Mwakyembe aigeuka rasmi bodi Bandari, kuivunja

Mwakyembe aigeuka rasmi bodi Bandari, kuivunja

Wewe Tina utakuwa na matatizo ya akili, ni bora ustaafu tu sasa ulee wajukuu na kuchangia kwa uhuru humu JF badala ya kutumia muda wa bosi wako kuposti utumbo humu kila siku. Hebu badilisha hizi topic zako za TPA kila uchao vinginevyo jisajili kwa verified user kama kweli ni mtetea watanzania. Maana mtetezi hana sifa za kujifichaficha kama wewe. Bravo Mwakyembe, asiyetaka kuishi kwa mshahara ageuke Punda mkutane JKNIA
 
Last edited by a moderator:
Wewe ndiye umenasa!! Na umenasa patamu kweli!! Hahahaaa!!! Endelea!! Kweli mimi nimenufaika sana tokea kwenye ile kamati yetu ya uchunguzi, tulikua tunalipwa 630,000 kwa siku kwa muda siku 90 na Mwenyekiti alilipwa 900,000 kwa siku na waliolipa walikua Bandari... Kwa maelekezo ya Waziri!! Na tulikua wajumbe sita na katibu,, na bado hata tulikua tunaishi Dar tulikua na chumba Southernsun USD 200 kwa siku hahahaa!! Na juzi tumelamba posho ya siku sita!!!(Angalao ingekua 3) kwa kikao cha Alhamis na Ijumaa tu!! Na sasa tumeahidiwa mambo kibao, alimradi tunamtetea Kipande!! Ndio maana nilimuonea huruma alipoanguka!! Duh! Hahahaaa!! Patamu hapa!

Mkuu, mimi sijanasa na wala siwezi kunasa kwa sababu sijaleta hoja za kinafiki na kizandiki au kujibu hoja kwa kinafiki au kizandiki.

Ninajibu hoja kulingana na maelezo yako unayoleta mezani ikiwa pia na yale ambayo yamejificha ndani ya hayo maelezo(between a line).

Polisi au vyombo vya usalama huwa mara nyingine vinatumia mabavu na nguvu kupata ushahidi au vielelezo zaidi kutoka kwa watuhumiwa lakini kwako imekuwa ni tofauti kwa sababu umenasa na unadhani kufunguka zaidi ndiyo kuta adjust or alter opinion na mitazamo ya wanaJF wengi kuhusiana na utendaji wa Dr. Mwakyembe ili upate back up to substantiate and validate your relentless and negative crusade.

Kitu ninachokiona hapa ni vindication, at the sametime, it just reinforces a well documented case kuwa bandari ilikuwa kama mzoga ambapo kwa sasa mainzi na fisi wanapambana kuhakikisha hawaondoki kwa urahisi.

Wajinga ndio waliwao, hamjui nchi inavyoendeshwa! Hamjui wezi wa EPA walikamatwa vp hata mtuhumiwa mmoja alisema,"wewe utanihoji vipi wakati tulichukua wote pesa BoT?" Mchezo ukawa umeisha maana alikua ameshakiri kosa akaambiwa! "Ehee, mlikua ne!!eeeh! Mlichukuaje? Ngap? Kwa hiyo alikuwapo?" My God alipogundua kizimbani!! Na nyie haya sasa subirini museme tu mnafiki??,,, Nyerere amekufa lakini wapo watakaofanya kazi hadi wafe wote! Najua mutajitahidi kuwafuta katika historia! Bye for now!! Ndimi dada yenu kipenzi!

Dr. Mwakyembe siyo malaika kwa maana kuwa, lazima ana mapungufu katika utendaji wake lakini vile vile hayo mapungufu hayawezi yakawa zaidi ya uozo wa mzoga alioukuta hapo Bandarini. Bandari stinks.

Uozo wa bandari kabla ya Dr. Mwakyembe ulifikia kiwango cha jamii kusema bora anayeiba kidogo na kubakisha kingi kuliko anayeiba vyote kwa maana kwamba, ni afadhali walipe rushwa ili mizigo yao itoke mapema na salama. Fikra kama hii inaonyesha ni jinsi gani jamii ilivyokuwa imekata tamaa na utendaji wa Bandari.

Jamii haihitaji kufanya kazi bandarini au serikalini ili kujua utendaji wa bandari ukoje. Watu kama wewe ambao kwa ubinafsi na unafiki wenu ndiyo mnaifanya jamii ifahamu vizuri utendaji wa bandari.

Mwenye macho haambiwi tazama na Penye wengi haliharibiki neno lakini vile vile ni kupoteza muda kupambana na ukweli.
 
Kikao cha baraza la wafanyakazi kilifanyika Bagamoyo kwa siku mbili Alhamis na Ijumaa. Leo hii Jumamosi tayari Waziri ameshachukuwa mamlaka ya Bodi na kuwatangazia wafanyakazi ongezeko la uboreshaji wa maslahi kabla ya Bodi kupitia! Hoja hapa ndiyo hii!Kiutaratibu ni kwamba uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi hujadiliwa kwenye Baraza la wafanyakazi ambalo linajumuisha chama cha wafanyakazi( DOWUTA ) pamoja na management. Makubaliano yatokayo kwenye kikao hicho hupelekwa kwenye kikao cha Bodi kwa approval na baadaye kwa waziri mwenye dhamana kwa taarifa. Kiutaratibu ni kwamba uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi hujadiliwa kwenye Baraza la wafanyakazi ambalo linajumuisha chama cha wafanyakazi( DOWUTA ) pamoja na management. Makubaliano yatokayo kwenye kikao hicho hupelekwa kwenye kikao cha Bodi kwa approval na baadaye kwa waziri mwenye dhamana kwa taarifa.
Hii Bodi haiwezi kasi ya mabadiliko yanayohitajika Bandarini. Wafanyakazi wa Bandari walishazoea pesa za ulaghai za chap-chap ambazo Mwakyembe kaziziba. Huyu Tina ni member wa management anayejua kuwa hatapona kwenye hiyo siment kali sasa anatafuta huruma hapa JF. Bandari ilikuwa inanuka mno kwa rushwa na ufisadi kabla. Watu walikuwa miungu watu. Sasa wamepatikana kwa Mwakyembe, JEMBE ambalo Mungu kaliokoa kwenye sumu. Mwakyembe kazi mtindo mmoja achana na akina TINA ni wazandiki. TINA kama mzalendo alipokeaje masurufu ya wiki kwa kikao cha siku mbili? halafu anaendelea kukenua meno na kuleta mada ya uongo hapa! Kama mzalendo mwenye uchungu wa kweli arudishe perdiem ya siku zilizozidi. Kibaya anasema anashiriki vikao vya Bodi, what a member are you? MWIZI? Badala ya Kipande kukushughulikia wewe, sasa wewe unataka umpande Kipande, acha hizo
 
Tatizo kila mtu anajua kuandika! Bodo imeundwa juzi na kusifiwa na Mwakyembe, nenda kaangalie kumbukumbu, je wakati ule wafanyakazi hawakuwapo? Sheria na kanuni zinasemaje? Majibu mepesi kwa maswali magumu! Si vyema tukafika mahali tukatukana lakini kuna watu sasa Tanzania wanaweza hata kuharibu utu wao maana wanapenda vibaya jamani lol! Kwamba chongo ni kengeza!!!
Tina, Bodi huundwa kutokana na watu kutoka sehemu tofauti. Kwa kuwaangalia historia zao huwa ni nzuri, lakini ikifika utendaji kwenye hiyo Bodi ndipo inajulikana hawafai au wanafaa. Kwa kukuangalia TINA mtu anaweza kukuteua kwenye Bodi kumbe ni kanyaboya, hata kwenye menejimenti (kama ni kweli) upo kimakosa. Mwakyembe hawezi kuacha kuitoa Bodi eti kwa kuwa aliiteua na kuisifia kwa mbwembwe. Kumbuka hata MUNGU alimteua LUCIFER/ aka SHETANI kuwa mkuu kutokana na sifa za wakati huo, lakini alipo shindwa kujiheshimu akamtimua na anasubiri kibano siku ya mwisho. Mwakyembe timua hiyo bodi. Nashauri pia yeyote anayeingia kwenye bodi ya sasa hivi timua pia maana ni CANCER itaambukiza new management.
 
Tina nini maoni yako kuhusu hii habari hapa chini........

APPOINTMENT OF DIRECTORS AT TANZANIA PORTS AUTHORITY (TPA) IS BEING DONE LEGALLY WITH BLESSINGS FROM THE CIVIL SERVICE COMMISSION, TPA, ACTING DIRECTOR GENERAL, ENG. MADENI KIPANDE HAS SAID.

Eng. Kipande told the ‘Sunday News’ that whoever is opposing the new appointments is part of a cartel of saboteurs who for years have benefitted from shifty deals at the country’s prime port.“We requested support from the Ministry and Civil Service Commission and the ministry suggested competent people and everything is being done in accordance to the law,” Kipande said.Dismissing allegations that the appointment of directors is being done irregularly, parallel to a competitive process which is being presided over by TPA’s board of directors.Reports show that some board members are questioning the process which has so far seen two directors transferred to the Ministry of Transport. “If there is any board member who is complaining then he or she has a personal problem.I advise you to contact the board chairman, the letter that I wrote was simply requesting for the board’s guidance,” he argued. Efforts to get TPA board chairman, Professor Joseph Msambichaka failed as his mobile phone went unanswered and text messages were not responded to......

Reports said Engineer Mathew Mtigumwe from TanRoads is now the Director of Infrastructure taking over from Eng Bakari Kilo who was sacked earlier this year by Transport Minister, Dr Harrison Mwakyembe alongside Director General, Eng Ephraim Mgawe.

Eng William Shilla from TanRoads is now the Director of Engineering and Technical Services, taking over from Julius Mfuko who has been transferred to the Ministry.
“The problem is that all this is happening while an official recruitment process is in place which raises questions as to the authenticity of the exercise,” a source from TPA said.

By FINNIGAN WA SIMBEYE, Tanzania Daily News

Upi n utaratibu sahihi kwa TPA......through Board ya Wakurugenzi au Civil Service Commission....kwanini watu wanatofautiana
 
Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameipa siku moja Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kutaja majina ya watu wanaoiba mafuta katika bomba kubwa la kupakulia mafuta bandarini (SBM). Alisema wezi hao bila woga wowote wametoboa bomba hilo ambalo ujenzi wake umeigharimu serikali mamilioni ya fedha, kuunganisha mabomba yao chini kwa chini kisha kunyonya mafuta hadi kwenye vituo vyao vya kuhifadhia mafuta. “Haiwezekani wizi huo ukafanyika bila TPA kuwajua wahusika kwa sababu hujuma hii inaonyesha kuwa inafanywa na watu wenye utaalamu wa hali ya juu,” alisema Dk Mwakyembe jana wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu changamoto na mafaniko katika utendaji wao wa kazi. Alisema wezi hao wamekuwa wakiibia serikali lita 35,000 hadi 40,000 za mafuta katika kipindi kisichojulikana. Ujenzi wa bomba hilo ulikamilika takriban mwaka mmoja uliopita. Alisisitiza, “Wizi umepungua kwa kiasi kikubwa TPA katika hilo nawapongeza, lakini wapo wachache ambao siyo waaminifu wamebuni mbinu mpya za kuihujumu serikali. Nataka mpaka Jumatatu (kesho) saa 6 mchana niwe nimeletewa hayo majina.” Alisema wizi huo unafanyika katika Kampuni ya kuhifadhia mafuta ya Tipper, huku akiagiza kampuni hiyo kuvunja mkataba na kampuni ya ulinzi inayolinda mafuta hayo. “Hao Tipper nao inatakiwa muwalete ili wawataje waliohusika na wizi huo. Pia nasikia kuna raia mmoja wa kigeni (mzungu) anatoa rushwa ili kufanikisha wizi huu. Katika hili nasema watarudi kwao Ulaya,” alisema na kuongeza: “Suala hili nimeshamfikishia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusu uhujumu uchumi unaofanywa na kampuni hii ya Tipper, amesikitika kweli.” Alisema kutokana na uzito wa suala hilo anashirikiana na Wizara ya Nishati na Madini ili kuhakikisha kuwa wote waliohusika wanachukuliwa hatua. “Serikali haitakaa kimya katika hili, kilichofanyika ni hujuma ambayo ingeweza kuangusha uchumi wa nchi na kuzorotesha huduma za kijamii. Ni lazima wahusika washughulikiwe” alisema. Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe aliutaka uongozi wa TPA kuachana na mpango wake wa kupeleka boti na mitambo mingine kwenye karakana zilizoko Mombasa, Kenya, kwa ajili ya matengenezo, “Huu mpango ni wa ulaji wa wachache tu.” Alisema mamlaka hiyo inatakiwa kujipanga kwa kuandaa bajeti itakayowasaidia kujenga karakana yake. SOURCE: Mwananchi,Jumapili
 
Tina nini maoni yako kuhusu hii habari hapa chini........

