Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
SerikaliI imekataa kutoa taarifa ya ripoti iliyopewa na madaktari bingwa wa Hospitali ya Apolo, India ambao walimtibu Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana na ripoti hiyo, alisema kuwa suala hilo haliwahusu na kama wameipokea hawezi kuzungumzia suala hilo.
Alisema Dk. Mwakyembe ndiye anaweza kuzungumzia na hajui kama imepokelewa au la.
Hata kama tumeipokea sina ruhusu ya kuzungumza na kama hiyo ripoti yake mfuate mwenyewe Dk. Mwakyembe akueleze
kwani sisi hatuwezi kutaja ugonjwa uliokuwa unamkabili, alisema Nyoni.
Akizungumzia hali ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami. ambaye alikuwa India kwa matibu, alisema kuwa hali yake inaendelea vizuri, lakini alisema hana taarifa za kurejea kwake.
Hivi karibuni, Dk. Mwakyembe alisema hospitali ya Apollo alikokuwa amelazwa alikuwa, imetuma ripoti kwa serikaali ya Tanzania kueleza walichobaini baada ya kumfanyia uchunguzi.
CHANZO: NIPASHE