Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

Mwakyembe anasikitisha! Walaaniwe wanaohusika!

kama Balali. Ana siri nzito. Hajaisema. Mi namshauri ajirekodi na kuipeleka CD taasisi zinazoweza kutunza vitu hivyo na aseme ni wakati gani iwe released kwa uma. Baada ya kifo chake ama wakati atakaoona unafaa kwake yeye na taasisi hiyo.
 
Hivi kwenye hiyo tume alikuwa peke yake mpaka aandamwe yeye tu?? Binafsi cant buy that unless kuna kitu kingine ambacho hakisemwi. Yeye alikuwa Mwenyekiti tu wa hiyo kamati ambayo ilikuwa na wajumbe wengine. Sasa inakuwaje wajumbe wengine hawajui kile anachokijua Mwakyembe?? Labda mseme kuna uchunguzi aliokuwa anafanya bila kuwashirikisha wenzake!!

yeye alikua ni mwenyeketi na mwanasiasa aliyejijenga baada ya kazi ya tume...wengine hawakua na nguvu za DR . Dr mwakyembe alikua kwenye national politics na kua waziri ilimpa nguvu kitaifa na kumbuka uhusiano wake na heavy weights mwandosya na Sitta kwa kifupi alikua tishio kwa kundi la watu fulani na maslahi yao binafsi kuliko wale wanatume wenzake....kumtoa ubunge kama akina shelukindo na seleeli walishindwa, Kyela hawakupaweza sasa 2015 mwakyembe hatakiwi kuwa around..

.tumia akili ndogo wakati mwingine una haja ya kufikiri sana kama unajua siasa hizi ndogo (i hope haupo mfukoni kwa mtu)
 
Ndugu wana jf, heshima kwenu. Siku chache zilizopita tumesikia ujio wa Mwandosya, sasa naomba mwenye updates kuhusu Mwakyembe. Hali yake kwa sasa iko vp? Je, ugonjwa gani unaomsibu na nini chanzo chake? Natanguliza shukrani.
 
jamaa hali yake ni tata sana maana ngozi inatoa vumbi mzee..
 
kwangu mimi jamaa ni mpambanaji namuombea Mungu apone arejee kwenye mapambano..
 
......issue ya Mwakyembe ni tata, tunatakiwa tumsemee mazuri kwa vile anaumwa, vinginevyo waliohusika na yeye, walijipanga, huo ndio ukweli.
 
Tuna haki ya kujua maendeleo ya matibabu na afya ya viongozi wetu, cha ajabu serikali haituambi wanasumbuliwa na nini hapa namaanisha mwakyembe, hata mwandosya ametunyima haki yetu kujua kiini cha kuugua kwake huku akijua kuna maelezo chini ya kapeti yanayohusisha kupewa sumu, anaishia kusema ni siri yake na daktari, hapa kuna walakini, kama vipi mwakyembe aseme nini kinamsibu ama la sivyo huruma yetu inapotea bure!
 
Amekusikia maana yeye pia ni mdau humu jamvini. Subiri akirudi atakujibu.
 
Ndugu wana jf, heshima kwenu. Siku chache zilizopita tumesikia ujio wa Mwandosya, sasa naomba mwenye updates kuhusu Mwakyembe. Hali yake kwa sasa iko vp? Je, ugonjwa gani unaomsibu na nini chanzo chake? Natanguliza shukrani.

anaendelea vizuri sana katoka hospitali yupo hoteli kwa uangalizi zaidi na karibuni atarudi na akirudi anaziujuli ubunge na uwaziri! anarudi kwenye fani yake ya kufundisha na uwakili na huko huko ataendelea kuwasema mpaka kieleweke
 
anaendelea vizuri sana katoka hospitali yupo hoteli kwa uangalizi zaidi na karibuni atarudi na akirudi anaziujuli ubunge na uwaziri! anarudi kwenye fani yake ya kufundisha na uwakili na huko huko ataendelea kuwasema mpaka kieleweke

sijakuelewa vizuri tupe japo source ya haya maelezo
''Naona tumumbee Mungu amponye kalivyowaponya ZITTO na MWANDOSYA tuache majungu
''
 
Dr Mwakyembe Pole sana mzee. Mungu akukumbuke akuponyeshe urudi kazini, wapenda haki wa nchi hii tunakumiss sana. Mungu asikie maombi yetu ya kutaka wewe upone Docta.
 
