuliza, hadi nikaitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge, kuwa nimetoa statement, kumbe sikutoa statement yoyote bali nimeulizwa swali tu, hivyo bandiko hili nalo ni swali tu lenye alama ya kuuliza hii? nisije nikaitwa popote kuulizwa kuwa nimetoa statement yoyote, unless kwenye janga hili la Corona, hata sisi waandishi haturuhusiwi kuuliza chochote, hata ukisikia chochote kinachohatarisha usalama wa taifa letu tunyamaze tuu tukisubiria hadi hao wasemaji 4 waseme, wasiposema, tupotezee huku tunateketea?.

Kufuatia janga la Corona, tunahimizwa tusitangaze taarifa yoyote bila kuipokea kutoka Vyanzo rasmi vya kiserikali.

Lakini inapotokea wewe ni mwandishi wa habari makini na Mzalendo unao jua wajibu wako kama mwanahabari na wajibu wako kwa taifa lako, ukipokea habari kutoka chanzo ambacho wewe unakiamini, na ukathibitishiwa kuwa serikali inajua ila imenyamaza, kwa vile kunyamaza huko kunaweza kutusababishia majanga, hiyo kuitangaza taarifa hiyo ili serikali ichukuwe hatua stahiki ndio uzalendo wa kweli kwa taifa lako.

Mimi licha ya kuwa ni mwana habari, pia nimebahatika kufuta tongo tongo za sheria, hivyo, ili ku tie in all loose ends kunizuia nisiitwe popote kuwajibishwa kisheria, naitoa taarifa bila kutaja majina yoyote, sijasema ni Waziri gani, au waziri wa wapi, hii ili kuisaidia serikali yetu ya JMT, kutimiza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania dhidi ya maambukizi ya Corona huku nikiheshimu haki zote za the right to privacy za wagonjwa na za watu, na ningeomba hata miongoni mwa wachangiaji ikitolea ukawa unamjua, ili kuheshimu haki za mgonjwa, nawaomba msimtaje kwa majina.

Nimepokea taarifa hii kutoka very reliable source.

... jina limehifadhiwa (Waziri wa ...) ashukiwa kuugua CORONA.
************************************************************************
Waziri wa... ambaye alikuwa safarini akitua nchini kutokea London (Uingereza 🇬🇧) ambapo safari yake ilianzia Italy 🇮🇹 kisha kurejea wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya ... akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA.

Dr. Mkuu wa Hospitali ya ... baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya ... akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Corona, itakuwa ni aibu kwake na kumdhalilisha!.

Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika... Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠

Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda , kituo Maalum cha wagonjws wa Corona, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya Italy kisha kupitia London kurejea Tanzania na homa kali!

Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya hiyo alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake.

Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali hiyo pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine.

Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Watanzaia wote!... Ameitaka serikali kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya hiyo haraka kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari!
Mwisho.
My Take.
Kwa vile Corona ni issue za kitabibu, sio lazima kila anayeugua mafua makali ni Corona, inawezeka Waziri ana homa tuu ya kawaida na mafua ya kawaida lakini sio Corona, kama madaktari wanasema sio Corona then sio Corona!.
Lakini kama ni Corona,
Natoa Wito, Only The Truth & Transparency ndio The Only Way Out Kushinda Vita Hii. Kama Waziri amepimwa na ikathibitishwa ni anaugua Corona, then his/her rights to privacy ziheshimiwe kwa kuwa upheld kwa kutokutajwa kwa jina wala wizara yake, ila asipewe any preferential treamement kwasababu yeye ni Waziri, kama mtu ameugua Corona, haijalishi yeye ni nani, msifiche waziri wetu kuugua Corona, ugonjwa wa Corona ni ugonjwa tuu hauchagui wa kumpata na sio ugonjwa wa aibu kusema tuufanye siri, unaficha nini?!. Marais wa dunia wame test positive na wametangaza, mawaziri wakuu wa dunia hadi mwana mfalme ametangaza ndio itakuwa waziri?.

Kama ni kweli kuna Waziri anaugua Corona halafu tunaficha kwasababu yeye ni Waziri, naomba kutoa angalizo la kisa cha mficha maradhi kisije..., nini huwa kinatokea ambacho Kitamuumbua. Naomba Tanzania tusifike huko!

NB. Naombeni tusianze kupiga ramli chonganishi kwa kuanza kumhisi na watu humu kutaka kumjua ni waziri gani, " umdhanie ndiye, siye!". Inawezekana ikawa ni jamaa mmoja tuu jina lake Waziri!

I wish you Saturday night njema.

Paskali
Update
Wanabodi, hii sasa sio tetesi tena, leo imethibitishwa rasmi Bungeni Dodoma, kuwa ni kweli kuna Waziri aliugua Corona na akagoma kwenda kutibiwa kwenye hospitali maalum iliyotengwa na badala yake akalazimisha kutibiwa hospital ya kawaida.

Serikali ilipopata taarifa ilituma watu wake na Waziri huyo alihamishwa kikuku na kuhamishiwa eneo rasmi lililotengwa, sasa anatibiwa huko na anaendelea vizuri.

