Mwafrika wa Kike mwezi una siku ngapi?

Status
Not open for further replies.

Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
Kwani wiki nne hazijaisha? Siku za kukaa kazini ngapi ktk wiki? Mtu kaamua tu kuleta thread isiyo na tija!

wiki nne zimekwisha tarehe 04. Huyu na wana ccm wenzake waliokuwa wanajisifia hapa kuwa wamekuja kukomesha upinzani alidhani amepata kitu cha kuhamisha nguvu za mjadala wa watu hapa na kumbe akajikuta anapata aibu ya mwaka.

kuna mtu alishauri watu waende shule kwanza kabla hawajaleta propaganda zao hapa. Nia yake ni kutaka watu wajadili vitu kama hivi badala ya kujadili mambo ya BoT, kiwira, iptl, report ya EPA, report ya kamati ya madini, kifo cha Ballali, buzwagi na mengine mengi.

Kama nilivyomshauri Bubu ataka kusema jana kuwa asihangaike na watu kama hawa wala kujaribu kuwafungia au kufunga thread zao. Watu kama hawa wape muda tu na wataanza kujiabisha wenyewe kama huyu hapa alivyopata aibu ya mwaka.

Na hii thread inabidi ikae hapa kwenye siasa ili azidi kuaibika vizuri.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
wiki nne zimekwisha tarehe 04. Huyu na wana ccm wenzake waliokuwa wanajisifia hapa kuwa wamekuja kukomesha upinzani alidhani amepata kitu cha kuhamisha nguvu za mjadala wa watu hapa na kumbe akajikuta anapata aibu ya mwaka.

Naona watu wa spin mnataka kulazimisha kuwa mwezi ni wiki nne, haya twende kwenye hesabu labda ndio mtaelewa manpokosea.
kama mwezi ni wiki nne mwaka una siku ngapi?

Miezi 12 kila mwezi una wiki 4 Na kila wiki ina siku saba 7: 12 * 4*7 = 336

Kwa hiyo wenzetu nyinyi mwaka wenu una siku 336!

Halafu wakati mwingine mnapojibu swali lisomeni vizuri kwanza kabla ya kukurupuka, swali ni kwani mwezi una SIKU ngapi, swali halikuwa mwezi una WIKI ngapi.

Spin zimetawala mwenendo wako MGAYA unapaswa kujirekebisha, unaweza kuonyesha post yoyote niliyosema mimi ni mwana CCM au niliyojisifia kuwa nimekuja kukomesha upinzani?
 
Ni wapi MWK aliposema kuwa anaongelea mwezi wa siku na sio mwezi wa wiki? wewe umeuliza swali lakini baadaye kwenye post yako nyingine ukasema kuwa MWK hakusubiri mwezi upite ndiyo amkosoe Kikwete.

Wewe ndiyo ulitakiwa kusoma alichoandika MWK kabla ya kuanzisha thread ambayo imekuumbua na kukuaibisha hapa.
 
Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
Sina matatizo na kubadilisha maamuzi. Siku yoyote mtu yeyote akigundua amefanya maamuzi yasiyo sahihi vi vyema kubadilisha ili aanze kufanya yale yaliyo sahihi. Tatizo langu ni pale maamuzi hayo yanapokuwa ni ya kuwapa mawazo watu wengine au ni kwa manufaa ya umma kama ilivyo hapa JF. Mtu anapofanya maamuzi na akaueleza umma maamuzi yake na pengine kuwashawishi baadhi ya watu wamuunge mkono kwa uamuzi wao huo basi ni JUKUMU la mtu huyo kuwaarifu umma kuwa AMEBADILI uamuzi. MWK amekuja na thread ya kumuomba Rais ajiuzuru na amelikwepa jukumu lake la kuwakumbusha wasomi wa thread hiyo kuwa hapo awali aliandika maelezo tofauti juu ya swala hilohilo.

Lengo la thread hii ni kukumbushana MAJUKUMU tuliyo nayo katika kuelemisha jamii.Tukiacha mapengo kama haya tunakuwa sio waelimishaji bali ni wana propaganda - spin masters!

