Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
Mvua hiyo kubwa imenyesha leo katika Manispaa ya Bukoba na kuwaachia hasara kubwa wananchi wengi hasa walio karibu na mto Kanoni.
Nyumba nyingi zimezingirwa na maji, huku maeneo mengine nyumba zikiwa zimeezuliwa paa kutokana na upepo mkali.
Moja ya nyumba ya ibada iliyopata madhara hayo ni Kanisa Katoliki Parokia ya Rwamishenye ambayo paa limeezuliwa huku waumini wakiwa wanasali Rozari Takatifu
Pia baadhi ya mazao yameharibiwa vibaya na mvua.
TANESCO mkoa wa Kagera imetoa hadhari kubwa kwa wananchi kuwa makini na miundombinu ya umeme na kuwataka kutoa taarifa endapo wataona nguzo ya umeme iliyoanguka.