Dar: Mvua kubwa sana imenyesha usiku wa kuamkia leo 21/01/2024

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,838
18,250
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha hapa Dar sijapata kuona. Tangu nizaliwe sijawahi kushuhudia mvua kubwa kiasi hiki.

Serikali ijiandae kukabiliana na athari za mafuriko zitakazosababishwa na mvua hii kwani kadri muda unavyoenda mvua inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilingo'a madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarajie baada ya mvua hii.

Pia soma: Mvua ilivyoacha maumivu mmoja adaiwa kufa Dar

UPDATES

*Mawasiliano kati ya Tegeta na Kunduchi yamekatika baada ya daraja la Kunduchi-Mtongani kukatika. Magari, nyumba na mali za raia zimesombwa na maji. Nguzo za umeme zimeanguka na baadhi ya raia wamefariki. Tatizo watu wamejenga karibu na mto kwa kupewa vibali na maofisa ardhi wa Serikali.

*Hadi sasa mvua inaendelea kunyesha baadhi ya maeneo hapa Dar. Serikali itoe tahadhari kwa wananchi na ichukue hatua kukabiliana na mafuriko.

*Serikali inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu na hasara iliyojitokeza. Madhara ya mafuriko haya mpaka sasa ni kama unavyoyasikia kutoka kwenye rekodi hapo chini iliyoripotiwa na Radio One Stereo. Katika rekodi hii utamsikia mwananchi akilalamika kupoteza Tsh 5,000,000 ambazo zote zimesombwa na mafuriko. Hakufanikiwa kuokoa hata shilingi moja.

* Nyumba 7, magari na mali za wananchi zimesombwa na maji, mtu mmoja amefariki na madaraja kadhaa yamevunjika na kukata mawasiliano ya barabara.

*Raia mmoja ameokota gari lillilosombwa na mafuriko lakini watu wenye roho mbaya wamemzuia kulichukua.

*Wakandarasi wanaendelea kuzibua barabara zilizozibwa na maji, mawe na magogo ili kurejesha mawasiliano.

Nitaendelea kuwapa updates na picha kadri nitakavyozipata.........
 
Attachments

  • Record-4.wav
    19.2 MB
Kuna nabii alitabiri, Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu, itafunikwa na maji, kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho. Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu. Ila walio wengi waliposikia unabii huo, walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii, bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
 
Kuna nabii alitabiri,Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu,itafunikwa na maji,kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho.Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu.Ila walio wengi waliposikia unabii huo,walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii,bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!
Achana na hao matapeli
 
bunch of Bullshit
 
Yule nabii alisema tuuze nyumba.
Sasa tuko Dar tuuze nyumba kukimbia maafa tuwauzie MBUZI?
Kati ya kuuza nyumba na kuomba kuzuia kipi ni rahisi?
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha mahali hapa sijapata kuona. Haki tabgu nicakiwe sijawahi kushuhusia mvua nyingi kiasi hiki.

Srtikali ijiandae kukabiliana adhali za mafuriko zitakazsababishwa na mafuriko haya. Kadri muda unavyoenda inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilibgoa madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarsjie baada ya mvua hii.

Nawasilisha.
sasa ndugu nabii hiyo mvua inanyesha au itanyesha usiku?

au ni katika ulimwengu wa Roho maana ndo naingia Misa ya kwanza na ni pakavu sana hapa vikindu 🐒
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja. Mvua kubwa sana inanyesha mahali hapa sijapata kuona. Haki tabgu nicakiwe sijawahi kushuhusia mvua nyingi kiasi hiki.

Srtikali ijiandae kukabiliana adhali za mafuriko zitakazsababishwa na mafuriko haya. Kadri muda unavyoenda inazidi kuongezeka

Mara ya mwisho mvua iliponyesha ilibgoa madaraja na kuua watu watatu. Safari hii tujiandae kwa maafa zaidi.

Tuambie mahali ulipo hali ikoje na nini tutarsjie baada ya mvua hii.

Nawasilisha.
Hapa kwangu ndiyo inaanza sasa hivi! Inataka tusiende Kanisani? Hebu nayo iache kiherehere!
 
Kuna nabii alitabiri,Dar kufikia mwezi Mei mwaka huu,itafunikwa na maji,kwamba kuna Tsunami itaipiga Dar.
Huenda hizi mvua ni maonyo ya mwisho.Watu wa Mungu watamuuliza Mungu ukweli wa unabii huu.Ila walio wengi waliposikia unabii huo,walimdhihaki mtoa unabii.

Biblia inasema "msiutweze unabii,bali zipimeni roho kama zimetokana na Mungu au la!

Swala la kutoelewa manabii halina wa kumlaumu, hao manabii wenyewe ndo wanafanya tusiwaelewe, reference : Joshua. TB
 
Back
Top Bottom