Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,097
- 43,309
Well, kuna wakati inabidi tuseme tu kuliko kuzungushana kwenye huu utando wa buibui wa ufisadi. TUmekuwa kama kumbikumbi, na kama vipepeo tumenaswa na wao wanatuchezea tu.. kama paka aliyeshiba anavyomchezea chezea panya aliyechoka kukimbia!
Sasa naomba tulimalize hili la Richmond/Dowans:
Then, tutaangalia haya mengine, haya mambo ya kuzugana kwa kweli wakati mwingine inabidi tukubali tu yaishe!
Sasa naomba tulimalize hili la Richmond/Dowans:
a.) Bw. Gire aachiliwe kwani tayari tunanyajua kampuni yake ilikuwa feki na kama maelezo ya jana yana dalili yote "upepelezi bado unaendelea". Sasa huu upepelezi wa miaka mitatu nadhani unatosha, na kwa vile hakuna ushahidi (msiniulize kwanini walimfungulia kesi kama hawakuwa wamekamilisha upepelezi au walikuwa wanakaribia kuukamilisha).
b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?
Sasa tumefikia kamati mbili za Bunge, Wizara, na wengine tunaanza kurushiana utadhani Taifa zima linacheza "Ready". Mara mpira huku, mara kule, huku mafisadi wanakwepa katikati wakiendelea kujaza chupa yao mchanga wa utajiri wa nchi yetu!, so why not just buy them, wapeni hizo fedha (kwani zipo nyingi tu). Tulimalize?
c.) Kwa vile hakuna mtu mwingine atakayepelekwa makahamani kwani muda unapita na mwisho mambo ya statutes of limitations inaweza kuingia kwenye baadhi ya mashtaka, kwanini tusiamue tu kusema "screw it" wameshajiuzulu watu (wakapewa mafao yao) na Richmond haipo tena.. so tulifunge tu.
Kimsingi, hatuwezi kulimaliza hili la Richmond na Dowans isipokuwa kwa kufuta hii kesi moja, kununua mitambo ya Dowans, kuwalipa kina Rostam na washiriki wake, halafu tumaliize yaishe. Hatuwezi kama taifa kuendelea kupiga kambi kwenye hili bonde la kashfa miaka nenda rudi. Hili la Dowans tulimalize, tujue limekwisha kuliko kuzunguka zunguka utadhani watoto wanaocheza "ukuti ukuti!"b.) Mitambo ya Dowans hatimaye tutainunua kwa vile tunapaswa kuinunua kwani kutoinunua haiingii akilini wakati "ipo tu pale"! Mitambo hii haiendi kwa mtu yeyote binafsi na matatizo ya umeme yanayokuja mwezi wa nne itakuwa ni ushahidi kuwa ni "bora" tuinunue tu!. So why not buy them!?