Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
Kesho ni kumbukumbu ya kutimiza mwaka 1 toka Raisi wa 5 wa Tanzania John Pombe Magufuli alipo fariki dunia, Magufuli alikuwa ni M-Socialist wa mlengo mkali wa Shoto na mwanamagauzi mkubwa wa uchumi.

Ni yeye Magufuli ambaye ameacha legacy kubwa sana Tanzania ya vitu ambavyo ni alama ya uongozi wake, vitu hivyo ni pamoja na;

1. Daraja la Busisi (Magufuli bridge)...

Daraja la Busisi-Kigongo linalojengwa katika ziwa Victoria lenye urefu wa mita 3,200 (sawa na kilomita 3.2) na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 1.66 ndio ilitakiwa daraja refu zaidi Tanzania (Tazama picha namba 1).

Pia ndio daraja refu zaidi kupita yote Afrika mashariki na kati, na ni daraja la 6 kwa urefu Afrika nyuma ya madaraja marefu ambayo ni 6th October Bridge la Egypt lenye urefu wa 20.5 km, kisha Third Mainland Bridge la Nigeria lenye urefu wa 10.5 km, kisha Suez Canal Bridge la Egypt lenye urefu wa 3.9 km, alafu Mozambique Island Bridge la Mozambique lenye urefu wa 3.8 km, kisha Dona Ana Bridge la Mozambique lenye urefu wa 3.6 km.

2. Reli ya kisasa ya SGR...

Ujenzi wa reli ya SGR ni reli ya kisasa na ya kwanza Africa mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa (Tazama picha namba 2 na 3).

Reli hii itakapo kamilika itakuwa na urefu wa km 1395, ambayo mchaganuo wake kwamba, Awamu ya 1 Dae es Salaam–Morogoro (Km 300), Awamu ya 2 Morogoro-Makutupora (Km 422), Awamu ya 3 Makutupora–Tabora (Km 294), Awamu ya 4 Tabora– Isaka (Km 130) na Awamu ya 5 Isaka–Mwanza ( Km 249).

Reli hii itakapo kamilika itakuwa ndio reli ndefu (one network railway) kuliko zote Afrika, achilia mbali Afrika mashariki na kati.

Pia ndio itakuwa reli ndefu (one network railway) Inayo tumia ememe Afrika, Amerika ya kusini na Ulaya.

Nadhani hapa sijaeleweka, namanisha kuwa SGR hii ya Tanzania ndio reli ndefu kuliko reli yoyote Ulaya (zingatia neno reli ndefu ya mtandao mmoja "one network railway") hivyo hii reli ni alama kwa taifa letu na alama aliyotuachia hayati Magufuli.

3. Ikulu ya Chamwino...

Ujenzi na upanuzi wa eneo la ikulu mpya ya Tanzania inayojengwa Wilayani Chamwino mkoani Dodoma itakuwa na eneo lenye ukubwa wa ekari za mraba 80,473 sawa na kilometa za mraba 34, hii itaifanya Ikulu hii kuwa Ikulu yenye eneo kubwa kuliko Ikulu yoyote Afrika (Tazama picha namba 4 na 5).

Pia itakuwa ni Ikulu ya pili duniani itakayotumika (zingatia neno kutumika) kuwa na eneo kubwa nyuma ya Ikulu ya "Istana Nurul Iman" ambayo ina eneo lenye mkubwa wa 2,152,782 square feet (sawa na 200,000 m2).

Pia jambo la kuzingatia hapa ni kwamba Ikulu ya Chamwino ndio itakuwa Ikulu ya kwanza duniani itakayokuwa na mbuga ya wanyama ndani yake hii ni kwaba eneo lote la Ikulu litazungushiwa ukuta wenye urefu wa Kilometa 27, na ndani kutakuwa na mbuga ya wanyama na aina mbalimbali za ndege.

Hivyo itakuwa ndio ikulu yenye eneo kubwa ulimwenguni yenye hifadhi ya wanyama.

Hii itakuwa record mpya kwa nchi yetu na alama aliyoiacha Magufuli.

4. Bwawa la Nyerere (JNHS)...

Ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa maji wa Julius Nyerere Hydropower Station (JNHS) unaojengwa eneo la Stiegler's gorge katika mto Rufiji itakuwa ndio kituo kikubwa Tanzania cha kuzalisha umeme wa Maji (Tazama picha namba 6).

Bwawa hili litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2115, na kuwa bwawa la pili Afrika kwa uzalishaji umeme wa Maji nyuma ya bwawa la Grand Ethiopian Renaissance litakalo zalisha 6,450 Megawati.

Lakini jambo muhimu ni kuwa bwawa hilo litakuwa ndio bwawa kubwa kuliko yote Afrika mashariki na kati na la 9 kwa mkubwa duniani.

Maana yake ni kwamba, ukubwa wa bwawa hilo utakuwa ni kilomita 25 za upana, ukubwa huu utajaza maji yenye mita za mraba bilioni 34 ambayo yatalifanya bwawa hili kuwa ziwa la 4 kwa ukubwa Tanzania nyuma ya Ziwa Viktoria, Tanganyika na Ziwa Nyasa, kubwa kuliko ni kuwa litakapo kamilika litakuwa bwawa la tisa kwa ukubwa duniani.

Magufuli bus terminal....

Kituo cha mabasi maarufu kama Magufuli bus terminal ni moja ya vituo 5 bora vya mabasi Afrika, kituo hicho kinashika namba 2 baada ya kituo cha mabasi cha Oshodi Bus Terminal kilichopo jijini Lagos, Nigeria.

Kubwa hapa ni kuwa kituo hicho cha Magufuli bus terminal ndio kituo bora, cha kisasa na kikubwa kuliko vyote kusini mwa jangwa la sahara (tazama picha namba 7 na 8)

Hii ndio legacy ya vitu vikubwa ambavyo vinaingia kwenye record ya Afrika na duniani aliyoiacha Magufuli ambayo inaacha alama ya mvuto nchini Tanzania.

Kila chenye uzuri akikosi Ubaya, pamoja na hayo mazuri lakini utawala wake ndio unaotajwa kuwa moja ya tawala iliyo didimiza demokrasia na utawala bora nchini Tanzania.

Sasa basi.....

Swala la kuniuliza kwanini sijataja na hayo mabaya yake wala lisikuumize, hilo nakuachia wewe utaje na kuiridhisha nafsi yako ili itulie.

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu(CMCA)
Wednesdays-16/03/2022
MPANDA, KATAVI TANZANIAView attachment 2153108View attachment 2153107View attachment 2153111View attachment 2153110View attachment 2153109View attachment 2153112View attachment 2153113
FB_IMG_1647444453950.jpg
 
Back
Top Bottom