Mwajiriwa achana na staff wenzio baada ya muda wa kazi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,242
103,943
Leo nataka kuwapa ushauri waajiriwa. Malalamiko ya mishahara kutokutosha yamekuwa mengi, hasa kwa waajiriwa na Mama Samia.

Malalamiko yenu ni ya msingi kabisa. Lakini inabidi mjiongeze. Najua hata mkiongezewa mshahara shida ziko pale pale. Simaanishi msiongezewe, la hasha!!

Naona kuna tatizo mahali. Wengi wenu mna matumizi mabaya sana ya muda baada ya kazi. Tena wengine wanatumia vibaya hata muda wa kazi.

Unakuta mtumishi baada ya muda wa kazi unaendelea kuwa na kampani ile ile ya staff wenzio. Mnaendelea kujadili mambo yale yale ya kazini kwenu.

Stori ni zile zile za majungu, kutafuta machimbo mapya ya bata, kufukuzia mademu na kula bia. Au mnaendelea kujadili assignments za kazini.

Sisemi kwamba staff wenzio hawafai lah hasha, wawe basi wana jipya!

Mimi niliacha huu mtindo wa maisha zamani sana. Natumia muda wangu kufanya vilinge na watu wengine wanaoishi maisha mengine.

Kuna wakulima wakubwa na wadogo, kuna wafanyabiashara wakubwa kati na wadogo, kuna mama na baba ntilie, fundi magari baiskeli nk.

Hawa watu wana mambo mazuri sana, ukiyapata ukayafanyia kazi unaweza kutoka hapo ulipo.

Ni mwaka wa pili sasa nilianzisha utamaduni wa kwenda kuweka kituo kwa fundi magari na mitambo mmoja hivi ana akili nyingi sana.

Yule mzee alikuwa ananipa ideas nyingi sana kwenye fani yake, fursa za biashara na jinsi ya kupambana na changamoto zake.

Leo hii mambo ni tofuati kabisa, matokeo yake leo hii huwa nikirudi pale ananiongezea network na kukutana na wenzangu waliokuja kwa matengenezo tunatafakari pamoja.

Hii topic ni ndefu sana ila dhima ya uzi wangu ni kuwakumbusha waajiriwa kuacha kurundikana na staff wenzio baada ya muda wa kazi.

Ukishindwa kabisa baki nyumbani na mkeo mcheze kidali pooh.
 
Ushauri mzuri mkuu, nilikutana na kijana mmoja majuzi hapa, yeye ni mfanyabiashara, alinipa ushauri mzuri sana kuhusu uwekezaji kwa mtaji mdogo tu.
 
Leo nataka kuwapa ushauri waajiriwa. Malalamiko ya mishahara kutokutosha yamekuwa mengi,hasa kwa waajiriwa na Mama Samia. Malalamiko yenu ni ya msingi kabisa. Lakini inabidi mjiongeze. Najua hata mkiongezewa mshahara shida ziko pale pale. Simaanishi msiongezewe,la hasha!!
Nimekukubali leo Chawa wa Mo
 
Leo nataka kuwapa ushauri waajiriwa. Malalamiko ya mishahara kutokutosha yamekuwa mengi, hasa kwa waajiriwa na Mama Samia. Malalamiko yenu ni ya msingi kabisa. Lakini inabidi mjiongeze. Najua hata mkiongezewa mshahara shida ziko pale pale. Simaanishi msiongezewe, la hasha!!
Akili kubwa sana ila subiri wakuda waje
 
Back
Top Bottom