Uthibitisho huu umetolewa leo Bungeni Dodoma na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakati akihitimisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake, katika hotuba iliyotangazwa live, mubashara kupitia TBC.

Waziri Mkuu amevishukuru sana vyombo vya habari kwa kutangaza habari kama hizi, ambazo zimeisaidia serikali kujua na kuchukua hatua.

JF ndicho chombo pekee rasmi cha habari kwa hapa nchini kuitangaza habari hii hivyo kuiwezesha serikali kuchukua hatua stahiki.

Nami niliyewaletea taarifa hii, naomba kumshukuru sana kwa dhati yule mshirika wangu muhabarishaji kutoka Zanzibar ambaye ni binti mrembo wa Kizanzibari anayejiheshimu na mimi namheshimu sana, Asante sana mwananahabari binti mwanamke shujaa wa Kizanzibari.

Kwa heshima ya mhe. Waziri na kwa kuzingatia maadili ya kidakitari ya kitu kinachoitwa " the confidentiality clause" cha kuficha siri ya mgonjwa kati ya dakitari na mgonjwa, na kwa kutumia kipengele cha " the right to privacy" kwa sisi waandishi kutuingilia faragha za watu, Waziri Mkuu hakulitaja jina la Waziri huyo, na mimi hapa naomba nisilitaje jina la Waziri huyo na kukuomba hata wewe, hata kama unalijua jina la Waziri huyu, tusilitaje.

Information is power, hongera kwa wewe mwana jf to be the first to know, na ukiwa na taarifa yoyote kama hii ambayo italisaidia taifa, usisite kuileta humu jf.
Nawatakia siku njema.

Paskali
Rejea za Mandiko ya The Same Author Kuhusu Janga la Corona
 1. Mtu kama huyu ni binadamu au shetani? Anaombeaje Corona ifike Tanzania. Kuiombea nchi yako majanga, sio zaidi ya uendawazimu? Huu sio ushetani? - JamiiForums
 2. Corona: Japo ni janga, pia ni fursa. Tanzania bado hakuna maambukizi, tupunguze panic, tuongeze Elimu. WB kumwaga mihela, tuchangamkie fursa - JamiiForums
 3. Corona inatufundisha Tanzania tuna tatizo kuchanganya siasa na professionalism. Hongera Prof. Janabi kwa elimu uliyotoa, so far you are the best! - JamiiForums
 4. RC Makonda, Dar ni jiji la wote, vyama vyote. Mbowe sio mwanasiasa uchwara aliyefilisika, Zitto sio mshirikina. Tunakupenda, heshimu wote uheshimiwe - JamiiForums
 5. Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out! - JamiiForums
 6. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums
 7. Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani!. Je Magufuli ni nabii? Tanzania wanambeza, Afrika wanamlilia! Tanzania yapigiwa mfano Magufuli awe Rais wa Afrika - JamiiForums
 8. Vita Janga la Corona: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas, Naibu Waziri wa Afya, Dr. Faustine Ndungulile, kesho watakuwa live JLNH-Star TV - JamiiForums
 9. Star TV: Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas na Naibu Wazuri wa Afya Dr. Faustine Ndungulile, Wanazungumzia Corona - JamiiForums
 10. Mungu ni Omnipresent. Kufuatia Local Transmission ya Corona. Je, Sasa Tushinikize Watu Wasalie Majumbani Mwao, ila Sadaka Ndio Itumwe Kwa M-Pesa? - JamiiForums
 11. Nabii Malisa: Mungu ameniambia Corona ni April tu, May hakuna Corona na hakuna atakayekufa!. - JamiiForums
 12. Kwa Kasi Sasa, Jee Tuendelee Ushujaa wa Ka-Corona, Tusitishane, Tuchape Kazi Tukiteketea, Au Sasa Tubadili Msimamo Tusitisishe Mikusanyiko Tuokoke? - JamiiForums
 13. TBC - Mjadala wa Role of The Media kwenye mapambano ya Corona, Je, Media Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
 14. Live on Star TV: Corona Kushika Kasi Ndio Habari Kubwa Tanzania, Jee Media ya Tanzania, Inatimiza Wajibu Wake Ipasavyo? - JamiiForums
 15. Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza! - JamiiForums
 
Keynez

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,690
2,000
Hivi Kabudi yuko wapi? Angekuwa mstari wa mbele katika mapmbano haya. Na juzi nimemuona Balozi Kairuki akitoa taarifa ambayo kimsingi ilitakiwa itolewe na Wachina wenyewe au na Waziri wetu wa Mambo ya Nje.
 
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
7,863
2,000
Nna jaribu tu kuwaza kama ni kweli ,je atakuwa amesha waambukiza Watu wangapi kwa ukaidi wak ?.Kutii Sheria kwa Afrika hii ni kwa Wanyonge tu lakini kwa wakubwa mmh hapana.

Hili Tatizo mna lifungia Macho ,ipo Siku litabisha Hodi Miguuni kwenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom