FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,063
- 40,724
Ilikuwa ni miaka takriban 13 Iliyopita, mwaka 2009, siku moja niliamka na kukuta nimechorwa alama hiyo ya kujiviringisha, na alama hiyo ilichorwa kwa kutumia kitu chenye ncha kali (nilihisi ni wembe), ambapo alama hiyo ilikuwa imechongwa juu kwenye dole gumba la mkono wa kulia, kwenye ile ngozi ya juu juu (dead skin).
Nilipoiona alama hii nilihisi labda niko usingizini naota, hivyo nikarudi tena kulala, ila nilipoamka ngoma bado ipo, bayana.
Niliogopa mno! Nikawa najaribu kukataa kwamba haiwezekani hiki kitu kimechanjwa mubashara kabisa kidoleni mwangu. Nilijiaminisha hii si kweli, ni ndoto tu, hata hata kama nashindwa kuamka usingizini. Baada ya siku kadhaa ile ngozi ya juu ilibanduka na alama ikapotea.
Ila hadi leo najiuliza, hii alama maana yake nini?