Mwaka Mpya 2021 umeanza; umejiwekea Malengo yapi? Malengo yangu niliyojiwekea ni haya

Malengo yangu ni, work hard, spend less, save more...my spending has left so much to be desired.
 
Kule kuna umafia na mauzauza mengi sana. Inahitaji iwe na roho ngumu sana.
Nitajaribu Mwaka huu, nimeshakuja kukita kambi kutafuta maeneo ya kuchimba.

Nikiona wanaleta habari za kutoana Makafara ndiyo nitaachana na hiyo biashara
 
Salaam,

Mwaka 2020 umeisha na sasa tumeanza Mwaka Mpya 2021. Wengi mtakuwa mlijiwekea malengo mbalimbali yawe makubwa, ya kati au madogo kwa mwaka uliopita, lakini kwa sababu mbalimbali kuna mliofanikiwa kuyatimiza na wengine mkashindwa kuyatimiza. Sizungumzii kuhusu malengo ya kuoa au kuolewa kwani binafsi nahisi ni kama malengo ya kijamii zaidi kwani ili kuyafanikisha unahitaji Support ya Ndugu na Jamaa.

Kufanikiwa kutimiza malengo yako au kushindwa kuyatimiza malengo yako, hakukufanyi ushindwe kujiwekea malengo Mapya mwaka huu wa 2021. Muda wa kujiwekea malengo ni sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza Januari 2021.

Binafsi Mwaka huu 2021 nimejiwekea malengo yafuatayo;-
  • Kukamilisha Ujenzi wa apartment mbili kwa ajili ya kupangisha
  • Kuanza Ujenzi wa Lodge ya vyumba 12
  • Kuanzisha shamba la ekari 50 za Korosho
  • Kufungua mgodi mdogo wa Dhahabu na kuanza uchimbaji
  • Kununua gari la kutembelea
  • Kuhakikisha malipo ya ada ya Mwaka kwa Watoto inalipwa.
Vyanzo vya Fedha
Ili kutimiza malengo yeyote uliyojiwekea ni muhimu kuwaza kuhusu rasilimali fedha itakayohitajika, Binafsi nategemea vyanzo vifuatavyo kutumika kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yangu. Vyanzo hivyo ni;-
  • Kupitia Mikopo kutoka Taasisi za Fedha
  • Kupitia mapato ya biashara
  • Kupitia mapato ya Kodi kutoka kwenye apartments zangu
  • Kupitia Mavuno ya Shambani
  • Kupitia mauzo ya gari lililopo
Maisha yana changamoto lukuki, lakini bila kujiwekea malengo itakuwa tunahesabu miaka ikikatika huku hali zetu za kimaisha na Kijamii zikibaki vilevile miaka nenda miaka rudi.

Swali ni Je, Umejiwekea Malengo gani Mwaka huu 2021?
watakuja tu inbobo...ulimbo mkali huu...mitano tena
 
Unadhani tukiacha kukumbushana kama hivi unategemea nani aje akukumbushe?

Unaikumbuka nyimbo ya Twanga Pepeta, Fainali Uzeeni

Keep fighting man 💪
 
ha
Salaam,

Mwaka 2020 umeisha na sasa tumeanza Mwaka Mpya 2021. Wengi mtakuwa mlijiwekea malengo mbalimbali yawe makubwa, ya kati au madogo kwa mwaka uliopita, lakini kwa sababu mbalimbali kuna mliofanikiwa kuyatimiza na wengine mkashindwa kuyatimiza. Sizungumzii kuhusu malengo ya kuoa au kuolewa kwani binafsi nahisi ni kama malengo ya kijamii zaidi kwani ili kuyafanikisha unahitaji Support ya Ndugu na Jamaa.

Kufanikiwa kutimiza malengo yako au kushindwa kuyatimiza malengo yako, hakukufanyi ushindwe kujiwekea malengo Mapya mwaka huu wa 2021. Muda wa kujiwekea malengo ni sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza Januari 2021.

Binafsi Mwaka huu 2021 nimejiwekea malengo yafuatayo;-
  • Kukamilisha Ujenzi wa apartment mbili kwa ajili ya kupangisha
  • Kuanza Ujenzi wa Lodge ya vyumba 12
  • Kuanzisha shamba la ekari 50 za Korosho
  • Kufungua mgodi mdogo wa Dhahabu na kuanza uchimbaji
  • Kununua gari la kutembelea
  • Kuhakikisha malipo ya ada ya Mwaka kwa Watoto inalipwa.
Vyanzo vya Fedha
Ili kutimiza malengo yeyote uliyojiwekea ni muhimu kuwaza kuhusu rasilimali fedha itakayohitajika, Binafsi nategemea vyanzo vifuatavyo kutumika kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yangu. Vyanzo hivyo ni;-
  • Kupitia Mikopo kutoka Taasisi za Fedha
  • Kupitia mapato ya biashara
  • Kupitia mapato ya Kodi kutoka kwenye apartments zangu
  • Kupitia Mavuno ya Shambani
  • Kupitia mauzo ya gari lililopo
Maisha yana changamoto lukuki, lakini bila kujiwekea malengo itakuwa tunahesabu miaka ikikatika huku hali zetu za kimaisha na Kijamii zikibaki vilevile miaka nenda miaka rudi.

Swali ni Je, Umejiwekea Malengo gani Mwaka huu 2021?
haraka haraka investment zako kama zipo Tanzania nzima..dhahabu shinyanga/mbeya appartment arusha/dar es salaam dodoma, korosho-mtwara/newala....hongera unaweza break down tuone unataka wekeza kiasi gani
 
Why should I tell every thing Sir.

Gharama za uwekezaji huwa zinatofautiana kutoka eneo moja hadi lingine.

Mind, you can also do your Maths to have preliminary costs for the type of investment that I do and share them here.

Mines let keep for myself. I am sorry
 
Even wastaafu tuna mipango uuuuwiii, nifungue fresh food niweke na two rooms for renting na niwe na serving ya kuamkia mwakani. God knows will do
Hiyo imekaa bomba Sana 👏👏👏

Muhimu serving ipatikane by hooks and crooks

Kumbe Pension umeanza kulipwa? Tukaribishane kuila wote 😋
 
Back
Top Bottom