Kilasara
JF-Expert Member
- Dec 21, 2008
- 577
- 116
Kama ilivyosemwa hapo awali, ugonjwa wa mtu ni siri yake na daktari wake. Kuhusu jinsi Mhe. Mwakyembe anavyoonekana katika picha, hata kama anaonyesha amezeeka, hatuwezi kutegemea mtu aliyelazwa hospitali kwa muda, na labda akilishwa vyakula asivyozoea, aonekane na sura yake ya kiafya, mara anapotoka hospitali.
WanaJF tuendelee kumtakia afya njema huyu mpinga mafisadi; na mimi binafsi nakutakia mapumziko mema, Mheshimiwa, wakati huu wa Siku Kuu ya Krisimasi na Mwaka Mpya; ukijiandaa kwa mapambano na mafisadi.