Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

HALI ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, inasikitisha kwani licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake siyo ya kuridhisha.
Watu wa karibu na Dk. Mwakyembe waliopata fursa ya kumwona, waliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa afya ya waziri huyo maarufu nchini bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.
Mbali ya hali hiyo, Dk. Mwakyembe hulazimika kuvaa gloves mikononi na miguuni, fuluna au mashati marefu pamoja na traksuti au suruali ili kufunika mikono na miguu yake ambayo licha ya tiba anayoendelea kuipata, ngozi yake ina hali mbaya kutokana na kuathirika na ugonjwa wa ajabu uliompata.
Kwa mujibu wa habari hizo, kucha za vidoleni na miguuni zimeoza na zina rangi nyeusi, miguu na mikono yake imepasuka mithili ya mtu mwenye magaga ambayo wakati mwingine hutoa damu na kumsababishia maumivu makali.
“Kwa jinsi alivyo, Dk. Mwakyembe hawezi kwenda ofisini leo au kesho. Siha yake ukimwangalia ni nzuri na anaongea kwa sauti kama kawaida, lakini ngozi yake iko vibaya, kichwani hana nywele wala kope, nyusi…
“Anahitaji muda zaidi wa kupumzika na kuendelea na matibabu,” alisema mmoja wa watu waliofanya ziara ya kwenda kumwona nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watu wa karibu na waziri huyo walioshuhudia mkanda wa matibabu yake akiwa India, waliliambia gazeti hili kuwa ukiuangalia, utatoa machozi kwani picha zake zinatisha.
Mkanda huo ambao Dk. Mwakyembe hupenda kuwaonyesha watu wanaofika nyumbani kwake Kunduchi Mtongani kumjulia hali, unamwonyesha katika sura na muonekano tofauti kabisa na jinsi alivyo na kama unauangalia leo bila kuambiwa, huwezi kubaini kama ni Waziri Mwakyembe.
“Ukiuangalia mkanda wa matibabu yake, unaweza kutoa machozi, unasikitisha sana. Kwa kifupi Dk. Mwakyembe amepata mateso makubwa yaliyotokana na ugonjwa ambao hadi sasa haujulikani,” alisema mtoa habari wetu.
Hata hivyo ingawa taarifa rasmi ya serikali haijatolewa, ripoti ya ugonjwa wa waziri huyo kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo nchini India ambayo hadi sasa imebaki kuwa siri, inadaiwa kueleza chanzo cha ugonjwa wa Dk. Mwakyembe kuwa umetokana na sumu kali aliyowekewa hapa nchini.
Taarifa za Dk. Mwakyembe kuwekewa sumu, mara ya kwanza ziliibuliwa rasmi nchini na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye ni rafiki mkubwa na mshirika wa karibu wa Dk. Mwakyembe katika mapambano dhidi ya ufisadi nchini katika mahojiano na kituo cha televisheni cha ITV katika kipindi chake cha dakika 45 kilichorushwa hivi karibuni, alisema wasiwasi huo unatokana na mabadiliko ya ngozi na nywele aliyoondoka nayo nchini kwenda India.
Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema alipokwenda kumwona Dk. Mwakyembe nyumbani kwake, alipata mshtuko mkubwa kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza katika umri alionao kushuhudia ngozi ya mtu ikitoa unga.
Sitta alikaririwa akisema, “Kuna kitu kama mba kwenye nywele na kwenye ngozi ya Dk. Mwakyembe. Akishika hivi, baadhi ya nywele zinadondoka. Mkono umevimba, sehemu mbalimbali. Mke wake alichukua video. Alikuwa anatuonyesha kwenye laptop (kompyuta ndogo). Kwa kweli inatisha.”
Hata hivyo, Sitta alihojiwa na polisi kuhusiana na taarifa hiyo kwa madai kuwa ingeweza kuhatarisha amani, lakini alipotakiwa kutoa ushahidi anadaiwa kutoa ushahidi wa habari za kwenye mitandao ya kijamii.
Kabla ya Dk. Mwakyembe kwenda India kutibiwa, kulikuwa na uvumi kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi huyo kulishwa sumu, ingawa yeye binafsi hajakanusha wala kuthibitisha habari hizo.
Katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu aliporejea nchini, Dk. Mwakyembe alisema ripoti ya ugonjwa wake iko serikalini.
Hata hivyo, serikali hadi sasa imekataa kuitoa hadharani ripoti hiyo ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Apollo, India, waliomtibu Dk. Mwakyembe.
Habari zaidi zinasema kuwa mwanasiasa huyo amepania kuianika ripoti hiyo hadharani kama serikali itaendelea kuifanya kuwa siri.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, alipoulizwa kuhusiana na ripoti hiyo, alisema kuwa suala hilo haliwahusu na kama wameipokea hawezi kuzungumzia.
Alisema Dk. Mwakyembe ndiye anaweza kuzungumzia na hajui kama imepokelewa au la.
“Hata kama tumeipokea, sina ruhusu ya kuzungumza, mfuate mwenyewe Dk. Mwakyembe akueleze kwani sisi hatuwezi kutaja ugonjwa uliokuwa unamkabili,” alisema Nyoni.
Mwakyembe alipelekwa India Oktoba 9 mwaka jana na kurejea nchini Desemba 11 mwaka jana.
Taarifa za awali, zilisema Dk. Mwakyembe alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Lakini, taarifa hizo za ugonjwa wa kisukari zilipingwa na baadhi ya washirika wake wa karibu kisiasa ambao waliamini naibu waziri huyo alilishwa sumu.
 
Kama kweli ni mpiganaji, si aseme ukweli kuhusu 'sumu' aliyolishwa? Kuendelea kukaa kimya hakuna maana yoyote. Aeleze ni sumu gani na anahisi/anajua ni vipi walimuwekea. Otherwiz, anapoteza maana ya upambanaji.

My take:
Mafisadi waende haraka kumuongezea 'doze' ili apotee haraka pamoja na hiyo 'siri' yake.
 
Kama kweli ni mpiganaji, si aseme ukweli kuhusu 'sumu' aliyolishwa? Kuendelea kukaa kimya hakuna maana yoyote. Aeleze ni sumu gani na anahisi/anajua ni vipi walimuwekea. Otherwiz, anapoteza maana ya upambanaji.

My take:
Mafisadi waende haraka kumuongezea 'doze' ili apotee haraka pamoja na hiyo 'siri' yake.

Sumu ambayo inaambatana na dallili zinazoonekana kwa mwakyembe -ya kunyonyoka nywele na ngozi kuharibka, na kuoza ni Thallium
lakini hata hivyo tusubiri ripoti kwani uchunguzi unaendelea. Kwa maelelzo zaidi soma Wikipedia hapahttp://en.wikipedia.org/wiki/Thallium_poisoning na hapa http://www.medicinenet.com/thallium/article.htm
 
HALI ya afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, inasikitisha kwani licha ya kupata matibabu nchini India na kuendelea na tiba hiyo hapa nchini, hali yake siyo ya kuridhisha.Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima kutoka kwa watu wa karibu wa Dk. Mwakyembe waliopata fursa ya kumwona, afya ya waziri huyo maarufu nchini bado siyo ya kuridhisha kwani amenyonyoka nywele, kope, nyuzi na hata vinyweleo vyote mwilini.Mbali ya hali hiyo, Dk. Mwakyembe hulazimika kuvaa gloves mikononi na miguuni, fuluna au mashati marefu pamoja na traksuti au suruali ili kufunika mikono na miguu yake ambayo licha ya tiba anayoendelea kuipata, ngozi yake ina hali mbaya kutokana na kuathirika na ugonjwa wa ajabu uliompata.


 
Naomba wenye ustadi wa kuandika, muanzishe thread ya kuomba taarifa za madaktari toka India kuhusu afya ya Mwakyembe. Kwani kuna utata mkubwa serikali inasema Tumuulize mgonjwa, na mgonjwa anasema report ipo serikalini. Lakini serikali ndio iliyo mpeleka huko hivyo inapaswa kutupatia hiyo report.
 
Naomba nikuulize, unaamini Dr alisema ukweli kuhusu Richmond bungeni bila kuficha taarifa muhimu kama mmiliki na mhusika mkuu?

Nijibu hilo ili nijue niendelee na mjadala au niachie hapa. Usije ukawa ndo Dr mwenyewe!
Ripoti tayari ni AZIMIO la BUNGE letu tukufu. Kungekuwa na hata chembe ya UONGO kwenye ripoti ile isingefikia hatua hiyo. Alichojitetea Lowasa wako siku ile ni kutohojiwa na kamati ya Mwakyembe. Baadae akatoa "wish" kisha akai-"grant" hiyo "wish" yenyewe! Sijui kama JMK alimpa uwazirimkuu mtu ambaye Lowasa alim-"grant".
 
Ripoti tayari ni AZIMIO la BUNGE letu tukufu. Kungekuwa na hata chembe ya UONGO kwenye ripoti ile isingefikia hatua hiyo. Alichojitetea Lowasa wako siku ile ni kutohojiwa na kamati ya Mwakyembe. Baadae akatoa "wish" kisha akai-"grant" hiyo "wish" yenyewe! Sijui kama JMK alimpa uwazirimkuu mtu ambaye Lowasa alim-"grant".

We are all smart. We have been in this game long enough to know that your game plan wont work.

I rest my case.
 
Ukicheza na mbwa utaingia naye msikitini, na ukicheka na nyani utavuna mabua.Mwakyembe alicheka na mafisadi akauficha umma jinsi JK na rafiki zake RA na EL walivyowafisadi watanzania kupitia mradi wao haramu wa Richmond kwa kuahidiwa uwaziri matokeo yake ndiyo hayo.Kama binadamu sifurahi hali aliyonayo Dr. tena namsikitikia sana ninchojaribu kueleza ni kuwa siku zote ukiamua kuwa mtetezi wa wanyonge hakikisha unakuwa na msimamo thabiti hata kama itakugharimu uhai kuliko kuwaonea haya mafisadi ambao wao itikadi yao ni kujilimbikizia mali kwa gharama yoyote hata kuua mamilioni ya watu, na itikadi yao nyingine ni kuwa hawana adui au rafiki wa kudumu, wao mungu wao ni fedha tu ziwe safi au chafu. POLE SANA MWAKYEMBE.
 
Inasikitisha sana kuona watanzania tumefikia siasa za namna hii ndugu yetu Harrison Mwakyembe kuonekana hivi kwa wale tuliopata kumuona na kumsikia akiwatetea wanyonge hasa masikini wanaoishi kwa mlo mmoja mpambanaji kipenzi cha watu alifanyiwa kitendo cha kumaliza Uhai wake yaani afe Taratibu watanzania wakishuhudia kifo chake nawaomba wapenda amani wote, wapinga Dhuluma mahali popote walipo tuungane kulaani kitendo hiki kiovu mwisho tunamuomba shujaa wetu mwakyembe usikae Kimya toboa siri kwa jinsi unavyo onekana unaishi kwa huruma ya Mwenyezi mungu si kwa tiba uliyopata na unayoendelea kupata (ebu jifanye Daudi Kabaka mtoboa siri mwanamuziki wa zamani toka Nairobi nchini Kenya ambaye akupenda kuficha maovu mpaka wakamuita mtoboa siri) ukingoja na kukaa na siri hiyo mwisho tutasikia wakavyojinadi ulivyo kuwa mchapa kazi Hodari, mpenda watu,msikivu, Je ? sasa kama unazo sifa hizo ukiwa hai kwanini wamekufanyia hivyo unavyoonekana katika picha kwenye magazeti yetu ya tarehe 04/01/2012 watanzania tumeanza kutokwa na machozi wakati bado upo hai !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.Anatory mujwahuzia
 
washindwe na walaaniwe miaka yote wote waliomtendea hili......kama ni kweli na wakae wakijua nao hawataishi milele.
 
nung'unung'u hakumbatiwi otherwise utaishia kuchomwa na miiba yake,mwakyembe alikuwa na opportunity ya kusema ukweli wote akaishia kuficha huku akiishia kuwitishia nyau mafisadi.
Matokeo yake yuko kitandani akivuna mshahara wa unafiki na woga wake kwa mafisadi,nwys pole kwako mwakyembe na ukipona au hata sasa unatakiwa umwage ugali na sisi wananchi tumwage mboga 2015.
 