Tujiweke katika nafisa ya wale walioamua kuungana na MWK kumpa Rais mwezi mmoja kama alivyoandika halafu kabla mwezi haujaisha tunaona haya aliyoandika tena, bila kugusia kile alichoandika awali - je tungemfikiriaje MWK?

kama umesahau, haya ndiyo umeandika hapa kwenye hii thread. Umeanza mashitaka na sio swali kama ulivyoanza.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,875
2,000
Ze Marcopolo, ingawa siko kumtetea Mwafrika wa Kike, naamini kuwa pale 08 May 2008 alipotoa duku duku lake alikuwa na hiyo dhamira ya kumpa muungwana hiyo moratorium ya mashambulizi kwa mwezi mmoja. Hata hivyo, kwa kuwa dada Mwafrika wa Kike akagundua, ebo mbona huyu ninayempa pumzi ajirekebishe mbona hajaafanya chochote cha maana, ilipofika 05 Juni 2008 akaamua kumfungia kazi. Kumbuka, Mwafrika wa Kikenaye ni binadamu ana uhuru wa kubadilisha mtazamo pale anapojisikia, kama mwanasiasa mahiri Harold Wilson anavyotukumbusha hapa chini:

"He who rejects change is the architect of decay. The only human institution which rejects progress is the cemetery" - Harold Wilson

hata hivyo hapajaharibika neno.Mwafika kaona hapana jamaa anazidi ku bore akaamua kuingia nuke sasa kuna ubaya hata kama siku zilibakia chache ili mwezi ufike ?
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,006
2,000
Ni wapi MWK aliposema kuwa anaongelea mwezi wa siku na sio mwezi wa wiki? wewe umeuliza swali lakini baadaye kwenye post yako nyingine ukasema kuwa MWK hakusubiri mwezi upite ndiyo amkosoe Kikwete.

Wewe ndiyo ulitakiwa kusoma alichoandika MWK kabla ya kuanzisha thread ambayo imekuumbua na kukuaibisha hapa.

Hivi kumbe kuna mwezi wa wiki na mwezi wa siku!

Kujadiliana na wewe Mgaya ni kupoteza muda, upeo wako ni mdogo. Nasikitika kukwambia hivyo.
 
Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
hata hivyo hapajaharibika neno.Mwafika kaona hapana jamaa anazidi ku bore akaamua kuingia nuke sasa kuna ubaya hata kama siku zilibakia chache ili mwezi ufike ?

Lunyungu,

MWK yeye amesema kwenye ile thread kuwa wiki nne zimepita kwa hiyo mwezi umekwisha. ukiangalia hata kwenye ile thread ya count down ya report ya madini, MWK alihesabu wiki 12 kuwa ni miezi mitatu aliyotoa Kikwete.

Zemarcopolo alikimbia hapa akidhani kuwa ana hoja kumbe amekumbana na aibu ya mwaka. Ni vizuri kusoma kabla ya kuandika ila inaonekana mwenzetu unazi umemjaa hata hawezi kupata muda wa kusoma.
 
Mgaya

JF-Expert Member
Oct 1, 2007
519
0
Hivi kumbe kuna mwezi wa wiki na mwezi wa siku!

Kujadiliana na wewe Mgaya ni kupoteza muda, upeo wako ni mdogo. Nasikitika kukwambia hivyo.

Je ni makosa kusema kuwa mwezi una wiki nne? MWK ndiye kwa ridhaa yake mwenyewe alitoa hicho kipindi cha mwezi mmoja (bila kutaja tarehe ya kumaliza au kama ni mwezi wa wiki nne au siku thelathini). Kama yeye mwenyewe amehesabu mwezi wake na ukaisha baada ya wiki nne kuna makosa katika hilo?

Kuhusu wewe kuongelea upeo wangu sikushangai, watu wakiishiwa hoja au kukosa majibu huanza kuongelea vitu vingine visivyohusika.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,208
2,000
Naomba niulize hivi: hivi miezi yote ina siku sawa? na Bi. Mdogo aliposema mwezi kwanini tumechukulia ule wenye siku 31 na siyo wenye 28/29 na yote ni miezi? Je kama katika mawazo alikuwa anachukulia mwezi wenye siku 28 tutasema mwezi wake ameuhesabu vibaya.. na kama amechukulia wa siku 31 tutasema ameupendelea? Kimantiki najikuta kulazimika kuamini kuwa kama siku zote ambazo amehesaba zisingepungua 28 na zisingezidi 31.... na bado angekuwa sahihi kwenye maana ya "mwezi"...
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom