Kwani wiki nne hazijaisha? Siku za kukaa kazini ngapi ktk wiki? Mtu kaamua tu kuleta thread isiyo na tija!
wiki nne zimekwisha tarehe 04. Huyu na wana ccm wenzake waliokuwa wanajisifia hapa kuwa wamekuja kukomesha upinzani alidhani amepata kitu cha kuhamisha nguvu za mjadala wa watu hapa na kumbe akajikuta anapata aibu ya mwaka.
kuna mtu alishauri watu waende shule kwanza kabla hawajaleta propaganda zao hapa. Nia yake ni kutaka watu wajadili vitu kama hivi badala ya kujadili mambo ya BoT, kiwira, iptl, report ya EPA, report ya kamati ya madini, kifo cha Ballali, buzwagi na mengine mengi.
Kama nilivyomshauri Bubu ataka kusema jana kuwa asihangaike na watu kama hawa wala kujaribu kuwafungia au kufunga thread zao. Watu kama hawa wape muda tu na wataanza kujiabisha wenyewe kama huyu hapa alivyopata aibu ya mwaka.
Na hii thread inabidi ikae hapa kwenye siasa ili azidi kuaibika vizuri.