Mwaka Mpya 2021 umeanza; umejiwekea Malengo yapi? Malengo yangu niliyojiwekea ni haya

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,644
2,000
Salaam,

Mwaka 2020 umeisha na sasa tumeanza Mwaka Mpya 2021. Wengi mtakuwa mlijiwekea malengo mbalimbali yawe makubwa, ya kati au madogo kwa mwaka uliopita, lakini kwa sababu mbalimbali kuna mliofanikiwa kuyatimiza na wengine mkashindwa kuyatimiza. Sizungumzii kuhusu malengo ya kuoa au kuolewa kwani binafsi nahisi ni kama malengo ya kijamii zaidi kwani ili kuyafanikisha unahitaji Support ya Ndugu na Jamaa.

Kufanikiwa kutimiza malengo yako au kushindwa kuyatimiza malengo yako, hakukufanyi ushindwe kujiwekea malengo Mapya mwaka huu wa 2021. Muda wa kujiwekea malengo ni sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza Januari 2021.

Binafsi Mwaka huu 2021 nimejiwekea malengo yafuatayo;-
 • Kukamilisha Ujenzi wa apartment mbili kwa ajili ya kupangisha
 • Kuanza Ujenzi wa Lodge ya vyumba 12
 • Kuanzisha shamba la ekari 50 za Korosho
 • Kufungua mgodi mdogo wa Dhahabu na kuanza uchimbaji
 • Kununua gari la kutembelea
 • Kuhakikisha malipo ya ada ya Mwaka kwa Watoto inalipwa.
Vyanzo vya Fedha
Ili kutimiza malengo yeyote uliyojiwekea ni muhimu kuwaza kuhusu rasilimali fedha itakayohitajika, Binafsi nategemea vyanzo vifuatavyo kutumika kupata fedha kwa ajili ya kutimiza malengo yangu. Vyanzo hivyo ni;-
 • Kupitia Mikopo kutoka Taasisi za Fedha
 • Kupitia mapato ya biashara
 • Kupitia mapato ya Kodi kutoka kwenye apartments zangu
 • Kupitia Mavuno ya Shambani
 • Kupitia mauzo ya gari lililopo
Maisha yana changamoto lukuki, lakini bila kujiwekea malengo itakuwa tunahesabu miaka ikikatika huku hali zetu za kimaisha na Kijamii zikibaki vilevile miaka nenda miaka rudi.

Swali ni Je, Umejiwekea Malengo gani Mwaka huu 2021?
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,623
2,000
Am struggling to move from level four forex trader to level five where I will be unconscious competence trader. That's final stages of trading. Where someone become master of himself
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,644
2,000
Am struggling to move from level four forex trader to level five where I will be unconscious competence trader. That's final stages of trading. Where someone become master of himself
That's nice Man. Whatever you are doing is real fine as far you are making Money
 

Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
2,147
2,000
Mpango mkuu ni kuacha tungi aise vijisenti vyote vinaishia huko naju nikiweza hilo basi mipango mingine itapangika fresh kabisaaaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom