Mwaka unaisha, umefanikiwa kufanya nini?

Nilikuwa na malengo ya kufungua kibiashara nilifanikiwa but kwa bahati mbaya kimeshindwa kuendelea hapa mwishon mwa mwaka ila mwakani nitatia nguvu kwenye biashara, Mwaka huu nimeandamwa na kuumwa sana tumbo kila nikipima

wanasema ni dalili ya vidonda au acid tumboni ila mwakani Mungu anisaidie niishi kwa kufuata mashart yasinitokee tena.
Nilipata hela kiasi nikafanya matumizi ambayo hayakuwepo kwenye budget hadi kupoteza pesa nyingi kwenye muda mfupi kisababishi ni mwanamke mwakani hela ya budget itayozidi ndio nitaitumia huko au nitatia nguvu kwenye ishu ya maana.

Nimempoteza watu niliokua nawafuatilia kujituma na kufanikiwa kwao Ruge Mutahaba na Regnald Mengi.
Mwisho na nachomshukuru Mungu zaidi niliweka lengo kwenye kijumba changu nifike kwenye lenta mwaka huu mafundi wapo site muda huu wanamalizia hizo line sita juu kutoka kwenye madirisha nifunge lenta licha ya hiki kipato kidogo.
 
Nimefanikiwa kwa mambo mengi ikiwemo ya kiroho 1.NIMEWAJUA ADUI ZANGU WOTE

2.NIMEACHANA NA MWANAMKE ALIYENIZINGUA NA KUNIRUDISHA NYUMA KIMAISHA

3.NIMEMILIK IPHONE KIDOGO MOYO UMETULIA

4.NIMEFANIKIWA KUFUNGUA SALOON YA KIKE MPYA

HATA KWA UHAI HUUU BADO NAMSHUKURU SANA MUNGU NAENDELEA KUPITA KATIKA YA WATESI WANGU ....NA HAWANA LA KUNIFANYA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka huu:

1. Nimeongeza ujuzi kwenye forex.

2. Nimejifunza website development (Hii nataka niitumie sana mwakani, infact mpaka sasa nimetengeneza websites mbili).

3. Nimesoma vitabu vinne vya kuongeza maarifa.

4. Nimeboresha ujuzi katika kazi yangu.

5. Nimejifunza kwamba "Bila pesa furaha hakuna".

6. Nimejifunza social media marketing hasa kwenye facebook na instagram.

MWaka huu sehemu kubwa nimetumia katika kuongeza ujuzi hasa maeneo yasiyo ya fani yangu!

The idea ni kuwa na wigo mpana kiuchumi! Kuanzia mwaka natarajia kuanza kuona matunda kwa uwekezaji wa elimu/ujuzi nilioufanywa mwaka huu.

Kwa sasa nakumbuka hayo.
Keep it up all the best in the coming year 2020
 
Wasalaam.

Zimesalia siku 20 tu mwaka 2019 uishe. Ni siku chache kweli kweli na zinakwenda kasi haswa.

Wengi watakuwa wanatafakari namna miezi 12 ilivyokwisha na huku wangali:

- Hawajatimiza malengo waliyojiwekea.

- Maisha yameharibika na kuvurugika.

- Familia zimesambaratika.

- Kupoteza ndugu jamaa na marafiki (misiba)

- Kuachwa/kusalitiwa ama kuachana.

- Kutimiza malengo ya kiuchumi na kifamilia.

- Kununua gari/kiwanja.

- Kujiwekea akiba.

- Kupata ulemavu.

- Kupoteza ajira nk.

Bila shaka kwa namna moja ama nyingine wengi tunaweza kuangukia katika masuala kama haya na mengine mengi.

Kwa kuanza na wale waliofanikisha malengo ya hapa na pale hongereni sana, haitoshi juhudu ziongezwe angalau mwaka ujao muwe pazuri zaidi.

Na wale kina wenzangu tuliofanikiwa kusajili kitambulisho cha NIDA, tupeane pole, maisha ndivyo yalivyo tusikate tamaa kwani kitambulisho nacho si mafanikio pia.

Mwenzangu umefanikisha nini mwaka 2019?

View attachment 1287987
Nimepima kuona kama nina maambukizi ya VVU. mara ya mwisho nimepima mwaka 2000. Nimekuwa na shauku ya kupima tangu 2012 lakini naogopa. Mwaka huu nimejilipua hospitali mbili tofauti one day. nimeanzia mwanayamara nikapewa majibu nikaenda mnazi mmoja same day. Wakati nipo Mwananyamara nilitangulizana na dada mmoja bonge sana mbele yangu akapima akatoka kusubuli baadae namimi nikapima nikaambiwa nisubili dakika kumi. Yule dada akaanza kuingia kuchukua majibu. Sasa wakati nipo mlangoni nasubili kuingia mlango ukafunguka kwa upepo nikaona yule dada anakabidhiwa makopo ya dawa kidogo nikimbie foleni ila nikajipa moyo. Alipotoka nikaingia jamaa akaanza kuniuliza maswali meengi huku anaandika kwenye daftari. Unaishi na nani? umeoa?du mimi nishachanganyikiwa. Mwisho kabisa ananiambia uko salama sikuaga. Nikatoka nikaenda mnazi mmoja hospital moja kwa moja kama vile sijapima napo niaambiwa nipo salama.

Kwa kweli kila nikiona mdada mzuri namkumbuka yule aliekuwa kwenye foleni mbele yangu kule mwananyamala sina hamu tena na wanawake wa njiani. sirudimo tena kwenye hiyo njia ya mashaka.
 
Mwaka huu:

1. Nimeongeza ujuzi kwenye forex.

2. Nimejifunza website development (Hii nataka niitumie sana mwakani, infact mpaka sasa nimetengeneza websites mbili).

3. Nimesoma vitabu vinne vya kuongeza maarifa.

4. Nimeboresha ujuzi katika kazi yangu.

5. Nimejifunza kwamba "Bila pesa furaha hakuna".

6. Nimejifunza social media marketing hasa kwenye facebook na instagram.

MWaka huu sehemu kubwa nimetumia katika kuongeza ujuzi hasa maeneo yasiyo ya fani yangu!

The idea ni kuwa na wigo mpana kiuchumi! Kuanzia mwaka natarajia kuanza kuona matunda kwa uwekezaji wa elimu/ujuzi nilioufanywa mwaka huu.

Kwa sasa nakumbuka hayo.
Sawa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom