Kumuenzi Hayati Magufuli kesho naanza ziara rasmi kuelekea Chato!

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
14,163
16,158
Nitaanzia ziara yangu Chongoleani kwenye bomba la mafuta ghafi mkoani Tanga.

Nitakwenda Mererani halafu.

Nitapita daraja la mto Wami nitaingia Dar nitakwenda moja kwa moja na kupita barabara ya morocco nakumbuka jpm aliagiza pesa za sherehe ya sikukuu ya jamhuri, zijenge barabara hiyo.

Nitapanda mwendokasi huyo mpaka daraja la tanzanite, nikitoka hapo huyoo nakatiza daraja la kijazi mpaka airport naangalia zile ndege na terminal III.

Then huyo nakwenda Morogoro ndani huko mbuga ya Selous kwenye bwawa la nyerere nawalaani wale wote waliokua wanaweka kauzibe bwawa lisikamilike.

Nkitoka hapo napanda treni naelekea Mwanza, mpaka Ziwa Viktoria nakwenda kuangalia zile meli zetu zilizotengenezwa na kampuni ya songoro.

Nikitoka hapo napiga picha daraja la furahisha, nakwenda daraja la Magufuli .

Nikitoka hapo nakwenda burigi narudi airport nakwenda kaburini.

Napanda basi ili nifike kKtuo cha Magufuli Mbezi ziara itakua imekamilika na nitakua nimemuenzi hivyo mwana wa Afrika mzalendo wa kweli!

John Joseph Pombe Magufuli pumzika kwa amani Samia anakamilisha yale yote uliyoyaanza.
 
well done comrade,

ikikupendeza ntahitaji unijalie mainfrustructure ili nione namna tunaweza changia wala maji tu 🐒
 
Nitaanzia ziara yangu Chongoleani kwenye bomba la mafuta ghafi mkoani Tanga.
Nitakwenda Mererani halafui...
Duh huyu si alikuwa mbabe sana.

Kuna kipindi aliiba kura mpaka za serikali za mitaa. Ni nini unacho muenzi au unataka kumkwamisha mama yetu Dkt.Samia?
 
Back
Top Bottom