Mwakyembe aigeuka rasmi bodi Bandari, kuivunja

Mwakyembe aigeuka rasmi bodi Bandari, kuivunja

Tina

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2007
Posts
572
Reaction score
584
Agenda ya Mwakyembe ya kufanya mkutano na wafanyakazi wa TPA ni kutafuta kuungwa mkono pamoja na kuprempt kikao cha Bodi kilichopangwa kufanyika siku ya Jumanne ijayo agenda zake mojawapo ikiwa kujadili maswala ya maslahi ya wafanyakazi.

Kwa kawaida Bodi ndicho chombo cha kupitia mapendekezo yoyote yanayowasilishwa na management na kuyapitisha au kuyafanyia marekebisho kabla ya waziri kufahamishwa ikiwa ni kwa taarifa tu. Hapa inavyoonyesha waziri amekaa na management( Kipande) na kuamua kutangaza kuyapandisha maslahi ya wafanyakazi bila Bodi kuhusika!

Kwenye kikao katika kile kilichoonekana ni kutaka kukonga nyoyo za wafanyakazi Mwakyembe amewaambia eti kwa sasa kuna ufa kwenye Bodi yake aliyoiweka kwa mbwembe mwaka jana hivyo atatumia cement kali kuziba na kuahidi kumweka mwakilishi wa wafanyakazi ( DOWUTA ) kwenye bodi atakayoisuka umpya! Hapa Mwakyembe na Kipande wametengeneza sanaa ya kutafuta kuungwa mkono na wafanyakazi kwa kuwapa aina fulani ya rushwa kwa njia ya uboreshaji wa maslahi!

Waziri anataka kurudisha utendaji ndani ya TPA kama enzi za mashirika ya umma ambayo yalifilisika. Wakati ule mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi alikuwa anaingizwa kwenye bodi nafasi ambayo anaweza hata kumkemea DG wake!!

tukio la kusikitisha ni Kipande kuanguka na tuliokuwapo tunamuombea Mungu apone na tunasema waliovumisha kuwa alikua na hirizi zilizomuelemea washindwe kwani ni uzushi kwa kuwa Madeni alipata tatizo la kawaida la kiafya na ni uchovu pamoja na maradhi
 
Leta habari nyingine wewe muhanga wa bandari kutwa nzima ni habari za Kipande saga chupa unywe nyambaf wewe

Uombewe maana hujui utendalo. Na we kama hazikuumi ama kukuhusu, povu la mini? Kaa pembeni wasome wenye kujua ulipo uchumi wa nchi. Ninashiriki hivyo vikao na ujue sitoacha kusema japo KIPANDE NA WAZIRI WANANIPENDELEA KULIKO WENZANGU, MEZA WEMBE WEEE MAANA MIMI NINGEKUA MBINAFSI NISINGESEMA MAAMA NAPATA ULAJI KISHENZI. WATU WAMEENDA BAGAMOYO KIKAO CHA SIKU 2 ALHAMISI NA IJUMAA ULAJI POSHO YA SIKU SITA
 
Penye mzoga msituni, mainzi na mafisi hayakosekani.

Hata vita zinazoendelea katika nchi mbali mbali zenye utajiri wa natural resources haipiganwi kwa sababu ya manufaa kwa wananchi wa nchi hizo bali kwa sababu ya manufaa ya wachache kupata natural resources.

Kwenye siasa na pesa huwa hakuna rafiki wa kudumu na adui wa kudumu.
 
Tina@wewe na tpa mara ukanushe mara uunge mkono what your stands

fafanua. Nimekanusha nini? Sikuelewi. Soma chini ya mstari. Ninachowasilisha ni taarifa si maoni yangu. Maoni yangu ni kwamba hata Mwakyembe amechoka na Kipande lakini ana jambo linalomshika kwa sasa. Time will tell.
 
Mwakyembe Kila la Kheri kwenye kazi kubwa ya kusafisha Kitalu cha Bandari!

siasa na uchumi vinahitaji uvumilivu na imani ya kweli na nchi si Sanaa zinazoendelea sasa. Tumekwisha kama Taifa. Iko siku tutajua kuwa nchi imetumbukia ktk dimbwi la ulafi mkubwa. Hamtajua maana akili zimeshikwa na wengine wanawasaidia kufikiri na nyie munaimba kama kasuku.
 
na bado cement lazima ikumalize ww mpenda rushwa

Naamini asilimia 99 hukumbuki umeandika nini. Ukimaliza kusoma maandishi yangu lazima utarudi kuiaoma post yako uliyoandika ujikumbushe umeandika nini. Hii inadhihirisha namna usivyokumbuka na kujua ufanyalo
 
Leta habari nyingine wewe muhanga wa bandari kutwa nzima ni habari za Kipande saga chupa unywe nyambaf wewe

Habari hii ni muhimu sana kwa mustakhabali wa taifa. Weee unaona bla bla kaa kimya. Mtu akisema kweli mradi tu ikiwa against mwakyembe basi amekuwa mhanga wa bandari, what a rubbish!
Kama una hoja yenye akili zaidi toa sio kulalama tu na kauli ya uhanga wa bandari!
 
Uombewe maana hujui utendalo. Na we kama hazikuumi ama kukuhusu, povu la mini? Kaa pembeni wasome wenye kujua ulipo uchumi wa nchi. Ninashiriki hivyo vikao na ujue sitoacha kusema japo KIPANDE NA WAZIRI WANANIPENDELEA KULIKO WENZANGU, MEZA WEMBE WEEE MAANA MIMI NINGEKUA MBINAFSI NISINGESEMA MAAMA NAPATA ULAJI KISHENZI. WATU WAMEENDA BAGAMOYO KIKAO CHA SIKU 2 ALHAMISI NA IJUMAA ULAJI POSHO YA SIKU SITA
Now you're talking!. Umetingishwa kidogo na wanaJF kwa sasa umeanza kufunguka. , it's the naked truth, you're acting as double agent kwa maslahi yako kwenye uwekezaji wa taifa kitu ambacho ni kosa kubwa sana.

Maelezo yako yanaonyesha UNAFIKI na UZANDIKI wa hali ya juu. Kama kweli unawapigania wajumbe wa bodi na taifa kama unavyodai, kwa nini huusemi ukweli kwenye bodi na kwenye uso wa Dr. Mwakyembe na badala yake uko very happy kupokea pesa za chini ya meza huku ukijifanya kwenye nyuso za kila kundi kuwa uko upande wao.

Maelezo yako yanaonekana wewe ni mwasilika wa mageuzi ndani ya bandari kwa sababu maelezo yako yanadhihilisha kuwa pesa unayopata kwa sasa ni ndogo ikilinganishwa na kipindi ambacho Dr. Mwakyembe na Kipande hawakuwepo ndiyo maana unadhani kuondoka kwa Kipande na Mwakyembe kutarejesha pesa uliyokuwa unapata mwanzoni.

I'm sorry, Unafiki ni kitu kibaya sana. Hii ni kansa kitaifa.
 
Naamini asilimia 99 hukumbuki umeandika nini. Ukimaliza kusoma maandishi yangu lazima utarudi kuiaoma post yako uliyoandika ujikumbushe umeandika nini. Hii inadhihirisha namna usivyokumbuka na kujua ufanyalo

kuioma ndo nini? hata kuandika na kusoma hujui,ulipasi vipi shule au ndo nyie akina said mara hamis!! kingwa.
 
Mtoa mada ni mnafiki aliyezidi kipomo! Kaniudhi sehemu Moja beyond explanation. Eti she is opposed to the idea of having a representative wa wafanyakazi kwenye bodi on flimsy grounds za mtu wa Memkwa! Go ahead wana JF, shake her a bit more! Viva Mwakyembe.
 
Haa haa, mleta mada pole naona rungu limekukamata, pole kama ulaji umekata
 
Eti una uchungu wa watanzania acha unafiki sema Wewe ni muathirika wa mabadiliko haya
 
Tina , mimi nimekuelewa na kwa bahati mwakyembe , kipande nawajua kwa karibu mno na hata kiutendaji , kwanza wana tabia moja hawa watu ya jamii kuwatambua na kuonekana zaidi , wanapobanwa huwa wanachanganyikiwa na kuwa na hasira ambacho si kitu kizuri kwao.

Kwa upande wa kazi ni watu wenye mipango madhubuti na dhamira nzuri , ila kama binadamu hawawezi kukosa mapungufu ya kawaida , hebu kwa sasa tuwachukuliwe kwa muda huu positevely na tuwashauri kwa kupitia hao wanaowaamini wao.

Nijuavyo mimi bandari si kama mamlaka zingine inatakiwa ujasiri ambao nauona sasa, na ndiyo maana miaka yote watu kimabandari(baharia, supervisors) huwa kama wehu kutokana na heka heka chini mpaka juu
 
Back
Top Bottom