Upi n utaratibu sahihi kwa TPA......through Board ya Wakurugenzi au Civil Service Commission....kwanini watu wanatofautiana

Utaratibu sahihi kwa TPA ni Kwa kupitia board ya wakurugenzi. Kiasi naanza kuamini board inahoja.
 
Tina usife moyo ! ukweli ni kwamba Mwakyembe anaiua na kuizika TPA. Ana agenda ya siri. Waziri unafanya kazi kupitia bodi na si vinginevyo. Tofauti kabisa na best management practices amekuwa part and parcel ya TPA management na lazima tujiulize why? and the reason is very simple to retain the status quo. Bodi ni ya kwake kwa nini aniogopa na kuikwepa katika maamuzi yake yasiyozingatia utaratibu. Kiongoxi ambaye siku zote ni kutafuta cheap popularity ni kiongozi hatari sana. To date hakuna maagizo yake yote aliyotoa yamefanyiwa kazi kwa kuwa yote yameonekana hayana mashiko kisheria au kimenejimenti. Juzi tu ametoa maagizo kwa TRA ambayo haiko chini ya wizara yake isimamishe an automated system irudi kwenye manual!
 
Badala ya Mwakyembe kuwaambia menejiment ya TPA wataje wezi wanaoiba mafuta kutoka katika bomba la kupakulia mafuta kwa nini asiagize ufuatiliaji wa hayo mabomba yaliyounganishwa kienyeji hadi mwisho wake?

Hii itakuwa njia rahisi na yenye uthibitisho. Hao wezi wakikamatwa watawataja viongozi wa TPA walioshirikiana nao kufanya huo uhalifu.
 
Hii ni drama nyingine! Mwakyembe aliitimua bodi na management iliyopita kwa madai kuna wizi! Leo anazungumzia wizi anairuka management maana wanajuana. Haa ajue kama kuna wizi kweli hajatatua tatizo na hajaelekeza hoja yake mahala husika na kimsingi ni sinema za kutafuta headlines za magazeti hakuna nia njema ya kutatua tatizo ni 'Mrema style' enzi za Naibu Waziri Mkuu!! Hili ni janga jamani hamjui tu. Tujiulize kesi za waliokamatwa kwa wizi wa mafuta ziko wap? Kesi ya mlinzi aliyetekwa ziko wap? Basi amfukuze na Kipande kwa wizi! Hapa anakwepa hoja ya matatizo yake na management na bodi anaibua sinema ya headlines! Ndio maana hata hapa imewekwa. Angalieni kila kukiwa na issue, kutakoea drama ya kupoteza lengo!! Tuamke Watanzania

Tusome hii
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=53653
 
Uombewe maana hujui utendalo. Na we kama hazikuumi ama kukuhusu, povu la mini? Kaa pembeni wasome wenye kujua ulipo uchumi wa nchi. Ninashiriki hivyo vikao na ujue sitoacha kusema japo KIPANDE NA WAZIRI WANANIPENDELEA KULIKO WENZANGU, MEZA WEMBE WEEE MAANA MIMI NINGEKUA MBINAFSI NISINGESEMA MAAMA NAPATA ULAJI KISHENZI. WATU WAMEENDA BAGAMOYO KIKAO CHA SIKU 2 ALHAMISI NA IJUMAA ULAJI POSHO YA SIKU SITA

huyu mama nafikiri ni vizuri Uraia wake ukafuatiliwa nina mashaka nae ana nia ya kufanya sabotage ili ufanisi usiwepo TPA kwa manufaa ya nani ??!!. Kwa nini kauli zake ni za kimajungu tu !!!! Watu wa uhamiaji kuleni sahani moja na huyu mhujumu uchumi ambae bila shaka anahusika kutoboa Bomba la mafuta.
 
huwa nashindwa kabisa kuwaamini wanasiasa wa CCM,wanafanya maamuzi kwa maslahi yao wenyewe,Mwakyembe mwenyewe baada ya kuwafukuza watu bandarini akaweka ndugu na marafiki zake,na wao wanachemsha vilevile,tangu mwanzo niliwahi kusema suala la kufukuza watu halitatatua tatizo,the ishu ni kuubadili mfumo wote wa utendaji kazi,mfumo wenyewe udhibiti wizi,na kuinfluence utendaji wenye tija,maana hakuna mzalendo anayeweza kuona tundu linavuja pesa akaziangalia tu,hayupo kabisaaa!!kila atakaye kuwa anaingia anafukuza waliopo anaweka washkaji zake
 