"Ukiangalia mkanda wa matibabu yake unaweza kutoa machozi, unasikitisha sana, Dk. Mwakyembe amepata mateso makubwa sana yaliyotokana na ugonjwa ambao hadi sasa haujulikani.."
"Hata hivyo taarifa rasmi ya serikali haijatolewa...ingawa wamekabidhiwa ripoti ya ugonjwa kutoka kwa madaktari bingwa wa hospitali maarufu ya Apollo..."
 
Sidhani kama serikali ina haki ya kutoa siri za ugonjwa wa Mwakyembe. Kama kuna jambo nafikiri ni yeye mwenyewe ndiye alipaswa kutupasulia. Mbona wakati wa sakata la Richmond alijitutumua akaongea na waandishi wa habari na kusema kuwa kuna watu wanataka kumuua. Barua aliyoandika ipo humu JF. Sasa kwa nini anashindwa kwenye swala ambalo ni life and death.
 
kwa alichofanyiwa mwakyembe sio tu wanambeya bali ombi langu ni kwa nchi nzima hii haikubaliki nchi lazima iwe na viongozi bora kwa style hii tunalazimishwa kutawaliwa na mafisadi na familia zao hii hapana 2015 watanzania wenzangu tulikatae hilo lichama litatumalizia viongozi bora
 
Sasa anasubiri nini kulipua mabom?au anataka afe kijerumani na tai shingoni?ye wameshamlostisha tayari, kinachotakiwa na yeye awalipue tu,kama noma na iwe noma.

mi kila siku namshauri, atengeneze CD,aipeleke kwa mwanasheria anayemwamini,au benki labda,au taasisi inayofanana na hiyo. Iwe realeased atakapoona ye mwenyewe inafaa..
 
Polonium kutoka magambani, itawamaliza.

Mwakyembe ulisema kuna mambo mengine mliamua kuyaficha ili kuilnda serikali wakati wa sakata la richmond.

Ni bora tu ungesema yote yajulikane.
 
ukicheza na mbwa utaingia naye msikitini, na ukicheka na nyani utavuna mabua.mwakyembe alicheka na mafisadi akauficha umma jinsi jk na rafiki zake ra na el walivyowafisadi watanzania kupitia mradi wao haramu wa richmond kwa kuahidiwa uwaziri matokeo yake ndiyo hayo.kama binadamu sifurahi hali aliyonayo dr. Tena namsikitikia sana ninchojaribu kueleza ni kuwa siku zote ukiamua kuwa mtetezi wa wanyonge hakikisha unakuwa na msimamo thabiti hata kama itakugharimu uhai kuliko kuwaonea haya mafisadi ambao wao itikadi yao ni kujilimbikizia mali kwa gharama yoyote hata kuua mamilioni ya watu, na itikadi yao nyingine ni kuwa hawana adui au rafiki wa kudumu, wao mungu wao ni fedha tu ziwe safi au chafu. Pole sana mwakyembe.

magambani hakuna jema, kwani walio juu yake kisiasa hawana utashi wa kisiasa wa kung'oa ufisadi. Kauli zao ziko midomoni tu, mioyo yao inasherekea raha ya kushirikiana na mafisadi.
Inaeleweka vema kwamaba mafisadi ndio waliowasaidia walio wengi magambani kuukwaa uongozi wa kisiasa kwa tiketi ya magamba. Hawana hasara hata ya kutoa uhai wa mtu aliye kinyume nao.
 
Back
Top Bottom