Augustine Moshi,
Ama kweli kuna wakati chongo huitwa kengeza! Mimi sioni tafsiri ama maana nyingine ktk maneno hayo hapo juu! Ebu tusome tena upyaaaa!
Serikali ya awamu ya nne iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete (JK) imefanikiwa kujenga shule mpya za sekondari 381 nchini kote ndani ya kipindi cha miezi minne tu tangu Januari hadi April mwaka huu.
Sasa ikiwa waona ajabu na kutaka kumpa sifa Mkapa mbona mabaya wamwangushia JK?....
Iwapo pongezi za ujenzi wa shule hizi anastahili Mkapa kwa sababu unaamini zimejengwa toka wakati wa Mkapa ama ni moja ya sera zake basi hata kodi pia zinakusanywa na wananchi walewale aliowaajiri Mkapa ktk mfumo ama sera zilezile za ukusanyaji aliouacha Mkapa!
Augustine, Kuna issue moja kuhusu Elimu nataka sana kuizungumzia.
Wenzetu nchi za magharibi wanaposema ELIMU kuwa msingi wa maendeleo huwa wanamaanisha ELIMU kuwa kitovu cha uzalishaji! na wasomi ndio WAAJIRI... kwa maana hii huwezi kupata liseni Ulaya ya kuendesha hata Kigereji cha magari mabovu, ususi wa nywele na kadhalika kama huna cheti cha ELIMU ya ufundi huo. Karibu kila biashara inayohusiana na ELIMU lazima tajiri awe na ELIMU yake hata iwe udalali wa nyumba. Naposema Tajiri nina maana mtoa ajira sio utajiri wa fedha maanake hata jambazi linaloondoka solo linaweza kuwa tajiri vilevile.
Kwa hiyo kinachonishangaza mimi huko nyumbani biashara zote zinazotakiwa ELIMU zimeshikwa na mtu yeyote mwenye fedha! Hotel za kitalii, Hospitali nahata vyakula vya makopo maadamu huyo tajiri awe ameajiri wafanyakazi wenye elimu hiyo. Hapa fedha zimezidi nguvu kabisa ELIMU kwani msomi na elimu yake hana sauti kwa mwajiri hata kama elimu yake ndiyo inayoendesha biashara!.. hakuna deal linaloweza kuendeka hapa kati ya msomi na mwenye mali.
Kusema kweli sioni tunakokwenda na Elimu ikiwa hakuna sheria ama system ambayo itaweza kumtajirisha msomi (esp. University na College) ktk fani yake. Nachoona mimi watu wanasoma ili wapate kutafuta ajira inayolipa na sio kwamba serikali yetu imeandaa mikakati ambayo itamwezesha msomi mwenye record nzuri kuanzisha kimradi chake...Na matokeo ya kuajiriwa hasa kwa wasomi mara nyingi hayana tofauti na Ujamaa..msomi hukosa uchungu pale mali sii yake na mara nyingi utawakuta wakipiga mahesabu!.. kazi niifanye mimi anayetajirika mtu mwingine!
Kwa kuondoa vitu kama hivi wenzetu nchi za nje serikali zao zimejitahidi sana ktk kukuza biashara ndogondogo kwa kuwapa miyaji (kupitia benki) nafuu ya kodi pia uwezo wa kuendesha biashara za ufundi lazima ziwe na shahada laa sivyo kauze embe na kahawa sokoni!..
Ebu tujiulize ikiwa sisi tunapewa fedha na benki kuu ya dunia kwa sababu tu tunaonyesha uwezo mzuri wa kujenga nchi inakuwaje viongozi haohao wanashindwa kuona upande huu na kuelewa kwamba maendeleo ya nchi nzima huanzia kwa watu wake (wazawa) na sio kuwa na miradi mikubwa chini ya wageni!