Siasa za tanzania mie siwez kuwa mshabiki ngoja niende kushabikia bongo fleva#tupogo- political art of eating
 
Uombewe maana hujui utendalo. Na we kama hazikuumi ama kukuhusu, povu la mini? Kaa pembeni wasome wenye kujua ulipo uchumi wa nchi. Ninashiriki hivyo vikao na ujue sitoacha kusema japo KIPANDE NA WAZIRI WANANIPENDELEA KULIKO WENZANGU, MEZA WEMBE WEEE MAANA MIMI NINGEKUA MBINAFSI NISINGESEMA MAAMA NAPATA ULAJI KISHENZI. WATU WAMEENDA BAGAMOYO KIKAO CHA SIKU 2 ALHAMISI NA IJUMAA ULAJI POSHO YA SIKU SITA

Hapa JF kuna watu wa fani mbalimbali na wajuzi wa mambo. kule kusema ETI katika uzi wako unataka kumaanisha Mwakyembe amekosea na anataka kulazimisha aungwe mkono. katika vita hii TINA huta shinda, kumbuka MUNGU huwa upande wa HAKI.wanaojua mambo wanajua unahangaikia tumbo lako tu na siyo zaidi ya hapo.kwani BOARD ni nini? watu tunataka tija na ufanisi tu ili TAIFA LISONGE MBELE.
 
naburudika sana maana hujui usemalo. Fanya utafiti. Mwenzako kaja na mpya ya kutaka uhamiaji wachunguze uraia wangu. Kati yangu na nyie inaonyesha wazi nyie ndio mko kazini maana munatukana, munatishia, kashfa, udhailishaji na wote munajielekeza kuwadharau wanawake mukiamini na mm mwanamke tena ready muna jina kichwani. Niwe mwanamke ama mwanaume, someni na kujibu hoja si jazba. Angalieni nafasi zenu kwa kutenda haki. Fanyeni utafiti si kukurupuka na kutoa kauli zenye utata.
 
Kuna watu walifanya bandari kama ni nyumbani kwao na sio ofisi ya umma kama nyingine.
 
naburudika sana maana hujui usemalo. Fanya utafiti. Mwenzako kaja na mpya ya kutaka uhamiaji wachunguze uraia wangu. Kati yangu na nyie inaonyesha wazi nyie ndio mko kazini maana munatukana, munatishia, kashfa, udhailishaji na wote munajielekeza kuwadharau wanawake mukiamini na mm mwanamke tena ready muna jina kichwani. Niwe mwanamke ama mwanaume, someni na kujibu hoja si jazba. Angalieni nafasi zenu kwa kutenda haki. Fanyeni utafiti si kukurupuka na kutoa kauli zenye utata.
No, no do not jump to conclusion kwamba watu wamekuhukumu kwa kudhani wewe ni mwanamke au la.

Ukweli ni kwamba watu wanaangalia madudu yaliyo kuwa yanafanywa pale TPA as if hakuna uongozi au hiyo BOARD unayoitetea na kutaka kuihalalisha uwepo wake.

Kumbuka Rais KAGAME amewahi kusema ile bandari angepewa yeye au serikali yake mapato yangeongezeka almost ten times! BOARD ilikuwepo na wala hawakuwahi kujiuliza kwanini Kagame aseme hivyo.

Lakini pia toka Mwakyembe aingilie kati mapato ya TPA yameongezeka almst three times.Je, akifanikiwa kuziba mianya yote ya wizi na kuongeza speed ya kuondoa mizingo si mapato yataongezeka zaidi?

Ndio maana kila anae mchukia DR, WATU WANATUKANA YEYE KWANZA NA KUTAKIA MWAKYEMBE AFYA NJEMA ILI AZIBE KILA UOZO PALE TPA.
 
Mkuu, mimi sijanasa na wala siwezi kunasa kwa sababu sijaleta hoja za kinafiki na kizandiki au kujibu hoja kwa kinafiki au kizandiki.

