Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

Na Mwandishi wetu

HALI ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, inasikitisha kwani licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake siyo ya kuridhisha.

Watu wa karibu na Dk. Mwakyembe waliopata fursa ya kumwona, waliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa afya ya waziri huyo maarufu nchini bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.

Mbali ya hali hiyo, Dk. Mwakyembe hulazimika kuvaa gloves mikononi na miguuni, fuluna au mashati marefu pamoja na traksuti au suruali ili kufunika mikono na miguu yake ambayo licha ya tiba anayoendelea kuipata, ngozi yake ina hali mbaya kutokana na kuathirika na ugonjwa wa ajabu uliompata.


Kwa mujibu wa habari hizo, kucha za vidoleni na miguuni zimeoza na zina rangi nyeusi, miguu na mikono yake imepasuka mithili ya mtu mwenye magaga ambayo wakati mwingine hutoa damu na kumsababishia maumivu makali.


"Kwa jinsi alivyo, Dk. Mwakyembe hawezi kwenda ofisini leo au kesho. Siha yake ukimwangalia ni nzuri na anaongea kwa sauti kama kawaida, lakini ngozi yake iko vibaya, kichwani hana nywele wala kope, nyusi…

"Anahitaji muda zaidi wa kupumzika na kuendelea na matibabu," alisema mmoja wa watu waliofanya ziara ya kwenda kumwona nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watu wa karibu na waziri huyo walioshuhudia mkanda wa matibabu yake akiwa India, waliliambia gazeti hili kuwa ukiuangalia, utatoa machozi kwani picha zake zinatisha.


Mkanda huo ambao Dk. Mwakyembe hupenda kuwaonyesha watu wanaofika nyumbani kwake Kunduchi Mtongani kumjulia hali, unamwonyesha katika sura na muonekano tofauti kabisa na jinsi alivyo na kama unauangalia leo bila kuambiwa, huwezi kubaini kama ni Waziri Mwakyembe.


"Ukiuangalia mkanda wa matibabu yake, unaweza kutoa machozi, unasikitisha sana. Kwa kifupi Dk. Mwakyembe amepata mateso makubwa yaliyotokana na ugonjwa ambao hadi sasa haujulikani," alisema mtoa habari wetu.


Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.


Taarifa za Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa hivi karibuni, alisema wasiwasi huo unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele aliyoondoka nayo nchini kwenda India.


Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema alipokwenda kumwona Dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga.


Sitta alikaririwa akisema, "Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha."


Hata hivyo, Sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.


Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo.


Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, Dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini.


Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo, India, waliomtibu Dk. Mwakyembe.

Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana na ripoti hiyo, alisema kuwa suala hilo haliwahusu na kama wameipokea hawezi kuzungumzia.


Alisema Dk. Mwakyembe ndiye anaweza kuzungumzia na hajui kama imepokelewa au la.


"Hata kama tumeipokea, sina ruhusu ya kuzungumza, mfuate mwenyewe Dk. Mwakyembe akueleze kwani sisi hatuwezi kutaja ugonjwa uliokuwa unamkabili," alisema Nyoni.


Mwakyembe alipelekwa India Oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana.


Taarifa za awali, zilisema Dk. Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa ambao waliamini naibu waziri huyo alilishwa sumu.

 
fair player ipi uliyoitaka? mbona mnarudia mle mle jamani? au ndio lowasa kawatuma!

Acha ushabiki ndugu yangu. Dr hakusema ukweli kuhusu mmiliki wa Richmond wakati anamjua. Kama una access na Dr kamuulize.

Labda nikusaidie kidogo. Lowassa waka Jakaya sio wamiliki wa Richmond. Sasa nenda akakwambie ukweli.

Acheni kumuota EL kwenye kila kitu. Kwenye Richmond Dr alifanya au amefanya makosa ambayo nina uhakika anayajutia. Zawadi ya uwaziri ni ishara tu ya asante aliyopewa kwa mojawapo ya kosa..

Kosa kuu litakalomtafuna ni kuwadanganya watanzania million 45.
 
