Mwaka 2018 DP World ilipigwa Marufuku Nchini Somalia na Mkataba wake kuitwa Batili na Usiotekelezeka

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1686131160704.png
Mwaka 2018, Somalia ilipiga marufuku kampuni ya bandari ya Dubai DP World kufanya kazi nchini Somalia, ikisema kuwa mkataba ambao kampuni hiyo ilitia saini mwaka 2017 na eneo lililojitenga la Somaliland ili kuendeleza eneo la kiuchumi ni batili na hautekelezeki

Bila kueleza kwa undani, Bunge la Nchi hiyo lilipitisha kwa kauli moja azimio la kupiga marufuku DP World kufanya kazi nchini humo kulisisitiza ushindani unaokua katika eneo la kimkakati la Pembe ya Afrika kuhusu uwekezaji wa kampuni ya bandari inayomilikiwa na serikali ya Dubai.

"Mkataba wowote uliotiwa saini na DP World ni batili na unapingana na katiba pamoja na kanuni ya uwekezaji wa kigeni nchini Somalia, na sheria nyingine za nchi. DP World ilikiuka waziwazi uhuru na umoja wa Somalia na hivyo DP World imepigwa marufuku kujihusisha na chochote Nchini Somalia," lilisomeka azimio hilo, ambalo liliidhinishwa na kuchapishwa na wakala wa serikali.

Hata hivyo, Serikali ya Somaliland ilikanusha madai ya upande wa Somalia ya kubatilisha makubaliano yaliyotiwa saini kati ya kampuni ya bandari ya UAE DP World na Serikali ya Ethiopia ya kupata asilimia 19 ya hisa katika Bandari ya Berbera.

Waziri wa Habari wa Somaliland, Abdirahman Abdillahi Farah, alisema katika taarifa yake kwamba serikali ya Rais Musa Behi Abdi ilifanya kazi ili kuhitimisha makubaliano na DP World na Serikali ya Ethiopia. na kuongeza kuwa Jamhuri ya Somaliland ni "huru na hairuhusu wengine kuathiri uhuru wake".

Ikumbukwe kuwa Bandari ndogo iliyopo Somaliland eneo la Berbera ambayo DP World ilisaini Mkataba wa kuiendesha, inasafirisha Ngamia hadi Mashariki ya Kati na kuagiza chakula na bidhaa nyingine nchini humo.

============

ia has banned Dubai ports operator DP World from operating in Somalia, saying that a contract that the company signed last year with the breakaway Somaliland region to develop an economic zone is null and void.

It is unclear how Somalia’s federal government could enforce the ban given Somaliland’s semi-autonomous status.

But parliament’s unanimous passing of the resolution banning DP World from working in the country underscored growing rivalries in the strategic Horn of Africa region over the Dubai state-owned port operator’s investments.

“Any agreement signed with DP World is null and void since it opposes the constitution, the rule of foreign investment in Somalia, and other rules of the country,” read the resolution, which was approved late on Monday and published by Somalia’s state new agency.

“DP World openly violated the independence and unity of Somalia and so DP World is banned from Somalia,” it said.

A spokesman for DP World did not immediately respond to a request for comment on Tuesday.

Somaliland’s small port of Berbera exports camels to the Middle East and imports food and other items.

It also provides some transport links for neighboring Ethiopia, a landlocked country that has friendly relations with the breakaway region.

Last month neighboring Djibouti ended its contract with DP World to run its Doraleh Container Terminal, citing failure to resolve a dispute that began in 2012.

Two days after the government canceled the contract, Djibouti’s ports and free zone’s authority accused DP World in a statement of using “aggressive tactics such as the deliberate slowing” of the development of Doraleh port “in favor of their main asset at Jebel Ali”, a major commercial port in Dubai owned by the company.

The company, one of the world’s biggest port operators, called Djibouti’s move an illegal seizure and said it had begun new arbitration proceedings before the London Court of International Arbitration.

DP World said last week it had signed a final agreement with Somaliland to develop the zone and expected to break ground in the 12 square km project later this year.

Situated at the northern tip of east Africa on the Gulf of Aden - one of the busiest trade routes in the world - Somaliland broke away from Somalia in 1991 and has been relatively peaceful since.

The region of 4 million people has not been internationally recognized but has recently attracted sizeable investments from the Gulf.

Last year Somaliland’s government agreed to allow the United Arab Emirates to build a military base alongside the Berbera port.
1686128374153.png
1686131160704.png

REUTERS 2018
 
Hao ni watoto wa Baba sio sisi. Pamoja na kupita misukosuko baina yao ila hawana ujinga huo.

Nimekumbuka kuna jamaa diaspora walileta wazungu toka Canada kuja kuchimba madini. Wasomali wazawa wakaweka biti.

Vijana wakachoma ndege ya wazungu na ndio ukawa mwisho wa mkataba.
 
Unatetea ujinga
Hao ni watoto wa Baba sio sisi. Pamoja na kupita misukosuko baina yao ila hawana ujinga huo.

Nimekumbuka kuna jamaa diaspora walileta wazungu toka Canada kuja kuchimba madini. Wasomali wazawa wakaweka biti.

Vijana wakachoma ndege ya wazungu na ndio ukawa mwisho wa mkataba.
 
Mkataba wa DPW na Tanzania nashangaa wanaoutetea, watu wanapiga kelele marekebisho ila wao wametia pamba masokioni tutakuja kugawana fito one day. Ibara ya 4(3) 6(2), 7(3), 23(4) ni za kitaahira hata hiyo ya 22 wanayojidai kuwa inaruhusu marekebisho ni changamoto
 
Uamuzi huo ulifanywa na upande mmoja uliojitenga (Somaliland) kupitia Azimio la Wabunge huku ukieleza Mkataba huo unapingana na Katiba, Kanuni ya Uwekezaji wa Kigeni na Sheria nyingine za Nchi
-
Taarifa ya Azimio la Bunge inasomeka "DP World ilikiuka waziwazi Uhuru na Umoja wa Somalia na hivyo DP World imepigwa marufuku Nchini Somalia,"
-
DP World ilisaini Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari ya Berbera, inayosafirisha Ngamia, Chakula na bidhaa nyingine. Hata hivyo, Mkataba haukuvunjika kutokana na Masharti yake kuwa magumu pamoja na upande mwingine wa Somalia kuutetea.

 
Back
Top Bottom