Ninajibu hoja kulingana na maelezo yako unayoleta mezani ikiwa pia na yale ambayo yamejificha ndani ya hayo maelezo(between a line).

Polisi au vyombo vya usalama huwa mara nyingine vinatumia mabavu na nguvu kupata ushahidi au vielelezo zaidi kutoka kwa watuhumiwa lakini kwako imekuwa ni tofauti kwa sababu umenasa na unadhani kufunguka zaidi ndiyo kuta adjust or alter opinion na mitazamo ya wanaJF wengi kuhusiana na utendaji wa Dr. Mwakyembe ili upate back up to substantiate and validate your relentless and negative crusade.

Kitu ninachokiona hapa ni vindication, at the sametime, it just reinforces a well documented case kuwa bandari ilikuwa kama mzoga ambapo kwa sasa mainzi na fisi wanapambana kuhakikisha hawaondoki kwa urahisi.

Dr. Mwakyembe siyo malaika kwa maana kuwa, lazima ana mapungufu katika utendaji wake lakini vile vile hayo mapungufu hayawezi yakawa zaidi ya uozo wa mzoga alioukuta hapo Bandarini. Bandari stinks.

Uozo wa bandari kabla ya Dr. Mwakyembe ulifikia kiwango cha jamii kusema bora anayeiba kidogo na kubakisha kingi kuliko anayeiba vyote kwa maana kwamba, ni afadhali walipe rushwa ili mizigo yao itoke mapema na salama. Fikra kama hii inaonyesha ni jinsi gani jamii ilivyokuwa imekata tamaa na utendaji wa Bandari.

Jamii haihitaji kufanya kazi bandarini au serikalini ili kujua utendaji wa bandari ukoje. Watu kama wewe ambao kwa ubinafsi na unafiki wenu ndiyo mnaifanya jamii ifahamu vizuri utendaji wa bandari.

Mwenye macho haambiwi tazama na Penye wengi haliharibiki neno lakini vile vile ni kupoteza muda kupambana na ukweli.

Bahati mbaya sana Watanzania tukiamini jambo tunakua vipofu. Mifano ni mingi hasa kwa wanasiasa, siwezi kuitaja maana nitaibua mjadala mpya hapa, yatosha tu kusema hata mm nimefanya kazi sana na Mwakyembe lakini anaweza, tatizo lake kubwa anapenda kucheza na akili za watu na hapendi kukosolewa. Katika hili Kuna uozo mwingi soma huko juu na jinsi anavyokwepa hoja kwa kuanzisha mjadala tofauti kunapokua na issue. Time will tell.

Kwa taarifa yako sijawahi kuwa mnafiki na ninachofanya hadi uvue huo Umwakyembe ndio utanielewa. Hivi management inapoghushi nyaraka kuhalalisha mkataba wa kifisadi tunasema mapungufu madogo! Kwa sababu tu Mwakyembe anawatetea! Kwanini Mwakyembe asiwaache wajitetee? Kwani yeye ni Waziri sio DG. Mbona kwingine wanavuruga na wanasemwa haingilii?

Tufumbue macho na tumsaidie kwa kumwambia awe msikivu asiwe mtengeneza headlines kila siku afanye kazi sio atangaze kazi. Drama hazisaidii
 
Chagueni watu wenye utaalam ndio wasaidie kuiendesha hiyo bandari badala ya kuingiza siasa!!! wataalam tunao wengi lakini hatuwatumii kwa sababu za ubinafsi!!!
 
tina , mimi nimekuelewa na kwa bahati mwakyembe , kipande nawajua kwa karibu mno na hata kiutendaji , kwanza wana tabia moja hawa watu ya jamii kuwatambua na kuonekana zaidi , wanapobanwa huwa wanachanganyikiwa na kuwa na hasira ambacho si kitu kizuri kwao. kwa upande wa kazi ni watu wenye mipango madhubuti na dhamira nzuri , ila kama binadamu hawawezi kukosa mapungufu ya kawaida , hebu kwa sasa tuwachukuliwe kwa muda huu positevely na tuwashauri kwa kupitia hao wanaowaamini wao. nijuavyo mimi bandari si kama mamlaka zingine inatakiwa ujasiri ambao nauona sasa, na ndiyo maana miaka yote watu kimabandari(baharia, supervisors) huwa kama wehu kutokana na heka heka chini mpaka juu

Well stated
 
Back
Top Bottom