Huyu ndio kiongozi Mpendwa anayeipenda nchi yake hakutaka kujilimbikizia Madaka hadi kwenye Kamati kuu ya CCM, halmashauri kuu ya CCM, kazi moja tuu kuonyesha Uwezo wake na wachafu wakamkodolea jicho baya

wabaya hao bado wako madarakani na wanakula meza moja na Rais wetu, wanaiba kama kawaida
 
....Halafu cha kushangaza hadi sasa Serikali haijatia hata neno kama inachunguza ugonjwa huu wa ajabu unaosemekana umetokana na kupewa sumu au la. Kama inachunguza kwanini inaogopa hata kuwafahamisha Wananchi kwamba uchunguzi wa yaliyompata Mwakyembe unaendelea? Kwa nini kumekuwa na kimya kizito toka Serikalini?
 
tulisikia anajua kila kitu kinachoendelea,kama ameamua kukaa kimya kulinda chama chake na kujipendekeza kama ilivyo kawaida yetu ataenda kusemea huo ukweli kaburini
 
Acha ushabiki ndugu yangu. Dr hakusema ukweli kuhusu mmiliki wa Richmond wakati anamjua. Kama una access na Dr kamuulize.

Labda nikusaidie kidogo. Lowassa waka Jakaya sio wamiliki wa Richmond. Sasa nenda akakwambie ukweli.

Acheni kumuota EL kwenye kila kitu. Kwenye Richmond Dr alifanya au amefanya makosa ambayo nina uhakika anayajutia. Zawadi ya uwaziri ni ishara tu ya asante aliyopewa kwa mojawapo ya kosa..

Kosa kuu litakalomtafuna ni kuwadanganya watanzania million 45.
Halafu uongo mkubwa namna hii ukavunja Baraza la Mawaziri.
 
"When the righteous prosper, the city rejoices; when the wicked perish, there are shouts of joy".

When shall wickedness perish in this LAND????
 
Nilisema na nitaendelea kusema kwa sasa nchini kwetu tuna manyang'au yenye sumu kali sana! Uroho wa URAIS unanfanya kiufikia hatua ya kutojali utu wa m-TZ mwenzako!

Na ni CCM ndo ya kulaumiwa kwenye haya yote, wamefanya uraisi kwao ni sawa na mbio za kupokezana kijiti!!! Wanapigana vikumbo hadi aibu. Nilicheka sana kusikia hata Dr. Nchimbi naye anawania urais!!
 
Acha ushabiki ndugu yangu. Dr hakusema ukweli kuhusu mmiliki wa Richmond wakati anamjua. Kama una access na Dr kamuulize.

Labda nikusaidie kidogo. Lowassa waka Jakaya sio wamiliki wa Richmond. Sasa nenda akakwambie ukweli.

Acheni kumuota EL kwenye kila kitu. Kwenye Richmond Dr alifanya au amefanya makosa ambayo nina uhakika anayajutia. Zawadi ya uwaziri ni ishara tu ya asante aliyopewa kwa mojawapo ya kosa..

Kosa kuu litakalomtafuna ni kuwadanganya watanzania million 45.
Dr alikuwa mwenyekiti tu wa kamati teule ya Bunge, na kile kilichowasilishwa na Dr ni taarifa ya Bunge. Kwa nini wewe katika mabandiko yako unapenda kumpakazia Dr? Wewe na EL hamuoni ukweli wa jambo hili? Tunawaambia OLE wenu!
 
Dah..atakua kala nini huyu muntu...!!hadi wahindi wameblow
 
nchimbi atakuwa rais wa nani yule? Labda rais wa chipukizi wa ccm.

Lakini hili swala la mwakembe nafikiri kama yeye hatataka kuuzungumzia ugonjwa wake, serikali haiwezi kuuzungumzia.
Kama anajua ilikuwa foul play, atoke atuambie bila kulinda manyang'au wa chama chake na serikali yake.
 
Aliogopa kusema yote kwenye ripoti ya kamati ya bunge ililyochunguza sakata la richmond ilikuokoa serikali yake ya CCM isidondoke hivyohivyo anaogopa kutoa ripoti ya ugonjwa wake ilikuogopa serikali yake isidondoke tena tusubili tuone maajabu tuliozoea ya kulindana hata kwenye afya za viongozi sembuse sisi walalahoi tutapona.
 
wanyakyusa ninaowajua ni majasiri'huyu mtu anaogopa nini na kifo kinamnyemelea?anaogopa kupoteza uwaziri?
 
Inawezekana uwezo wa mtanzania kutambua mambo ni mdogo ila si kama hawa wanasiasa wanavyotufikria,alienda Mwl.Nyerere kutibiwa nje tukaambiwa anasumbuliwa na nini hata bila kuhoji sana,haijalishi kama tulidanganywa au tuliambiwa ukweli.Juzi kati hapa kapelekwa Zitto na ndani ya muda mfupi watanzania tuliambiwa anasumbuliwa na nini.Sasa,hili la Mwakyembe kuna nini?Kwa nini atibiwe kwa kodi zetu na bado tusipewe taarifa anasumbuliwa na nini?Kwamba ugonwa wa mtu ni siri yake na Dr,realy?mbona hvyo visukari vyenu na pressure mnatamka wenyewe na wala si madaktari wenu wala wizara?Stop fooling us.Dr Mwakyembe popote ulipo,kwanza pole kwa kuugua....it is time now,twambie watanzania unasumbuliwa na nini if at all you feel so and you think we deserve to know it,si lazima sana lakini kama vipi twambie kama hautuhusu na twambie umetumia kodi zetu kiasi gani kukutibu na uzirejeshe and we wont take trouble anymore kujua tatizo lako,watanzania tuna shida nyingi na mambo mengi ila we keep on sparing time kujua u hali gani when you dont even care.....Fed upppppppppp
 
Dr alikuwa mwenyekiti tu wa kamati teule ya Bunge, na kile kilichowasilishwa na Dr ni taarifa ya Bunge. Kwa nini wewe katika mabandiko yako unapenda kumpakazia Dr? Wewe na Bwana wako EL hamuoni ukweli wa jambo hili? Tunawaambia OLE wenu!

Wewe ongea kama umechanganyikiwa ila LAANA ya Watanzania millioni 45 ni kubwa sana! Hata mkimsingizia EL haisaidii. TUBUNI kwa waTanzania.
 
Tanzania hatuna sense of privacy wala dignity kwa wagonjwa, mtu unaenda kumuangalia mgonjwa halafu unakuja kuwaambia waandishi wa habari "jamaa kanyonyoka nywele, kope, ndevu mpaka...." na waandishi wanaandika.

Ndiyo maana wengine wanaona gozigozi, hamna mtu zaidi ya close friends and family kujipendekeza.
 
Inasikitisha sana....
Ila pliz Mzee wangu Dr Mwakyembe!
Dont let them kill you for nothing.... waumbue kabla hawajafanikiwa!
Nasi tutazivaa Tshirts za sura yako na kuta za mitaa tutaipamba kwa michoro ya sura yako kama shujaa wa kweli...
Kukaa kwako kimya kwanza kuna rahisha sana madhara zaidi sababu kifua chako kinaelemewa na mambo mengi zaidi.
Onyesha kujipenda na kutupenda pia kwa kuweka hadharani ukweli wote na kila kitu
 
Wewe ongea kama umechanganyikiwa ila LAANA ya Watanzania millioni 45 ni kubwa sana! Hata mkimsingizia EL haisaidii. TUBUNI kwa waTanzania.
Mara nyingi UONGO hausemwi hadharani tena mbele ya Waheshimiwa miatatu na ushei hivi. Uongo, kama yalivyo MAOVU mengine yote hayafanyiki hadharani.
 
Inasikitisha sana....
Ila pliz Mzee wangu Dr Mwakyembe!
Dont let them kill you for nothing.... waumbue kabla hawajafanikiwa!
Nasi tutazivaa Tshirts za sura yako na kuta za mitaa tutaipamba kwa michoro ya sura yako kama shujaa wa kweli...
Kukaa kwako kimya kwanza kuna rahisha sana madhara zaidi sababu kifua chako kinaelemewa na mambo mengi zaidi.
Onyesha kujipenda na kutupenda pia kwa kuweka hadharani ukweli wote na kila kitu


thubutu yake.........atakufa nayo hiyo siri na hatasema.......kwenye kamati hakuwa peke yake hata hao wajumbe wengine wanajua ...wenye guts za kusema wasema wakione!!.....
 
Back
Top Bottom