I am sorry siko interested kujua siri alizonazo, nimetafakari na kugundua kwamba kama alikua na siri kweli angeshzitaja, labda ni another politico-toffees
 
Ama ye mwenyewe afunguke huko aliko! Kama alivyofanya Zitto. Zitto alilalama humu ndani akiwa India! Hadi watu wakambembeleza na kumkumbusha kuwa ametoka kufanya upasuaji wa kichwa hivyo atulie na aendelee na mapumziko.
 
......issue ya Mwakyembe ni tata, tunatakiwa tumsemee mazuri kwa vile anaumwa, vinginevyo waliohusika na yeye, walijipanga, huo ndio ukweli.
Ni kweli kabisa tunatakiwa tumsemee mazuri hasa wakati huu anapougua lakini mimi watu wanafiki huwa siwasemei mazuri aslani, mtu anawajua waliohusika lakini akirudi utamsikia anawasifia kama Mwandosya anavyofanya, kama mtu ameamua kufa na tai shingoni mwacheni mwenyewe na Mungu wake.
 
Kweli inauma sana, ila kama kuna wanafamilia wa Mwakyembe anasoma hii comment naomba muwe mnasoma zaburi 35 kila siku mpaka atakapopona, zaburi ya 46, na 109, hii ni kwa ajili ya mgonjwa na pia ni njia nzuri ya kuwashughulikia maadui zenu.

Ingekuwa vizuri kama mke wake angekuwa anasoma. Mgonjwa mwenyewe awe anasema haya maneno kila siku Maombolezo 3:22-23, Yakobo 5:15-16, Zaburi 20 yote.

Awe na moyo wa kusamehe yote, hakika Mungu atauokoa uhai wake na kaburi. Maana imeandikwa katika Marko 16:18b hata wakinywa kitu cha kufisha hakitawadhuru kabisa.

I hope anybody who is closer to this family will take this very seriouse. Hulituma neno lake lipate kutuponya na kututoa katika maangamizi. I will keep praying for him
Si muumini wa hicho kitabu, lakini kusoma kwa dhati ya moyo na Mungu alietajwa humo ndani ya kitabu basi inategemea na usafi wa mtu alietendewa hayo! sasa inategemea na Ndugu Mwakyembe ni msafi kiasi gani ili Mungu nae amsikie, ispokuwa ninachojua, Mungu ni mlipaji, yeyote alofanya hivi basi kama hili halikumkuta yeye basi ni wazi vizazi vyake vitalipizwa, hakika wajue wote walofanya hivi wamejitengenezea dhimma kwa Mungu alie juu na ipo siku atalipiza japo wale walotenda watasahau, kwenye Quraan Mwenye Ez Mungu Sub-hana wa Taala anasema kuwa "MWENYE EZ MUNGU HATOBADILISHA KAULI YAKE MPAKA MBADILISHE YALE MLOTANGULIZA KUYAFANYA KWA MIKONO YENU" sasa hata yasipowakuta wao basi jua wazi waoto wao yatawafika tu....
 
nimetumaini yangu kuwa mwakyembe karudi nchini na ameweza kuongea na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu yaliyo msibu,japo hakuweza kuweka bayana hilo lakini macho,masikio ni kwa watanzania kutaka kujua ukweli juu ya nini hasa,hivyo basi naamini kuwa jamii forums pekee ndo inaweza kuwahabarisha watanzania juu ya nini hasa dr mwakyembe kilimpeleka india na ambacho selikari haitaki kuwaambia watanzani!
 
imeniuma kuona sura yake imekuwa yakizee mpaka nashindwa hata kuitazama raia wabaya sana. Nitarudi baadae kidogo
 
Back
Top Bottom